Deal ya Ali Kiba na Sony: Makosa yanayojirudia..

Deal ya Ali Kiba na Sony: Makosa yanayojirudia..

Hii thread haijaandikwa kwa mahaba ya uteam yoyote ile!! Nimeongea uhalisia ulivyo
Mrengo wako unajulikana hata uandikeje kashasaini ningekuona wa maana ungekuja na way forward sio malalamiko kibao binadamu yoyote anayewaza Ku feli kabla ya kufanya jambo ana matatizo in real life kwanini utumie mfano wa waliofeli na sio kufanikiwa hii ndo akili ya baadhi ya majority wa kitizii kuwaza kufeli kabla ya kufanya jambo ua among them
 
Pale mbongo anapoleta ujuaji hata kwa vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wake..acha kukariri ungeishia kumpongeza tu wala usingepungukiwa chochote ila umezunguka wewe ukikebehi kwa dili alilosaini afu unamalizia kwa kusema unampongeza si unafiki huo
Mleta mada autonaturally ni team dimondi...
 
Mrengo wako unajulikana hata uandikeje kashasaini ningekuona wa maana ungekuja na way forward sio malalamiko kibao binadamu yoyote anayewaza Ku feli kabla ya kufanya jambo ana matatizo in real life kwanini utumie mfano wa waliofeli na sio kufanikiwa hii ndo akili ya baadhi ya majority wa kitizii kuwaza kufeli kabla ya kufanya jambo ua among them
Usitoke povu sana bibie, hebu slo mo kidogo..

Ni hivi, binadamu unatakiwa ujue kujifunza kutoka kwa makosa ya wengine, usisubiri mpaka ufanye makosa mwenyewe, itakula kwako!! Hiyo ndio akili ya maisha.. So nimejaribu ku-highlight vitu kadhaa kiba ajifunze kwa wenzake waliofanya makosa tayari ili yeye achukue tahadahari
 
Nani aliyeponda bibie!! Nimetoa angalizo achukue tahadhali wenzake wamepotea baada ya kujiassociate na hao watu.. Alafu watu gani hao wa insta wamepoa??? Team simba??? Hahahahah inaonekana huwajui hao jamaa
Kupotea kwa wasanii sidhani ka eti kulisababishwa na Ku sign contract kuna vtu vingi tusiwasingizie hao son music hu change na huita creativity kubwa, efforts hata ung"are vipi msanii mda ukipta ndo basi tena
 
Usitoke povu sana bibie, hebu slo mo kidogo..

Ni hivi, binadamu unatakiwa ujue kujifunza kutoka kwa makosa ya wengine, usisubiri mpaka ufanye makosa mwenyewe, itakula kwako!! Hiyo ndio akili ya maisha.. So nimejaribu ku-highlight vitu kadhaa kiba ajifunze kwa wenzake waliofanya makosa tayari ili yeye achukue tahadahari
Una changanya madesa kwahyo we we ukifeli jambo na mwingine lazima afeli simply kwa kuwa kuna waliofeli loh hyo poor thinking kwanini utumie reference ya failures ingekuwa hivo watu wasingefanya mambo maishani.
 
Bro lets not get there kuhusu hiyo video maana nikitoa maoni yangu utaniona hater!! Tujadili mkataba wa Sony, meneja Seven kamshauri msanii wetu vibaya... Hata fika popote na Sony, awe makini sana, sony wana record nzuri sana ya kuwapoteza wasanii kwenye ramani ya mziki
Hata akipotea sio mbaya kwa kua sio mara ya kwanza kiba kupotea na kurudi alishakaa kimya mpaka tukamsahau na mwisho amerudi kama mfame
Mwache azidi kupotea bold mbona una uchungu nae sana kwani ndugu yako bongo hii hatuna msanii wa kimataifa ni ujanja ujanja tu na ushetani
 
Wabongo inatubidi tubadilike sana tuwe na critical mind mleta mada kaleta kitu ambacho kinaweza kukusaidia kupanua ubongo wako kwa namna moja au nyingine critical questions ndo znaitajika hapa sio ushabiki tu mtapotea lakin najua hum tupo watu tofauti wenye uelewa tofauti ndo mana wengine kazi yao ni kuongea pumba tu siku iishe.
 
Mrengo wako unajulikana hata uandikeje kashasaini ningekuona wa maana ungekuja na way forward sio malalamiko kibao binadamu yoyote anayewaza Ku feli kabla ya kufanya jambo ana matatizo in real life kwanini utumie mfano wa waliofeli na sio kufanikiwa hii ndo akili ya baadhi ya majority wa kitizii kuwaza kufeli kabla ya kufanya jambo ua among them


jaman mungu wangu hivi unaweza kuwekeza kwenye kitu bila kufikiria athari zake na madhara yake hii kali.....
 
Hata akipotea sio mbaya kwa kua sio mara ya kwanza kiba kupotea na kurudi alishakaa kimya mpaka tukamsahau na mwisho amerudi kama mfame
Mwache azidi kupotea bold mbona una uchungu nae sana kwani ndugu yako bongo hii hatuna msanii wa kimataifa ni ujanja ujanja tu na ushetani
Haahahaa eden kimaro hapana mkuu!! Sina undugu na kiba wala sina uchungu nae, but hapa ni JamiiForums where we dare to talk openly.. Najaribu kuangalia tu hili suala kwa jicho la tatu
 
Kifupi kinachombeba msanii ni kipaji na ubunifu wake afu ndio vingine vinafuata,so Kiba awe zaidi ya makini sasa hv maana wale ni wafanyabiashara,atapewa vyote lkn asipoonesha ubunifu basi hawatakubali kuingia hasara.
 
Nadhani haikuwa busara kuwa na haraka ya kuuponda mkataba wa mtu kabla hujauona au kabla hujaona utekelezwaji wake.
Inawezekana wengi hawajui namna Sony Music inavyofanya kazi kwa wasanii, yenyewe pamoja na mambo mengine inashughulika zaidi na market ya product ya msanii.
Kila msanii aliye chini ya Sony Music anabaki na Management yake ya msingi pamoja na wao, kwa maana Alikiba kuendelea na Rocstar4000 huku akiwa na Sony Music.
Kama alivyo Drake aliye kwenye Sony Music lakini bado yuko na Management yake ya msingi ambayo ni Young Money.
Kingine ambacho nadhani wengi hawakuwa wakikifahamu ni kwamba Sony Music ina mikataba ya aina kadhaa, kulingana na uwezo wa msanii husika.
Ndio maana kila mkataba wanaosaini na msanii huwa ukitajwa jina lake kabisa, kwa hiyo unaweza kufuatilia wasanii hao na utaona tofauti hiyo.
Kuna mkataba ambao wao huwa hawajikiti sana katika maandalizi ya product na kubaki katika kutafutia soko kubwa zaidi product hiyo.
Na kuna mkataba wa pili wa kushiriki kuanzia maandalizi ya product ya msanii hadi kwenye kutafutia masoko.
Alikiba na AKA (Aliyeimba na Nassib) wote wako chini ya Sony Music ila mikataba yao inatofutiana, mkataba wa Alikiba unafanana kila kitu na mkataba wa Davido.
Ni mkataba unaoanzia katika maandalizi ya product ili kuipa thamani zaidi, pia kuwaunganisha wasanii wa label yao kufanya kazi za pamoja (collabo).
Katika hafla iliyofanyika February (kama sikosei) mwaka huu mjini Lagos wakati wa uzinduzi wa ofisi za Sony Music za Lagos, bosi wa Sony Music alisema kwa sasa wanajikita zaidi kwa soko na product za Afrika.
Na ndio maana hata hafla ya Alikiba kusaini nao mkataba kuwa kubwa sana na kuoneshwa live Africa nzima kwenye runinga na mtandaoni.
Naona hapa umetolewa mfano kwa kutaja wanamuziki wachache wenye mkataba na Sonny Music ambao kwa sasa wamefifia.
Lakini nashangaa haikusemwa kama karibu wasanii wote waliotajwa hapa waliyumba baada ya kuharibika kwa uhusiano wao na management zao za msingi.
Kama tatizo la Nakaaya lingekuwa ni Sony Music, basi tungekuwa tukimsikia hata hapa nchini. Ina maana hamjui kama tatizo la Nakaaya lilisababishwa na mgogoro wake wa mapenzi na bosi wa TBL?
Au kama ilivyo Destiny's Child ambao wako Sony Music lakini wamefifia baada ya kuyumba kwa management yao ya msingi iliyokuwa chini ya Mzee Knowles.
Ieleweke kwamba Sony Music ndio label kubwa kabisa ulimwenguni, ina wasanii toka mabara yote ulimwenguni na imetoa mafanikio makubwa kwa wasanii mbalimbali.
Na isidhaniwe kwamba kila msanii anaweza kuchukuliwa tu na label hii na kusimamiwa, wanaangalia uwezo ili kulinda hadhi ya Sony Music.
Kwa maana hiyo Alikiba aliiridhisha Sony Music kwa kipaji na uwezo wakena kumchukua na kuwekeza kwake.
Ieleweke, kila label kubwa haichukui msanii ovyo na kumpa mkataba mkubwa hadi ijiridhishe na uwezo wake, coz kuna hela nyingi zitawekezwa kwa ajili yake, iwepo imani ya pesa kurudi.
Hivi ni nani anajua maendeleo ya ile deal ya Diamond na Rais wa zamani wa Def Jam? Ambaye aliunganishwa na JK mwaka juzi akiwa Marekani.
Miaka miwili sasa imepita sasa tangu wakutanishwe na bado mkataba haujasainiwa, maana yake bado kuna kazi ya kujiridhisha kama kuwekeza kwake kutaleta faida au lah? Hakuna kubebana katika label kubwa.
Kila mtu anayejua music kama shabiki wa kweli, anajua umuhimu wa kuwa na label itakayoshughulikia soko la nje ya maeneo unayoishia msanii husika.
Na ndio maana hata Diamond amesaini mkataba na Upfront & Personal ya Nigeria ambayo licha ya kutokuwa worldwide lakini sihaba endapo itamsaidia kupenya Nigeria.
Hata Chadema licha ya uimara wao katika siasa za upinzani, lakini walimchukua Lowassa aliyesaidia wafike ambako awali hawakuweza kufika na wakaichukua Arusha na Dar es Salaam kwa kishindo.
Watanzania tujifunze kuwapongeza wenzetu waliopata mambo mazuri, huu ujanja ujanja wa kukwepa kutoa pongezi na kuanza kupotosha mambo hakusaidii wala kumnyima aliyepata.
Ina nadhani kama wengi wetu tungepata muda wa kutazama live ile hafla na kusikia wahusika wa Sony walivyoongea kusingekuwa na upotoshaji huu.
Kupitia mkataba huu Alikiba atapata mambo mengi makubwa na mazuri.
Hongera Alikiba, Mungu anakupenda sana.

Ova
 
Na nyie mwe wasanii msaini makampuni makubwa yatakayo wasaidia. Hicho ni kipaji chake na ana uhuru wa kukitumia atakavyo.... fanyeni yenu naye kafuataa njia yake.
Kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake sasa nawewe unayeponda au kushabikia bila maslahi binafsi shauri zako mwenzako anapata angalau chochote ili wanawe wanywe hata chai.
Tujafilini mambo ya bunge ya wasanii hayatuhusu
 
Back
Top Bottom