Dear Mama, Can you Offer An Unconditional Amnesty to All Zanzibaris Waliokimbia After Revolution, Incl Sultan, Be Free to Return & Start Afresh?

Kwanini usiwaombee wale waliotimuliwa na ben mwaka 2001 waliokimbilia kenya?
 
..Kuna jamaa mmoja Muarabu yuko hapa JF aliwahi kudai kwamba Waarabu walifika Zanzibar kabla ya Waafrika. Kwa hiyo akawa anadai kwamba Zanzibar sio ya Waafrika.

Alithibitishaje madai yake au yanaendelea kuwa madai yasiyothibitishwa?
 
Ukiona hivyo huyu Sultan amemtumia kitu kidogo ndugu yetu aanze kutengeneza mazingira kama anavyofanya kwa akina Halima Mdee
 
Paskali, kwani wameomba kurudi?
Na anayerudi akitaka kiti chake cha usultani je?
Tusiichokoze historia iliyokuwa ya mabwana na watwana.
 
Ukiona hivyo huyu Sultan amemtumia kitu kidogo ndugu yetu aanze kutengeneza mazingira kama anavyofanya kwa akina Halima Mdee
Wasitake kuturudisha kule tulikotoka , enzi za ubaguzi, enzi za watwana, wakwezi na mabwana na waungwana.
Hatutaki kurudi kule.
Tatizo wengi humu ni wa watoto wadogo hata kama wana miaka 45 au 50.
Sisi wengine tumeona adha ya mapinduzi 1964, watu kuchinjana na kuuana kwa sababu ya ubaguzi(yaliyofuatana na maasi ya jeshi, KAR)
Hali ile ilikuwa inatisha.
Tuteme mate chini
Su... tusirudi huko kamwe.
 
P, hili bandiko umeandikiwa au umeandika mwenyewe itnandula?
 
Pasi, tujadili uhalisia na is influence ama here-feel facts...,unajua usichamganye influence ya mtu kuwa rais wa JMT na u-Zanzibar wa SSH. Yeye angali ni rais wa JMT na sio rain wa SMZ! Hayo mambo mwachie Hussein Mwinyi na Baraza lake la mapinduzi kama lipooo....,kumbuka Komando alishalitolega kauli jambo lile....,then kumbukaa kuzaliwa makunduchi na kukaa kizmkazi haihalalashi na kuwa rais wa JMT haiharalishi maamuzi yake, kubali kataa zenj wanakuaga na mambo Yao ya kizenj zenj, yeye hana mamlaka hayo on paper....unayaona kwa kofiaa ya njee tu ya urais wa JMT.
 
Journalist mbona unatuangusha? Seyyid Said hakuwahi kuiachia Oman na Muscat. Alichokifanya ni kuhamishia makao makuu ya himaya yake yote Zanzibar. Kwa sababu hiyo aliendelea kutawala Oman kutokea Zanzibar. Himaya yake iligawanywa baada ya kifo chake ambapo mtoto wake wa tatu wa kiume Thuwaini bin Sultan Said akawa mtawala wa Oman na Muscat na wa sita Majid bin Said akawa mtawala wa Zanzibar.

Hilo la undugu na Sultan wa Brunei ni uongo mtupu. Sultan wa kwanza wa Brunei aliitwa Awang Alak Betatar ambae baada ya kuingia kwenye uislamu alichukuwa jina la Muhammad Shah. Watu wa Brunei ni wa Malay na sio waarabu. Nashindwa kuelewa ni kwa nini ulisema uongo wakati ukijua kabisa Google itakuumbua?

Amandla...
 
Acheni mboyoyo wapeni Warabu ardhi yao maana Sultan Seyyid Said ndio mwanzilishi wa Zanzibar alianza kwa kufanya mashamba ya karafuu na minazi, watu wote wenye asili ya kiafrika hapo Zanzibar ni uzao wa watoto wa Watumwa waliokua vijakazi na vibarua kwenye mashamba ya Sultan.
Hivyo basi alivyoanza kuvuna karafuu na mazao ya minazi Sultan aliufanya mji wa Zanzibar kuwa sehemu ya soko la bidhaa mbalimbali ikiwemo na biashara ya utumwa.
Baada ya migogoro katika koo ya kifalme huko Oman kupamba moto ndio mwamba akaamua kujenga kasri yake Zanzibar na kuhamia rasmi kwa makazi.

Hivyo muwaache jamaa waje Zanzibar ni yao/kwao wanahistoria mtatusaidia zaidi yaani hao ni kama vile mimi na wewe tunavyomiliki mashamba na viwanja kisha tukaviendeleza na kuvijenga.
Jamaa wakaifanya mwanzilishi wa Zanzibar..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ