PostGE2025 Death line and life line on 29 October ukumbusho wangu ni huu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

heartbeats

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2014
Posts
8,042
Reaction score
13,383
Kama Sio Mungu na akili za kusurvive basi nisingekuwapo Nyumba yetu imetawaliwa na matobo ya risasi, kibaraza watu walichokuwa wanaketi watu ilibaki kidgo wamwagwe utumbo.

Nilikuwa mlangoni getini majirani walikuwa nje wameketi wala hawakuwa na nia ovu , nageuza shingo naona umbali wa mita 60 askar wamevaa kiraia mmoja kakoki smg uelekeo wetu alikuwa anautazama, kwa akili yangu nikaona hapa kuna jambo nikamwaambia majirani kimbieni yule anapiga huku kweli namaliza maneno dk ile ile ikatua pale pale kibarazni

Napambana kurudi ndani ile naingia tu naskia paaa pale pale getin so ilikuwa ni sekunde tu ningechelewa ningekula ya kichwa

20251129_101021.jpg
je wewe ilikuwaje
20251103_175337.jpg
 
kwa tuliofanikiwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine salama tumshukuru Mungu Sana,tulishuhudia ukimya wa ajabu Yaani Barabara nzima uko peke yako lakini automatic unakosa Amani!!
Baada ya internet kurudi ndo nikaamini Kumbe nilikuwa nacheza na kifo!
 
Hakika ulikuwa unacheza na kifo bila kujua, imagine walikuwa wanashoot to randomly kama wanaua nguruwe pori
 
Kama Sio Mungu na akili za kusurvive basi nisingekuwapo Nyumba yetu imetawaliwa na matobo ya risasi, kibaraza watu walichokuwa wanaketi watu ilibaki kidgo wamwagwe utumbo.

Nilikuwa mlangoni getini majirani walikuwa nje wameketi wala hawakuwa na nia ovu , nageuza shingo naona umbali wa mita 60 askar wamevaa kiraia mmoja kakoki smg uelekeo wetu alikuwa anautazama, kwa akili yangu nikaona hapa kuna jambo nikamwaambia majirani kimbieni yule anapiga huku kweli namaliza maneno dk ile ile ikatua pale pale kibarazni

Napambana kurudi ndani ile naingia tu naskia paaa pale pale getin so ilikuwa ni sekunde tu ningechelewa ningekula ya kichwa

View attachment 3509150 je wewe ilikuwajeView attachment 3509153
Hiyo risasi ndio mlioitoq hapo kwenye geti la kuslide?
 
kwa tuliofanikiwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine salama tumshukuru Mungu Sana,tulishuhudia ukimya wa ajabu Yaani Barabara nzima uko peke yako lakini automatic unakosa Amani!!
Baada ya internet kurudi ndo nikaamini Kumbe nilikuwa nacheza na kifo!
Hali hii ilinipata pia. Tarehe 30 nilitoka na bajaj maeneo ya Maili Mbili, Dodoma mpaka Uwanja wa Jamhuri ambapo dereva alisema anaishia hapo maana mjini hakuingiliki. Nilishuka na kuanza kutembea mpaka General Hospital ili nipate usafiri mwingine wa kufika Nzuguni.

Nilikuwa nikitembea barabara ya 8 na kupandisha mpaka nilipofika Safina House. Ukimya ulikuwa mkubwa. Nilipishana na magari matatu ya Polisi. Hawakuniuliza kitu. Mitaa mingi ilifungwa kwa utepe wa Polisi, maana yake nilikuwa naongozwa kutembea barabara hiyo hiyo bila ya kukata kulia wala kushoto.

Mfano, kama kungekuwa na snippers kama wanavyodai watu wa Dar, biashara yangu ingeishia siku hii.

Baada ya internet kurudi, ndipo nilipogundua kuwa nilikuwa nabet na maisha yangu. Ilikuwa ni hatari sana kufanya safari ile.

Pia nilipata shida sana wakati wa kurudi. Usafiri haukuwepo. Nauli zilipanda mara tatu na usafiri haukupatikana kwa urahisi. Nilipata boda boda na akaniambia nauli ni 25,000/= kutoka Nzuguni mpaka Maili Mbili. Nilivutana nae mpaka tukakubaliana 20,000/= maana muda huo ilikuwa ni saa 2 usiku.

Barabara ilikuwa kimya na tulipofika Kwa Mudi, Maili Mbili nilikuta barabara imechafuka kwa mawe na takataka. Nikaambiwa kulikuwa na purukushani za Polisi na raia na vijana wawili walikufa kwa risasi.

Nilipofika nyumbani, nikampigia boss wangu na kumwambia sitaweza kwenda tena kazini mpaka hali itakapotulia.
 
Polen huku kwetu tulikua tuna sikia miji jiran tu, ila kwetu tulikua tukiendelea kuchagua samaki na fungu za nyanya rabda tu pale police walikuja na kuamuru watu warudi majumban biashara zkafungwa.
pakawa peupe pee kama zile muvi za mazombi miji iliyotelekezwa
 
Wapi huko kulikokua na amani hivyo
 
Tulibebwa na makarandinga ya jeshi kutoka vigwaza (hapo tulilala siku mbili nikitokea mkoani) mpaka mjini,
Morogoro road ili kua nyeupe magari ya jeshi na ambulance ndio tulipishana nazo, kasheshe nilivyoshushwa kutoka kwenye karandinga kuitafuta nyumbani ni mtiti. Kila sehemu wajeda wametanda.
Kuna sehemu boda alisimamishwa tulinyosha mikono juu akaniulia kwenye beji Kuna nini wakati namjibu nikasikia vyuma vinajikoki! haloo!Huruma ya mjeda tu hajabonyeza kitufe.
 
Ndio mzee na mbele kuna geti lingine imetoboa risas ingine walipiga mbili maeneo hayo
 
Tulibebwa na makarandinga ya jeshi kutoka vigwaza (hapo tulilala siku mbili nikitokea mkoani) mpaka mjini,
Morogoro road ili kua nyeupe magari ya jeshi na ambulance ndio tulipishana nazo, kasheshe nilivyoshushwa kutoka kwenye karandinga kuitafuta nyumbani ni mtiti. Kila sehemu wajeda wametanda.
Kuna sehemu boda alisimamishwa tulinyosha mikono juu akaniulia kwenye beji Kuna nini wakati namjibu nikasikia vyuma vinajikoki! haloo!Huruma ya mjeda tu hajabonyeza kitufe.
D9 again..
 
Back
Top Bottom