Decoder ya Azam ni moja ya Decoder za ovyo/cheap quality ambazo nimepata zitumia

Decoder ya Azam ni moja ya Decoder za ovyo/cheap quality ambazo nimepata zitumia

Kifupi sio remote tu mpka maudhui Yao bado ya hovyo na hayajawahi nishawishi , at bei zao tu sio rafiki yaani Kuna mda unauziwa laki mbili kwa seti Moja !!Content zao nyingi ukiondoa michezo ni biased pia so kwa kua taifa limetupa uhuru wa kuchagua heri kujiongeza tu ukae kwingine .😀😀😀😀
 
Ujinga si tatizo huwa unatoka. Wewe naamini Unaabudu Dini ya Upumbavu. [emoji1787]
.
giphy.gif
 
Ninayo ya Startimes ya kwanza kabisa zilipoingia, mpaka leo lakini ni kama mpya na rimoti yake ileile, lakini cha Azam kwanza dishi halijamaliza miaka miwili limeoza na rimoti inamakengeza, nilitoa taarifa wakasema ninunue nyingine! King'amuzi wakatengeneza bure!
Niliwahi kuweka humu Post nikiwataka TBS na Tume ya Ushindani Bora ivikague lakini wanaogopa.
Jamiiiforums raha sana , eti " dishi limeoza, remote ina makengeza".
 
Yangu hadi uipige pige ndio inafanya kazi

Pili rimot ya tv yangu star x inaingiliana na king'amuzi so nikiongeza sauti tv kwenye decoder inabadili chanel kutokaza tv to redio.
 
Azam wana matatizo , ukiongeza sauti yenyewe inapunguza saut ya know tv...ya kwanza ilishakufa hii ni mpya.

Nadhan wameamua wafanye biashara kwenye hizo remote.
 
king'amuzi cha azam kina aina mbili ya remote, aina ya kwanza ni remote ngumu na bora ambazo zinauzwa elfu 20 elfu 25 kama sijakosea.

aina ya pili ni remote nyepesi ambazo unapewa bure kama replacement endapo utarudisha remote iliyoharibika.


wewe bila shaka unatumia romote uliyopewa bure.
Mkuu remote wamekataa kutoa bure, mimi nina king'amuzi cha antenna, button kadhaa ziliacha kufanya kazi ikowa ni mwezi mmoja tu baada ya kununua, nilipoenda Mbezi kwenye duka lao la matengenezo wakaniambia AZAM wanatengeneza decorder tu rimoti natakiwa kununua, Tshs. 15,000/=, sasa hizo za bure for replacement wanatoa wapi?
 
Nimeshabadilisha remote mara 3. Remote bado mpya unabonyeza Menu yenyewe ina change program. Unaongeza sauti sometimes ina change channel.

Unarudi Back inakupeleka kwenye menu. Unaweza bonyeza button hata mara tatu isi respond na hapo umeielekeza kabisa karibu na decoder siyo kwamba ipo mbali.

Inanikwaza sana na inakuwa kero. Huwezi fanya kitu once. Nliwasiliana nao wakaniambia nitakuwa nimeharibu nikanunue nyingine hii sasa ya tatu. Bado haijielewi.

Na wateja tukisema mnaleta habari zenu utadhani sisi sote ni wale wengine. Maana hili mimi linanikwaza ukilinfanisha hawa jamaa nawapigia debe sababu ni wa hapa hapa lakini sasa tusifuge ubovu. Mnanilazimisha niendelee kitumia tu DSTV.
Jaribu kuwekea battery mpya mi remote yangu nimeanza kuitumia toka 2016 Hadi leo ukibadilisha battery inapiga mzigo fresh ingawa hizo tabia huwa zinatokea mara chache sana hasa battery ikiwa imetumika mda mrefu...
 
Jaribu kuwekea battery mpya mi remote yangu nimeanza kuitumia toka 2016 Hadi leo ukibadilisha battery inapiga mzigo fresh ingawa hizo tabia huwa zinatokea mara chache sana hasa battery ikiwa imetumika mda mrefu...
Daaah.... Yaani unaamini battery ndo sababu? 🤣 Battery ni issue ndogo sana ambayo matokeo yake huonekana kirahisi pale ambapo remote hai respond. Hapo nimezungumzia kupeleka wrong information kwenye TV. Unabonyeza menu. Yenyewe ina ongeza sauti. Unaongeza sauti yenyewe inazima. Inawezekana ya kwako ilitengenezwa kwa viwango.
 
Back
Top Bottom