Decoder ya Azam ni moja ya Decoder za ovyo/cheap quality ambazo nimepata zitumia

Decoder ya Azam ni moja ya Decoder za ovyo/cheap quality ambazo nimepata zitumia

Mimi king'amuzi Chao kina kwama kwama Sana..unaweza ukawa unatazama kipindi..ghafla inastaki mpaka.ukazime na kuwasha kwenye main switch
 
Wenzetu mambele wanakuaga na kipindi flani (mwezi moja hadi sita) kwamba kuna bidhaa ukinunua usiporidhika nayo unaweza kurudisha. Azam wangeweka hii ningerudisha kadude kao. Bora niendelee kupambana na DStv
 
Tafuteni hizi una clone remote original unakua unatumia hii, inauwezo wa ku operate devices 3 tofauti mfano tv, kingamuzi, na radio au receiver kwa wakati mmoja.


-1795488250-2031889773.jpg
 

Attachments

  • -1795488250-2031889773.jpg
    -1795488250-2031889773.jpg
    27.9 KB · Views: 7
Mim sisem sana mana itakua kama unaonekana unaishambulia.
Nachojiuliza ni sawa vifurushi vinawekwa kibiashara.

Hiv aljzeera arabic kwneye kifurush cha 23000 hamweki chanel hio ila mmeacha ajzeera English...sasa ndio nini kwa mfano kwamza news chanel nazo ni za kuweka kwenye mavifurushi ya bei juu ??
Na kwanin RT mmeiondoa sa ndio nini
 
Nimeshabadilisha remote mara 3. Remote bado mpya unabonyeza Menu yenyewe ina change program. Unaongeza sauti sometimes ina change channel.

Unarudi Back inakupeleka kwenye menu. Unaweza bonyeza button hata mara tatu isi respond na hapo umeielekeza kabisa karibu na decoder siyo kwamba ipo mbali.

Inanikwaza sana na inakuwa kero. Huwezi fanya kitu once. Nliwasiliana nao wakaniambia nitakuwa nimeharibu nikanunue nyingine hii sasa ya tatu. Bado haijielewi.

Na wateja tukisema mnaleta habari zenu utadhani sisi sote ni wale wengine. Maana hili mimi linanikwaza ukilinfanisha hawa jamaa nawapigia debe sababu ni wa hapa hapa lakini sasa tusifuge ubovu. Mnanilazimisha niendelee kitumia tu DSTV.
Bongo kila kitu hovyo, Zuku wapo vizuri,hila hawakuwa wabunifu tu tokea mwanzo,wangeliteka soko la tz
 
Labda za miaka hii ndiyo fake,ninayoremote nilinunua na dish lake miaka 6-7 iliyopita,ila haijawahi kunizingua na sijawahi kubadilisha remote zote mbili.

Natumia ila dish lao ni lakipuuzi sana mvua kidogo tu,linakata matangazo.........
 
king'amuzi cha azam kina aina mbili ya remote, aina ya kwanza ni remote ngumu na bora ambazo zinauzwa elfu 20 elfu 25 kama sijakosea.

aina ya pili ni remote nyepesi ambazo unapewa bure kama replacement endapo utarudisha remote iliyoharibika.


wewe bila shaka unatumia romote uliyopewa bure.
Hii remote mimi nimenunua pamoja na package nzima ya king'amuzi na Dish, lakini kiukweli ni nyepesi na haina ubora wowote.... Imenibidi ninunue ingine kubwa na imara kidogo
IMG_20220908_114544_874.jpg
 
Hivyo rimoti unayopewa ununuapo king'amuzi ni ya bure! Punguza ujuaji kwani tatizo la ving'amuzi vya Azam ni kubwa kuliko vya vituo vingine na vimekuwa vikilalamikiwa sana, hata madishi ya Azam hayakawii kuoza.
Nenda kwa maajenti wa Azsm wanaofanya matengenezo ukaone jinsi vibovu vilivyojaa.
Hoja ya kindezi sana hii, cha bure pale ni kile kifurushi cha mwezi mmoja unachopewa baasiii... Lakini remote, waya za HDMI na vikoro koro vingine vyote viko kwenye package ya bei sawa??
 
Back
Top Bottom