Tetesi: DED Iramba ashikiliwa Ushetu Shinyanga kwa ubadhirifu wa Milioni Tsh. 180 alipokuwa DED

Tetesi: DED Iramba ashikiliwa Ushetu Shinyanga kwa ubadhirifu wa Milioni Tsh. 180 alipokuwa DED

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Habari kutoka huku Mkoani Shinyanga, halmashauri ya Ushetu, ni kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Iramba- Singida, anashikiliwa na Polisi.

Mkurugenzi Mtendaji huyo Michael Matomola anashikiliwa kwa ubadhirifu wa Milioni 180, fedha za halmashauri ya Ushetu iliyopo hapa Shinyanga. Amri ya kukamatwa kwake Ilitolewa na TAKUKURU baada ya malalamiko kutoka kwa Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo.

DED Michael Matomola alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ushetu kabla ya kuhamishiwa Iramba mkoani singida.
 
Tatizo takukuru hawajawai kushinda kesi hapo kesi hakuna na fidia lazima alipwe tu au afukuzwe kazi na hela alio iba hatonyanganywa kwanza wakati anahamishwa alie muhamisha alijua kila kitu.
 
Hizi kesi ni jaramba la kesi kubwa zijazo za wakubwa na wazito walioharibu huko nyuma
Kwenye hizo chawa tasafali sana,mtupishe wazalendo wakweli tulitumikie taifa bila kikwazo wala gogoro🤸🤸
 
tatizo takukuru hawajawai kushinda kesi hapo kesi hakuna na fidia lazima alipwe tu au afukuzwe kazi na hela alio iba hatonyanganywa kwanza wakati anahamishwa alie muhamisha alijua kila kitu
Unamaanisha Rais alijua kila kitu?? Cha ajabu ni Kama walibadilishana, wa Iramba alihamia Ushetu na wa Ushetu akahamia Iramba. Sasa hapo si mnayajenga na kulindiana Maovu!!
 
tatizo takukuru hawajawai kushinda kesi hapo kesi hakuna na fidia lazima alipwe tu au afukuzwe kazi na hela alio iba hatonyanganywa kwanza wakati anahamishwa alie muhamisha alijua kila kitu
Watashindaje wakati wao ni wala rushwa no.1, kama wangekuwa hawapokei wangefungwa wengi na tungekuwa mbali kama nchi
 
Kufungwa mtu ni jambo gumu sana huko kwani wanabebana sana na kila mmoja anajua siri za mwenzake

Ila ipo siku kuna watu watawajibishwa tena wakubwa zaidi ya hao dagaa
 
Kama kweli TAKUKURU mmeamua kufungua ukurasa mpya,BASI HONGERENI,..maana huyu ni kigogo wa Pili
 
kahama kuna jipu kubwa watu wanapiga huku serikali muangalie upya.
 
Back
Top Bottom