Tetesi: DED Iramba ashikiliwa Ushetu Shinyanga kwa ubadhirifu wa Milioni Tsh. 180 alipokuwa DED

Tetesi: DED Iramba ashikiliwa Ushetu Shinyanga kwa ubadhirifu wa Milioni Tsh. 180 alipokuwa DED

Hatua zenyewe hazimtii hata muwasho mhalifu, ingekuwa wanapigwa risasi hakuna mtu angefanya huo ujinga
Mimi naona kifungo cha maisha na kazi ngumu gerezani yatosha. Ili ajutie vizuri makosa yake.
 
Habari kutoka huku Mkoani Shinyanga, halmashauri ya Ushetu, ni kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Iramba- Singida, anashikiliwa na Polisi.

Mkurugenzi Mtendaji huyo Michael Matomola anashikiliwa kwa ubadhirifu wa Milioni 180, fedha za halmashauri ya Ushetu iliyopo hapa Shinyanga. Amri ya kukamatwa kwake Ilitolewa na TAKUKURU baada ya malalamiko kutoka kwa Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo.

DED Michael Matomola alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ushetu kabla ya kuhamishiwa Iramba mkoani singida.
Huyu jamaa kama ni yeye ninayemfahamu anajisikia sana ukifika ofisini kwake hata watu wazima wanamwogopa
 
Back
Top Bottom