DED monduli na tanesco wamedhulumu taasisi za dini fidia ya ardhi

MWIBAPORI

Member
Joined
Feb 10, 2017
Posts
60
Reaction score
35
Hii imetokea katika kijiji cha Makuyuni mkoani Arusha tangu 2017 hadi leo ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli amedhulumu taasisi za dini ya kiislam na kikristo na baadhi ya wananchi fidia ya ardhi yao baada ya TANESCO kupitisha umeme wa kilovolti 400 katika maeneo yao.

Makuyuni ni kijiji lakini ili DED huyu achukue hela za wananchi yeye na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha Kimanta walisema kijiji cha Makuyuni ni eneo la Halmashauri hivyo hiyo fidia anaichukua yeye.

Rais wetu tusaidie maana huu ni wizi na dhuluma kubwa ambayo wananchi wamefanyiwa.

Juhudi za kumwona na kuongea naye hazijazaa matunda na amekuwa akiwazungusha wananchi kwa kushirikiana na TANESCO Arusha na Afisa mipango miji wa manispaa ya Arusha aitwaye Deo.

DED anatumia mabavu na uvunjifu mkubwa wa sheria maana hana nyaraka zozote za kiserikali zinazoonyesha kama Makuyuni ni mji au mji mdogo kwani bado ni kijiji chenye vitongoji na siyo mitaa. Pia kijiji cha Makuyuni kinaongozwa na mwenyekiti wa kijiji pamoja na Mtendaji wa kijiji.

Na pia Rais wetu kipenzi tunakuomba sana utakapochagua wakurugenzi wa Halmashauri utuondolee huyu DED pale Monduli kwani amesababissha mateso makubwa kwa wananchi.

Zipo kesi zilizopelekwa mahakama kuu ambapo DED alishindwa na hakuweza kukata rufaa lakini bado anashindana na mahakama ili wahusika wasilipwe fidia kwa kuwarubuni TANESCO pamoja na afisa mipango miji wa Arusha.

Tunawasilisha kwa mara nyingine ombi letu kwako mh. rais ili utasaidie tupate haki yetu
 
Mh. Rais sikia kilio chetu watu wa Makuyuni mkoani Arusha maana tunadhulumiwa na mtu uliyemweka atuhudumie
 
Naona umeamua kurudia haya malalamiko
 
Back
Top Bottom