DED Mtwara Mikindani: Muuza Samaki anayetozwa ushuru kisha akiomba risiti anatishiwa, aje aripoti tuwabaini wanaofanya hivyo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Hassan Nyange ametoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya wafanyabiashara wa Soko la Samaki Feri, kuhusu madai ya ukiukwaji wa taratibu katika ukusanyaji wa ushuru.

Hoja ya awali ya Mdau hii hapa ~ Wafanyabiashara wa Soko la Samaki Feli, Manispaa ya Mtwara Mikindani tunakatwa ushuru, tukiomba risiti wanatutishia

Mdau alisema wanakatwa ushuru wa kila siku bila kupewa risiti za malipo kama inavyotakiwa na hata wanapodai kupewa risiti hizo, baadhi yao hutishwa kufukuzwa eneo hilo.

Akizungumzia malalamiko hayo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mwalimu Hassan Nyange amemtaka mwananchi anayelalamika ampigie simu moja kwa moja ili kumbaini ofisa anayefanya ukikwaji huo na kujua eneo husika.

“Kama unaweza kumpata huyo mlalamikaji mwambie anipigie simu moja kwa moja, maana ni jana tu (Agosti 13, 2026) nilikuwa eneo hilo la Feri na nilikula hapo na huwa na kwenda kutembelea mara kwa mara. Isitoshe, Mbunge wa Mtwara Mjini alifanya mkutano na wafanyabiashara wa Feri wakamweleza kero zao, Mkuu wa wilaya amefanya mkutano hapo na Mkuu wa Mkoa pia na wote wameelezwa kero zao,” amesema.

Ametaja baadhi ya kero zilizotolewa na wafanyabiashata katika mikutano hiyo kuwa ni pamoja na vyoo kukosa maji.

“Tumenunua tanki la maji na maji yalikuwa hayatoki tumechimba mfereji pale sasa hivi maji yanatoka saa 24. Kero nyingine tunasubiri mwaka mpya wa fedha ndio tutatekeleza. Hilo eneo la Feri kuna vyombo vya ulinzi na Usalama hapo maana ni mpaka na Msumbiji na kuna wananchi wa Msumbiji wanafika hapo kununua mahitaji,” amesema.

Nyange pia amesema kulikuwa na mkutano kati ya uongozi wa Wizara ya Viwanda na Biashara na wafanyabiashara wa Mtwara, lakini hakukuwa na malalamiko ya utozwaji wa ushuru holela.

“Hata hivyo, nitafuatilia zaidi kujua tatizo liko wapi,” amesema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…