BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
Khalif akiwa ameambatana na Wataalam kutoka divisheni ya Ujenzi, Mipango na uratibu na Afya wametembelea Miradi yenye thamani ya Shilingi 582,017,569 ya Sekta ya Afya na Elimu ambayo utekelezaji wake upo katika hatua tofauti kwa lengo la kuwahimiza wakandarasi kuongeza kasi ya kukamilisha miradi kwa wakati ili iweze kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Khalif amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia fedha nyingi Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa zinazolenga kuboresha sekta zote ikiwemo Afya na Elimu.
Aidha,ametoa rai kwa wakandarasi kukamilisha miradi kwa wakati ili wananchi waendelee kunufaika na matunda ya Kodi yao na kwamba mkandarasi atakayechelewesha mradi ama Kujenga chini ya kiwango atakumbana na rungu la sheria kwa mujibu wa taratibu.
Evelyne Mwakibete Mratibu wa Miradi, Miriam Panja Mchumi na Mhandisi Allen Mshiu wamesema wataendelea kutoa ushauri wa kitaalam wa kifedha na kihandisi kwa wakandarasi ili kuhakikisha kuwa Miradi inakamikika kwa wakati na ubora unaolingana na thamani ya fedha.