A
Anonymous
Guest
Mimi ni mdau wa JamiiForums.com nina kero ambayo naomba ujumbe ufike kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya pamoja na ofisini yake kwa jumla.
Sisi Watumishi katika ngazi Elimu Msingi hatujalipwa fedha yetu ya likizo tangu Desemba 2024, licha ya kuwa tulijaza fomu ya malipo lakini cha kushangaza baada ya hapo waliitwa Watu wachache sana na wanaofamiana na waliopo kwenye “mfumo”.
Wengine tumeachwa na hakuna taarifa yoyote, tunahofia kwenda kuuliza kwa kuwa mazingira ya ajira zetu sote tunajua siyo rafiki kwa mtu ambaye anaonekana anahoji, kwani hali hiyo inatupunguzia morali ya kufanya Kazi.