Deep State Kumbe Ndio Hii?

Ndebile

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2011
Posts
7,745
Reaction score
11,267
Haya ni mawazo na mtazamo wangu Tu na sio lazima ukubaliane na mimi!

Kwa jinsi mambo ya uvunguni ya shirika kubwa la misaada la USAID yanavyozidi kuweka wazi na jinsi myororo WA ushahidi unavyowaunganisha wanasiasa na watu maarufu, CIA, vyombo vikibwa vya habari,nk nchini Marekani naanza kuelewa "deep State" ni akina nani.

Naanza kuona kwa mbali kwanini baadhi ya tawala na wanasiasa kutoka nchi zetu za Afrika kwanini maovu yao huwa hayasemwi kabisa na viranja wetu akina USA, UK, EU, upo uwezekano hao ni mawakala wao na wanufaika Sana na utawala wao,

Hapo imeguswa USAID kidogo tu, ngoja nitulie nione mtanange huu utanifundisha nini zaidi maana sasa hivi nimejifumza kwamba kama ambavyo CCM wamefanya ufisadi WA kutisha ndio hivyo hivyo baadhi ya wanasiasa wa Marekani nao wanakwiba, ama kweli binadamu ni wale wale bila kujali wapo sehemu gani duniani.

Nawaza pesa tulizokopa kupambana na uviko 19?
 
Wizi kwa mtu mwafrica ni sawa na kumesa dawa ya kutulisa maumivu (Panadol)

Kwa mtu ya ngosi nyeupe, wizi ni sawa na kunywa sumu ya (Cutter)
 
Kwamba CIA kutumia USAID kama "front operation" ni ufisadi?? Au ndio ushahidi wa "deep state"?.

Acha kuchekesha umma.

Tena hao jamaa nakupa miezi 6 tu wanarudi. Taasisi haiwezi kutumia miongo kadhaa kujenga mtandao wa inteligensia kisha wakubali kuupoteza kizembe.
 
Nafikiri USAID watarudi ila wataweka masharti mengi na vigezo vingi zaidi ili kutoa misaada yao na pia kupata access ya mambo yako.
 
Jiulize anarudi wakiwa chini ya "ofisi ya Rais" alafu tuone kama watadhamini tafiti kama hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…