sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Katika kila hatua na kila tendo tulifanyalo mbele ya watu, toleo letu lengine la ziada hutengenezwa kwenye fikra za watu ambazo hatuwezi zibadili, pia katika Maisha haya nafasi ndogo hujengwa na mambo yanayotokea lakini nafasi kubwa zaidi ni maamuzi yetu tunavyokabiliana na hayo matukio iwe ni katika furaha, majonzi, mafanikio, kujinasua katika tatizo, n.k.
Katika akili za watu waliowahi kukutana na wewe, wanakujua kwa toleo tofauti ya lile unanolijua wewe akilini mwako, watu wanavyokuchukulia huwa ni tofauti na wewe unavyojiona na kuamini kwamba kila mtu atakuona kwa jinsi unavyojiona wewe.
Japo kila mtu ana mtazamo tofauti, kuna msingi wa mitazamo ambayo hujengwa kwa tamaduni zetu, kanuni, mafundisho ya dini, n.k. jaribu sana kuishi humo.
Mbaya Zaidi kunakuwaga na wingu kubwa la kila mtu kujipa toleo bora katika akili yake na kuona kwamba ile afanyacho hakina tatizo, unaweza ukawa uepandishwa cheo kazini na kuweka status ya picha, ukatumiwa messej na Rafiki yako ambae umempiga gepu kiuchumi, wewe ukam blue tick na kuona ni sawa maana umesoma pongezi yake, hapa toleo lako jipya litakua ni mtu mwenye kuringa na kiburi, ni muhimu katika hii hali kuejea katika misingi ya utu mwema iliyowekwa katika tamaduni zetu n ahata dini zetu kwamba kufanya kitu kama hicho ni dharau hivyo ni uamuzi mwema kumjibu Rafiki huyo kwa kusema asante.
Ni muhimu sana kuweka balansi ya toleo lako la utu unalolijua wewe na toleo la utu wako lilomo katika fikra za watu wengine.