Hata kama wizi upo kote ila kwa waafrika ni default settings
Lori likipiga mzinga default settings za waafrika huwa ni Baraka imeshuka, watu wanajsevia hawajali hasara wanayotengeneza
Mwajiriwa anaelipwa kwa kodi za wananchi bado anahitaji mlungula au ya soda ili afanye kazi yake, bila hivyo unaweza kusubiri siku nzima.
Kiongozi ana uhakika wa posho ya kalio na kiinua mgongo sifuri nane lakini hatosheki kabisa, anaumiza kichwa ni namna gani aibe hela za miradi ya maendeleo.