AfricaUnited
JF-Expert Member
- Jul 31, 2010
- 2,367
- 1,293
Utawala ni fani sawa na fani zingine kama vile uhandisi, tafadhari usichanganye vitu hapa! Kumbuka, mtawala atafanya kazi yake kwa ufasaha zaidi kuliko ambavyo mhandisi angeliweza kutawala, vivyo hivyo mhandisi atafanya kazi yake ya uhandisi kwa ufasaha zaidi kuliko mtaalamu wa fani iliyo tofauti na uhandisi! Zaidi, nikukumbushie ya kuwa, mtawala aliyesoma kozi fupi ya utawala, atakuwa na uwezo mfupi/mdogo wa kutawala sawa na kiwango cha elimu yake! Elewa kuwa, aliyesoma shahada ya sheria na aliyesoma stashahada ya sheria, wote ni wanasheria, japo uanasheria wao unazidiana kutokana na viwango vya elimu zao! Je umenielewa? Kamabado, niambie nikuelimishe zaidi kwani bado sijachoka!utawala huo hata engineer au lawyer anaweza akawa mtawala kozi fupi ya muda mfupi unaweza ukawa mtawala.je unaweza ukapewa kozi fupi ya kuwa lawyer au engineer ? Nijibu