Degree ni karatasi tu, haisaidii lolote kiuchumi?

Degree ni karatasi tu, haisaidii lolote kiuchumi?

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Posts
1,769
Reaction score
1,390
Ndg. Asubuhi nimesikiliza mjadala wa saa 2 katika ile platform ya Clubhouse ya mindset transformation. Katika mjadala huo watu watatu wenye degree zaidi ya nne na mmoja mwenye PhD kwa kudai kuwa kupata degree is just a paper na kwamba katika maisha yao hazijawahi kuwasaidia lolote.

Wamekwenda mbali zaidi kuwa Watanzania wengi wanaendesha maisha nje ya degree walizopata.

Wamepata wakati mgumu baada ya members kuwataka watoe ufafanuzi maana humo wapo vijana wanaosikiliza na wanajipanga kuelekea vyuoni lakini wamesisitiza tena kuwa mtu anayetegemea kutumia degree imsaidie anachemka.

Yamesemwa mengi lakini binafsi nikaona si vibaya nikaleta humu kisima cha great thinker tuidadavue maana hawa motivation speakers pasua kichwa.
 
Kutokana na ajira zimekuwa chache sana kiasi ambacho hiyo hoja ndio inakuja pahali pake, lakini sehemu kwenye ajira za kutosha kauli hyo haiwezi kufanya kazi, mfano, wakati mwengine unaweza kusoma degree ya uchumi, lakini ukawa mtangazaji, sio wakati wote unachosoma ndio unachopata kazi, ila kusoma muhimu kwa sababu unakuwa umekitanua kichwa zaidi kimaarifa.

Hayo yapo mpaka nchi nyengine, ila nchi mfano wa Marekani, unaweza kusoma usipate kazi ya ulichosomea ila kazi zipo nyengine nyingi sana kiasi ni wewe mwenyewe tu, ukienda kuomba unapata, na tofauti ya mshahara unaweza kuwa sawa wewe ulomaliza darasa la saba na alomaliza degree mbili. au unaweza kile ulochosomea hela yake ni ndogo kuliko kazi nyengine ambayo hela yake ni kuba zaidi.

Mfano wa viwandani, mtu anaweza kulipwa dola 20 kwa saa (elfu 45,000), wakati huo unaweza kuwa umesomea, ukawa cashier bank ukalipwa dola 15 kwa saa.

Ila kuna faida kubwa ya kusoma mpaka ukafika degree na kutofika, muhimu kusoma tena muhimu sana, kupata kazi hiyo ni changamoto nyengine kabisa.
 
Degree ni ungese tu jwa Tanzania and i think na hata East Africa yote.
 
Only in Tanzania but in so many other countries around the World especially the Western countries degree is very important to open so many doors for you.

Jamaa waliokuwa wakiongea wengine wapo katika hicho hizo
 
Wataalamu wa masuala ya uchumi wanasema mpaka kufika mwaka 2039 Africa itategemewa kwa mambo mengi sana kuanzia Elimu na maisha mengi tu kama chakula na hata maji

Tukianza na elimu kama mnavyoona wale watoto wa kizungu waliokuwa wanategemewa kuwa engineers na doctors Leo wengi wamejikita kwenye social media na kuwa actors, singers, comedians na ubunifu usiokuwa na tija kwa jamii bali wafuasi milioni

Hapo kama tutawekeza kwenye elimu wao ndio watatuhitaji zaidi kuwa doctors na kazi nyingi tu

Rejea wameanza taratibu kuchukua nurses toka Kenya kuja UK

Waarabu pia walishtuliwa zamani wakafikiri watauza mafuta kwa wingi maisha yao yote ila mambo yatakuwa magumu sana kwani Solar zitatawala na magari ya umeme yatakuwa mengi na kuyatupa yanayotumia mafuta

Tuna wakati mzuri sana wa kujipanga na vijana kusoma sana kwa vitendo sio kukariri

Msiwasikilize hao kwani walienda kukariri sio kusoma
 
Mwakyembe analizungumziaje hili! Kwanza yupo kweli!
 
MNA mfumo mbaya was Elimu na wala sio kwamba degree ni karatasi, sema kwaa Tanzania ndio degree ni zaidi ya Tissue ya chooni!

Kenya wana satellite yao wenyewe wamerusha! Sisi tuna nyungo
 
Wataalamu wa masuala ya uchumi wanasema mpaka kufika mwaka 2039 Africa itategemewa kwa mambo mengi sana kuanzia Elimu na maisha mengi tu kama chakula na hata maji

Tukianza na elimu kama mnavyoona wale watoto wa kizungu waliokuwa wanategemewa kuwa engineers na doctors Leo wengi wamejikita kwenye social media na kuwa actors, singers, comedians na ubunifu usiokuwa na tija kwa jamii bali wafuasi milioni

Hapo kama tutawekeza kwenye elimu wao ndio watatuhitaji zaidi kuwa doctors na kazi nyingi tu

Rejea wameanza taratibu kuchukua nurses toka Kenya kuja UK

Waarabu pia walishtuliwa zamani wakafikiri watauza mafuta kwa wingi maisha yao yote ila mambo yatakuwa magumu sana kwani Solar zitatawala na magari ya umeme yatakuwa mengi na kuyatupa yanayotumia mafuta

Tuna wakati mzuri sana wa kujipanga na vijana kusoma sana kwa vitendo sio kukariri

Msiwasikilize hao kwani walienda kukariri sio kusoma
Hizo kazi za social media zina malipo kuliko hata hizo kazi nyingine , sasa kwann waumie kusoma saana
 
Back
Top Bottom