Dreadnought
JF-Expert Member
- Mar 25, 2013
- 2,876
- 3,942
Tanzania tunataka mtu akiwa msomi basi awe tajiri kitu ambacho si sahihi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nakubaliana na wewe mitaala yetu ya elimu ndio tatizo.Only in Tanzania but in so many other countries around the World especially the Western countries degree is very important to open up so many doors for you.
Hizo kazi za social media zina malipo kuliko hata hizo kazi nyingine , sasa kwann waumie kusoma saana
Shukran Sana mkuu unaona mbali sana
Shida namba moja hapa tanzania kwenye sekta ya elimu ni kwamba hatuwafunzi wasomi wetu lengo rasmi la elimu bali tunawapa tamaa ya kupata fedha kiwepesi kwa kupitia elimu na ajira rasmi.Jamii huwaaminisha vijana wetu tangu utoto wao, endapo watasoma watakuwa na ajira yenye tija ndio maana si ajabu kuona kijana akiulizia kozi gani inalipa akaisomee chuoni. Hivyo chachu ya wasomi wengi(si wote) ya kusoma kwa bidii msingi wake ni fedha kupitia ajira nzuri ili asaidie familia yake, wakati malengo halali ya elimu ni kutoa huduma kwa jamii(kila taaluma kwa nafasi yake), kutawala mazingira yetu,kuifanya dunia kuwa mahali bora pakuishi sisi na vizazi vijavyo(making better Earth) na kuamisha ujuzi kwa vizazi( Transfer knowledge through generations) na hayo mambo ya fedha kwa mtu huja kama zawadi ya utoaji huduma kwa jamii. Hili kosa ndo hupelekea wasomi wapenda rushwa maofisini,magraduate wasiojua fani zao vyema, kukosa utu na kunyanyasa watu ktk ofisi za umma, uzalendo mdogo kwa taifa, maendeleo madogo ya kitaaluma na technolojia, degree kuonekana karatasi tu na mengine mengi..Ndg.Asubuhi nimesikiliza mjadala wa saa 2 katika ile platform ya club house ya midset transformation. katika mjadala huo watu watatu wenye degree zaidi ya nne na mmoja mwenye PHD kwa kudai kuwa kupata degree is just a paper na kwamba katika maisha yao hazijawahi kuwasaidia lolote.
Wamekwenda mbali zaidi kuwa watanzania wengi wanaendesha maisha nje ya degree walizopata.
Wamepata wakati mgumu baada ya members kuwataka watoe ufafanuzi maana humo wapo vijana wanaosikiliza na wanajipanga kuelekea vyuoni lakini wamesisitriza tena kuwa mtu anayetegemea kutumia degree imsaidie anachemka.
Yamesemwa mengi lakini binafsi nikaona si vibaya nikaleta humu kisima cha great thinker tuidadavue maana hawa motivation speakers pasua kichwa
Wataalamu wa masuala ya uchumi wanasema mpaka kufika mwaka 2039 Africa itategemewa kwa mambo mengi sana kuanzia Elimu na maisha mengi tu kama chakula na hata maji
Tukianza na elimu kama mnavyoona wale watoto wa kizungu waliokuwa wanategemewa kuwa engineers na doctors Leo wengi wamejikita kwenye social media na kuwa actors, singers, comedians na ubunifu usiokuwa na tija kwa jamii bali wafuasi milioni
Hapo kama tutawekeza kwenye elimu wao ndio watatuhitaji zaidi kuwa doctors na kazi nyingi tu
Rejea wameanza taratibu kuchukua nurses toka Kenya kuja UK
Waarabu pia walishtuliwa zamani wakafikiri watauza mafuta kwa wingi maisha yao yote ila mambo yatakuwa magumu sana kwani Solar zitatawala na magari ya umeme yatakuwa mengi na kuyatupa yanayotumia mafuta
Tuna wakati mzuri sana wa kujipanga na vijana kusoma sana kwa vitendo sio kukariri
Msiwasikilize hao kwani walienda kukariri sio kusoma
acha kujidanganya ndugu
Umenena vyemaShida namba moja hapa tanzania kwenye sekta ya elimu ni kwamba hatuwafunzi wasomi wetu lengo rasmi la elimu bali tunawapa tamaa ya kupata fedha kiwepesi kwa kupitia elimu na ajira rasmi.Jamii huwaaminisha vijana wetu tangu utoto wao, endapo watasoma watakuwa na ajira yenye tija ndio maana si ajabu kuona kijana akiulizia kozi gani inalipa akaisomee chuoni. Hivyo chachu ya wasomi wengi(si wote) ya kusoma kwa bidii msingi wake ni fedha kupitia ajira nzuri ili asaidie familia yake, wakati malengo halali ya elimu ni kutoa huduma kwa jamii(kila taaluma kwa nafasi yake), kutawala mazingira yetu,kuifanya dunia kuwa mahali bora pakuishi sisi na vizazi vijavyo(making better Earth) na kuamisha ujuzi kwa vizazi( Transfer knowledge through generations) na hayo mambo ya fedha kwa mtu huja kama zawadi ya utoaji huduma kwa jamii. Hili kosa ndo hupelekea wasomi wapenda rushwa maofisini,magraduate wasiojua fani zao vyema, kukosa utu na kunyanyasa watu ktk ofisi za umma, uzalendo mdogo kwa taifa, maendeleo madogo ya kitaaluma na technolojia, degree kuonekana karatasi tu na mengine mengi..
Yaaani unakuta mtu yupo kazini ila anaenda kuongeza elimu ili apande cheo tu au ngazi ya mshahara pekee na sio ongezeko la utoaji bora wa huduma kwa jamii na taifa lake. Pia leo huko mitaani kipimo cha usomi wa mtu kinapimwa kwa namna alivyofanikiwa kiuchumi yaani ajabu sana ...hii ndo husababisha wasomi waliokosa ajira rasmi kudharaulika/ kudharau elimu zao na kuita karatasi tu kwa kuwa hawana matumizi nazo nje na lengo la fedha za ajira rasmi.
Conspiracy Theories zinakuharibu! Degree hizi za UDSM ndio ziwe tegemeo la baadae, Yena kama kuna sehemu Duniani ambayo Elimu imeshindwa kuonesha faida yake basi ni Africa. Angalia hadi leo hii hali yetu kulingana na Idadi ya wasomi tulionao.Wataalamu wa masuala ya uchumi wanasema mpaka kufika mwaka 2039 Africa itategemewa kwa mambo mengi sana kuanzia Elimu na maisha mengi tu kama chakula na hata maji
Tukianza na elimu kama mnavyoona wale watoto wa kizungu waliokuwa wanategemewa kuwa engineers na doctors Leo wengi wamejikita kwenye social media na kuwa actors, singers, comedians na ubunifu usiokuwa na tija kwa jamii bali wafuasi milioni
Hapo kama tutawekeza kwenye elimu wao ndio watatuhitaji zaidi kuwa doctors na kazi nyingi tu
Rejea wameanza taratibu kuchukua nurses toka Kenya kuja UK
Waarabu pia walishtuliwa zamani wakafikiri watauza mafuta kwa wingi maisha yao yote ila mambo yatakuwa magumu sana kwani Solar zitatawala na magari ya umeme yatakuwa mengi na kuyatupa yanayotumia mafuta
Tuna wakati mzuri sana wa kujipanga na vijana kusoma sana kwa vitendo sio kukariri
Msiwasikilize hao kwani walienda kukariri sio kusoma
Hizo kazi za social media zina malipo kuliko hata hizo kazi nyingine , sasa kwann waumie kusoma saana