Degree ni karatasi tu, haisaidii lolote kiuchumi?

Only in Tanzania but in so many other countries around the World especially the Western countries degree is very important to open up so many doors for you.
Nakubaliana na wewe mitaala yetu ya elimu ndio tatizo.
 
Hizo kazi za social media zina malipo kuliko hata hizo kazi nyingine , sasa kwann waumie kusoma saana

Inamsaidia nini mwanachi ambae atahitaji kutibiwa kama kijana badala asomee Uganga
Huyo wa aliyeko kwenye tiktok na kupata hela au YouTube na kupata hela akifika miaka 20 ijayo ataweza kuisaidia jamii kwa lipi?

Hapo nazungumzia hao ambao wanategemewa kuwa wataalamu baadae ila wame drop shuleni kisa anauza bidhaa kwenye Amazon

Mkuu angalia ya mbele hao hao watakuja kutuhitaji sisi maana tiktok na YouTube haitawasaidia wananchi wao

Huyo unasema anatengeneza hela hiyo ni faida yake bali jamii haisaidii lolote na ni upotevu wa rasilimali watu

Naongelea kwa ujumla na uhalisia wa maisha yatakavyokuwa baadae
Ila kila mmoja anavyoona na wewe unavyoona ndio hivyo
 
Mzee wa digrii nne, mwakiembe hakosi hapo...
 
Shukran Sana mkuu unaona mbali sana

Natamani kama waafrika tutaliona hili na kuwaza tofauti
Tuna kila kitu kuwazidi na neema zote ziko kwetu
Kuna nchi zina hela ila hata nyanya hawajui inaotaje

Hakika tusifurahie kuja kwao kununua Ndizi kwa matani huu ndio mwanzo
Watajazana mpaka wengine watanunua na ardhi kwenye serikali mbovu za Africa

Mungu Ibariki Tanzania [emoji1241]
 
Japo maisha siyo kutesa Kila siku ila pesa ndiyo Kila kitu...

Ngoja waje kutia miongozo...
 
Shida namba moja hapa tanzania kwenye sekta ya elimu ni kwamba hatuwafunzi wasomi wetu lengo rasmi la elimu bali tunawapa tamaa ya kupata fedha kiwepesi kwa kupitia elimu na ajira rasmi.Jamii huwaaminisha vijana wetu tangu utoto wao, endapo watasoma watakuwa na ajira yenye tija ndio maana si ajabu kuona kijana akiulizia kozi gani inalipa akaisomee chuoni. Hivyo chachu ya wasomi wengi(si wote) ya kusoma kwa bidii msingi wake ni fedha kupitia ajira nzuri ili asaidie familia yake, wakati malengo halali ya elimu ni kutoa huduma kwa jamii(kila taaluma kwa nafasi yake), kutawala mazingira yetu,kuifanya dunia kuwa mahali bora pakuishi sisi na vizazi vijavyo(making better Earth) na kuamisha ujuzi kwa vizazi( Transfer knowledge through generations) na hayo mambo ya fedha kwa mtu huja kama zawadi ya utoaji huduma kwa jamii. Hili kosa ndo hupelekea wasomi wapenda rushwa maofisini,magraduate wasiojua fani zao vyema, kukosa utu na kunyanyasa watu ktk ofisi za umma, uzalendo mdogo kwa taifa, maendeleo madogo ya kitaaluma na technolojia, degree kuonekana karatasi tu na mengine mengi..
Yaaani unakuta mtu yupo kazini ila anaenda kuongeza elimu ili apande cheo tu au ngazi ya mshahara pekee na sio ongezeko la utoaji bora wa huduma kwa jamii na taifa lake. Pia leo huko mitaani kipimo cha usomi wa mtu kinapimwa kwa namna alivyofanikiwa kiuchumi yaani ajabu sana ...hii ndo husababisha wasomi waliokosa ajira rasmi kudharaulika/ kudharau elimu zao na kuita karatasi tu kwa kuwa hawana matumizi nazo nje na lengo la fedha za ajira rasmi.
 

acha kujidanganya ndugu
 
acha kujidanganya ndugu

Huo ndio ukweli ila kwa sisi tunaangalia kesho tunakula nini
Ya miaka 40 au 50 ijayo hayatuhusu kwani hatuna la kuvumbua kwa hiyo tunasubiri watutafunie kila kitu

Kubali au kataa utakuwa mtumwa wao tu kama hutabadili mentality hii
 
Umenena vyema
 
Degree ni muhimu sababu mtu akijuwa umesoma ndio atakapoanzia kukusaidia au msomi mwenyewe ataangalia opportunity kwenye field yake
Ubaya tunaona hvyo wengi tumesoma fata mkumbo au tulichaguliwa na wazazi sio kitu tulipenda toka udogoni au moyoni
 
Wako sahihi PhD ya uchumi inashindwa kutafuta vyanzo vya mapato inakimbilia mihamala ya simu
 
Conspiracy Theories zinakuharibu! Degree hizi za UDSM ndio ziwe tegemeo la baadae, Yena kama kuna sehemu Duniani ambayo Elimu imeshindwa kuonesha faida yake basi ni Africa. Angalia hadi leo hii hali yetu kulingana na Idadi ya wasomi tulionao.
 
Tatizo ni umaskini, mapinduzi ya viwanda waliyopitia wenzetu miaka 300 iliyopita ndio yali solve problems walizokuwa nazo ambazo ndizo tunazo sisi kwa sasa.
Democracy
Uchumi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…