Degree ni karatasi tu, haisaidii lolote kiuchumi?

Naam kwa kuchanganya elimu na kipato plus ajira basi mwenye elimu asiye na ajira ama kipato kizuri ni lazima alalamike lakini mimi nafikiri kuwa elimu ipo kwa ajili ya kumkomboa mwanadamu na kama haijamkomboa basi hiyo si elimu. Bado niende mbali na kusema hao wanaopinga elimu leo hii wanamtazamo finyu elimu ina mambo mengi mno ya msingi sema watu tunashindwa kutofautisha ujuzi wako na maarifa yako kwa ajili ya kusustain maisha. Watu wanataka elimu iwe hardware ya kuwabeba wakati elimu ni software.
Kama ilivyo kwa computer programs na computer yenyewe yaani katika program za computer yaani software zina-operate kwenye hardware na hivyo ukikosea kuweka data inayotakiwa katika program fulani ni lazima ikuletee error.
Ndivyo ilivyo degree si karatasi ila degree ni kiwango cha software alizonazo na wewe ni hardware sasa ni namna gani unaweza kuzitumia hizo software zako kukuletea unachotaka.
Hapo ndipo utagundua kuwa kushindwa kuitumia vizuri elimu na kuiona kama karatasi tu ndiyo maana mengi sana yanafeli hata kwa serikali zetu. ukitaka kujua elimu ina umuhimu gani basi soma thread yangu katika #stories-for-Change inayohusu kushuka kwa thamani ya elimu nchini nadhani hii inaendana na mjadala huu na inaweza ikawa majibu mazuri kabisa kwa mjadala na namna mtazamo wa elimu unavyozidi kupuuzwa na kuonekana hauna maana.
 
Nadhani kila mtu anachanganya hivi vitu viwili hasa wasomeshaji ambao ni wazazi.

Nia ya kusoma sio kupata pesa bali kutanua uwezo wako wa kifikra na kutatua kila aina ya tatizo, degree na kuwa imara kiuchumi kutokana na ulichosomea ni nyongeza tu ya kuwa na elimu.

kutokuwa imara kiuchumi ni tatizo.
sasa kama mtu umesoma then hauko imara kiuchumi basi hujatumia dhumuni la kwanza la kusoma, yaani kupanua uwezo wa kifikra ili kutatua kila aina ya tatizo.

Kusoma na kutokuwa imara kiuchumi haiondoi umuhimu wa kusoma sababu elimu unaweza kuitumia popote, ni kutanua uwezo wa kifikra.
means huyo aliyesoma na kutegemea degree pekee ili awe imara kiuchumi ni hana akili sababu ameshindwa kutumia elimu yake.
 
Kulinganisha degree na kazi huwezi kupata mantiki, ni sawa na utotoni ulipoulizwa pesa na Elimu Bora Nini??

Mimi naona degree bado ni wadhifa wa kuivisha akili nguo, kwa kuongeza maarifa, Maana tumeagizwa kuwa na akili nguvu na maarifa.

Pesa hata wehu wanazo wanashinda mpaka kamali, na pesa huisha.
 
Mtaani ni elimu nyingine kabisa.Degree ni makaratasi
 
Badala ya Midset ingependeza MINDSET.
 
Tunaenda shule ili kupata knowledge ili iweze kutusaidia kutatua matatizo yetu mbalimbali yanayotukabili!!!!!
 
Mi naona tunachanganya vitu viwili tofauti. Tunasoma ili tupate elimu siyo shahada. Lakini vijana wa sasa wanasoma ili wapate shahada. Matokeo yake wanapata shahada lakini hawana elimu (hawana uwezo wa kupambana na mazingira yao). Ndio maana mijadala kama hii inaibuka.
 
it's not what you know but who you know. Tanzania oyee.
 


Ni swala la kuogofyakwa taifa letu kwa kuona mtu mwenye degree nne (zinatia mashaka kama kweli anazo kutokana na anayosema) akiponda elimu. Hili jambo inaonekama muhusika alikuwa na false assumption kwamba kiasi cha elimu ina equate na fedha au mali. Lakini sivyo hivyo elimu ni kwa ajili ya kupanua fikra na kwa taifa ni kuwa na watu wenye fikra pana.
 
hiyo sio leo wala kesho, subiri baada ya miaka 1000 yesu anaporudi.
 
Ndg yangu hakika unaeleweka vizuri sana, ni kweli kwamba huwezi mlinganisha graduate na asie na degree(form 4 au std 7) kwa uwelewa/maarifa.

Sawa tumepata maarifa au kupanua fikra ILI IWEJE ? iwapo huyo asie na degree ana maisha BORA kuliko sisi tuliona hizo degree ? mbaya zaidi anakuwa ndio BOSS wako aidha kwa kukuajiri au kupitia SIASA, n.k

Dunia hadaa, leo vijana wa mitaani, wameshindwa kusoma wasiochana mwele na bangi zao,, wasio na maadili kabisa, malezi ya hovyo wasiojua msikiti wala kanisa lilipo, kupitia sanaa au michezo ndio matajiri,, wenye hadhi kwenye jamii, umaarufu n.k kuliko aliyelelewa na wazazi vizuri akasoma shule za maana, chini ya maadili ya imani n.k

UKWELI MCHUNGU NA UNAUMA SANA SANA
 
Elimu ya bongo imekuwa biashara skuiz, na viongozi tulionao wapo kimya tu.

Wanarundika wanafunzi mavyuoni, na kuchezea pesa za serikali kwa kuwapa mikopo. Badala hizo pesa wawape mitaji wakafanye kazi.

Matokeo yake wanafunzi baada ya kumaliza vyuo hawapewi ajira wanateseka mtaani, na mkopo wa kurudisha hawana wanakuwa hawana tofauti na la saba. Wanaanza tena moja. Heri na la saba wao walishajipanga toka zamani, wengine unakuta mpaka wameoa na watoto wanae na familia wanaendesha vzr kabisa.
 
Conspiracy Theories zinakuharibu! Degree hizi za UDSM ndio ziwe tegemeo la baadae, Yena kama kuna sehemu Duniani ambayo Elimu imeshindwa kuonesha faida yake basi ni Africa. Angalia hadi leo hii hali yetu kulingana na Idadi ya wasomi tulionao.

Kama wajinga wamebaki Tz sawa lakini mimi nimeandika Africa kutokana na wachambuzi walivyoandika
Kwa hiyo na wewe umo kwa hao waliokariri na kutokuweza kubuni chochote
 
hiyo sio leo wala kesho, subiri baada ya miaka 1000 yesu anaporudi.

Wala sio mbali sana mkuu
Unaona wachina wameanza kuchangamkia fursa Africa

Hata mwarabu aliambiwa mafuta yatapungua sana na watabuni mbadala wake ila ni Dubai tu akasikiliza ushauri

Na sasa unaona electric cars zimeanza na solar badala ya umeme

Usiseme ni mbali sana
 
ndo mnavojidanganyaga hivo kwa kujitia moyo. Wanachofanya wao ni kupata pesa nyingi wateke uchumi wa dunia sawasawa.

Mapesa yote hayo, washindwe kuagiza wataalamu kutoka nchi za ngozi nyeupe wenzao, eti waje kuchukua tz na kenya.

Kwanza kwao ni wajanja, uschukulie mzungu poa sana. Wenzako walishawekeza wataalam toka kitambo mpaka sasa.

Kule kuna watu special kabisa, hawatokagi ndani wamefungiwa maabara mpaka sasa wapo kazini wanaendelea na utafiti. Na wanalindwa, wanalipwa na kugharamikiwa kila kitu na serikali zao na makampuni yao makubwa. Ndo maana mnaletewa chanjo na madawa.

Sasa wewe endelea kuota ndoto zako za mchana eti mzungu aje akutafute. Mtasubiri mpaka yesu anashuka. Labda mjiongeze wenyewe mkaombe kazi kwao, na ukipewa ni bahati nasibu.
 
tusidanganyane, kwa mazingira ya sasa degree/masters sio kitu katika kutafuta mafanikio.

wewe kama umeamua kuwekeza mda wako kutafuta elimu tafuta tu ili upate maarifa. usifanye hivyo kwa kudhani kwamba itakuja kukusaidia katika safari yako ya kutafuta mafanikio ya kimaisha.

connection na bahati(zali) ndio jambo la kwanza kwa sasa. hali hii ndio chanzo cha uchawa na kujipendekeza.

huku mtaani hali ni mbaya sana kwa hawa wadogo zetu wa kizazi hiki cha mitandao.
sio wavumilivu, wana haraka sana ya kufanikiwa. matokeo yake wanaishia kujipendejeza kwa watu mpaka kufikia kufanya matendo ya aibu.
 

Kweli una haki ya kuchangia mawazo yako ila mimi nipo London na kulikuwa na mjadala kwenye bunge wapinzani wakisema kwanini tunachukua doctors kutoka africa wakati wanahitajika zaidi huko ambapo watu wao wanakufa kwa kukosa huduma na sisi tunachukua wataalamu wao?

Na sasa UK wamechukua manesi kutoka Kenya kwa sababu ya upungufu
Sasa unapopinga uje na facts zako

Mambo mengi hutokea wakati wengine wanaona ni kama ndoto au anaewaza ni mjinga


Hata hawa mwaka 1963 walisema haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…