KWELI Déjà Vu inaweza kutengenezwa kwa njia za kitaalam

KWELI Déjà Vu inaweza kutengenezwa kwa njia za kitaalam

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Hivi ni kweli kuwa teknolojia ya electroneurone inaweza kupangiliwa kwa vifaa maalumu ili kumfanya mtu kuhisi amewahi kuwa sehemu hiyo kabla, na watu wale wale huku akizungumza maneno yaleyale? (Déjà vu)

IMG_6669.jpeg
 
Tunachokijua
Umewahi kuwa na hisia za kufanya jambo fulani, kutamka maneno, kufika sehemu fulani au kupitia hali mpya ambayo unadhani tayari umewahi kuwa nayo hapo awali? Huwa una hisia kwamba baadhi ya mambo yanayokwenda kutoea huko mbele tayari unayafahamu?

Hisia hizo mara nyingi hufafanuliwa kama Déjà Vu, maneno ambayo kwa lugha ya kifaransa humaanisha “Jambo ambalo tayari umewahi kuliona”

Takwimu
Utafiti wa Marija Bošnjak Pašić et al (2018) wenye kichwa cha habari “
Many Faces of Déjà Vu: a Narrative Review” unafafanua kuwa takriban 97% ya binadamu wote wamewahi kupatwa na hali hii walau mara moja kwenye kipindi fulani kwenye maisha yao na 67% wakipatwa na hali hii mara kwa mara.

Déjà Vu hutokea zaidi kwa watu wenye umri wa miaka 15-25 na huendelea kupungua kadri umri unavyozidi kuongezeka. Pia, watu wanaokumbuka ndoto, wanaosafiri mara kwa mara, wenye mkazo (stress) pamoja na wale wanaofanya kazi ngumu sana zinazowaweka kwenye mazingira ya kuwa na uchovu mkubwa mara kwa mara huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupatwa na hali hii.

Chanzo cha Déjà Vu
Sababu za kutokea kwa Déjà Vu huwa hazipo wazi sana. Lakini, tafiti nyingi za afya zinataja uwepo wa changamoto za kimawasiliano kwenye mfumo wa taarifa za fahamu za ubongo kuwa ni chanzo cha kutokea kwa hali hii hasa ikiwa degedege/Kifafa kinachoanzia kwenye eneo la ubongo ambalo kitaalam hufahamika kama temporal lobe (Temporal lobe seizures/epilepsy) kitatokea.

Pia, wanasayansi wengine huamini kuwa hali hii husababishwa na changamoto za kiutendaji zinazotokea kwenye ubongo wakati wa kutekeleza majukumu yake.

Déjà Vu kutengenezwa kitaalam
Baada ya kufanya ufuatiliaji wa jambo hili, JamiiForums imebaini kuwa;
  1. Pamoja na sababu za kiasili zilizotajwa awali, Déjà Vu inaweza kutengenezwa kwa mtu kwa njia za kimaabara, kupitia utaratibu wa hypnosis unaohusisha utulivu mkubwa wa mtu ambao hutenganishwa na mazingira yake ya asili na kumezwa na uzoefu wa ndani wa hisia, utambuzi na taswira.
  2. Usisimuaji wa kimaabara wa umeme unaopatikana kwenye eneo la ubongo linalofahamika kama Insula, maarufu kama “electrical stimulation of the insula” unaweza pia kusazalisha Déjà Vu.
Mwanafalsafa na Mtafiti wa Ufaransa Émile Boirac ndie binadamu wa kwanza ambaye mwaka 1876 alitunga jina la Déjà Vu na kuanza kulitumia rasmi tangu wakati huo.
Bado nipo kapa...ila hili suala humtokea mtu bila ridhaa yake (super natural)..sasa kama litatengenezwa maabara huoni suala hilo litakuwa kumuingilia binaadamu kwenye kumbukumbu zake bila ruhusa......huoni ni dalili za kutengeneza akili za bandia,fikla bandia kwa kisingizio cha deja' vu
 
Bado nipo kapa...ila hili suala humtokea mtu bila ridhaa yake (super natural)..sasa kama litatengenezwa maabara huoni suala hilo litakuwa kumuingilia binaadamu kwenye kumbukumbu zake bila ruhusa......huoni ni dalili za kutengeneza akili za bandia,fikla bandia kwa kisingizio cha deja' vu
Upo sawa mkuu, nafikiri wao walilenga tu kuthibitisha kilichoulizwa na mdau kama kinaweza kutokea au la.
 
Back
Top Bottom