Saint Murano alikuja na hoja kwamba kuna mwamba nadhani ni Fernando Sucre (ambaye baadae members wengine walikuja kutoa ushuhuda juu ya kesi zake za ubabaishaji ambazo walikuwa wanaficha kisa bullying). Murano alileta uzi wa kutafuta kazi, Sucre akamwambia atafute vyeti kadhaa. Murano akatumia savings zake zote kwa shida akapata vielelezo vyote akamtumia Sucre. Jamaa alipopata akaacha kupokea simu wala kujibu PM. Murano akafungua uzi baada ya siku nyingi kutaka watu wasio na uwezo kusaidia wasiwe wanakwamisha watu na kuwaingiza gharama (baadae wajuzi wa mambo ndio walisema zile details na vyeti vitatumika kwenye utapeli na kufoji vielelezo, hivyo sio kwamba Murano kapotezewa muda ni kwamba details zake zitatumika na kuna muda anaweza kamatwa kwa tukio).
Manengelo akaja na kashfa kwa Murano akimuita mzembe, akadai hata yeye huwa anatapeliwa hela nyingi zaidi ila hasemi, akadai huwa anasaidia watu humu JF ila hawana shukrani. Watu wengi walikaa kimya hasa wadada ila mimi na raia wachache tukakomaa nae.
Kila uzi wa matapeli huwa yuko upande wa tapeli, matapeli na ID zao mpya au za zamani wanajuana naye na waliwahi fanya deals nae. Kuna wawili niliowajua PM walikuwa affiliated naye waliwahi taka kunitapeli. Kama mnakumbuka yule jamaa aliyejitangazia kifo kwa ID nyingine alafu Manengelo akaja kutoa huzuni nyingi na kudai anamfahamu wakati mtu mwenyewe hajafa.
Manengelo/Wangari kila kitu anafanya at the same time. Kuuza dagaa, kuchimba madini, mbao, kilimo, samaki, kusafirisha kwenda wapi sijui. Niliichukulia kama mbinu ya kupata watu alafu channel yake ya anaowatetea iingie kazini. Kwa asiyeeelewa atasema wanawake walimuonea wivu ila sio kweli, hakuna uwezekano wa wewe kumiliki mashimo ya madini, wakati huo uko visiwani, wakati huo ushawahi uza nguo, wakati huo una mashamba ya mpunga, wakati huo 24/7 uko JF unachamba watu, na mengine kibao.
Wangari alichofanya ni kuwashika masikio raia humu. Alizoeana kwa lazima na watu maarufu na wasio na rekodi mbaya ila vichwa ngumu kama Kiranga huwezi kuja kizembe hivi lazima wakilushtukie. Kila mtu shosti, bestie, ndugu yangu mpaka watu wakawa wanaogopa kumkosoa. Kwa mazoea yake ya kuogopwa akawa anamzodoa kila anayetapeliwa ila hiyo siku hatukukubali.
Kuna member wanasaidia na hawasemi bali aliyesaidiwa ndio anakuja kusema ila kwa Wangari yeye kila uzi wa msaada lazima aseme anasaidia watu humu, anaosaidia hawajulikani wakijitaja ndio zile ID zenye mushkeli. Ila connection alikuwa nazo kweli.
Hata hivyo sikupendezwa kabisa na yule jamaa aliyeleta mambo yao ya kimasihara. Nilimuomba afute ile comment ila alikomaa nayo