Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
DEMOKRASIA HAIWAFAI WATU AINA YA MDUDE CHADEMA
Kwa Mkono wa, Robert Heriel
Mwaka juzi niliandika makala moja iliyokuwa ikimuonya na kumrekebisha Mwanaharakati na mwana chama wa Chadema, Ndugu Mdude Chadema kuwa ukosoaji wake haufai kwani anatumia lugha chafu zilizochanganyika na matusi.
Napenda wakosoaji, warekebishaji, Wanaharakati, ambao Wana misimamo mikali na wenye lugha ngumu lakini zisizo chafu wala matusi.
Mdude Chadema yakupasa ujirekebishe tena Kwa sehemu kubwa.
Kama ulivyozoea kukosoa basi Leo hii natumia nafasi hii kukukosoa kuhusu ukosoaji wako, ikiwa hii ni mara ya pili tangu nilipokukosoa mwaka 2019.
Tumia Lugha Kali Kama za wenzako kina Malisa, Maria Sarungi, Fatma Karume, miongoni mwa wengine.
Usije sema wewe u-unique wako ni kutumia lugha chafu zenye matusi. Huo ni Upumbavu.
Niliwahi andika kuwa Demokrasia haiwafai watu Masikini na Wapumbavu.
Wapumbavu wao huitumia demokrasia Kama kichaka cha kutukana wengine, kuwadhalilisha, kuwavua nguo Kwa matusi ya nguoni kabisa.
Watu dizaini ya Mdude Chadema huweza kuvumilika Kwa Watawala wenye dharau, wanaowapuuza, na wasiojali watu wapumbavu.
Lakini Kwa Watawala wasioweza kuvumilia, watu mithili ya Mdude huweza kujikuta katika taabu, dhahama na shurba isiyoelezeka.
Mdude Chadema Kwa vile hawezi kujizuia mipaka yake ya kuongea ni hatari ikiwa atakutana na mtawala asiyejua naye kujizuia mipaka yake ya mamlaka.
Hii ni kusema,
Mdude atatumia Uhuru wake wa kuongea vibaya.
Na mtawala naye atatumia Madaraka yake vibaya.
Hata hivyo,
Mdude Chadema anaweza akawa jasiri Jambo ambalo ni zuri, lakini kuwa jasiri kipumbavu ni Jambo baya.
Uwezo mzuri wa Mdude wa kuonyesha ujasiri wake ingependeza Kama angeutumia Kwa njia nzuri ya kukosoa kama mtu mwenye hekima.
Vita ya Mdude kipindi cha nyuma dhidi ya utawala wa JPM ilikuwa vita nzuri lakini iliyoharibiwa na wachezaji, wote Mdude na JPM.
Mdude alikuwa na hoja, lakini alikuwa akizitoa Kwa njia chafu na matusi Jambo ambalo halikuwa zuri na nilimtahadharisha.
Wembe alioutumia Mdude awamu ya JPM unafahamika, ulikuwa ni wembe wenye lugha chafu, matusi na lugha zenye ukakasi. Ndio maana mpaka naandika hapa ni kutokana na kuielewa kauli yake Kwa namna hiyo, nikikusudia kumtahadharisha na kumuomba atumie mbinu nyingine.
Kwa maana Kama atatumia wembe ule ule basi mtawala naye Hana budi kutumia shoka Kama alivyokuja akifanya JPM.
JPM naye hakuona ulazima wa kutumia busara Kwa kijana atumiaye upumbavu kumshambulia. Matokeo yake tunayajua.
Mdude na wenzako WA namna yako.
Lazima uelewe kuwa kanuni ya mapambano au vita hutumia Mirror principles ambapo unashambuliwa kadiri unavyokuja.
Ukija unacheka utashumbuliwa unacheka, ukija unapiga mayowe utashumbuliwa wakiwa wanapiga mayowe.
Kanuni za kioo ambazo huzingatia law isemayo input is equal to output ndio msingi WA mapambano.
Wahenga walisema; Dawa ya Moto ni Moto.
Mdude Chadema sitaki kuamini kuwa wewe ni mpumbavu ambaye Demokrasia huiwezi.
Tafadhali, fanya Sub katika mapambano yako, ingiza akili na hekima alafu mtoe upumbavu akae bench Kwanza.
Siku zote ukitumia upumbavu basi matokeo yatakayo kupata yatafanana kiwango cha upumbavu uliowekeza. Halikadhalika na ukitumia akili, hekima na maarifa.
Pambano liendelee lakini tahadhari zizingatiwe, sheria za mchezo zisipuuzwe.
Linda nchi yako, penda watu wako.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro