Demokrasia haiwafai watu aina ya Mdude Nyagali

Demokrasia haiwafai watu aina ya Mdude Nyagali

Mdude hajakosea

Na mimi nasema hivi, kama Samia atafuata njia ileile ya kidikteta ya Magufuli, basi wembe uleule tuliotumia kumnyoa Magufuli tutamnyoa nao na yeye pia.

Mimi nampongeza Mdude kwa kauli nzuri kabisa ya kijasiri.

Kama Mdude kakosea mpelekeni mahakamani
itakua vipi na Samia akajibu mapigo na akatumi wembe aliyo tumia Magufuli? Nani atakayeumia?
 
Watu wengi sana wakiwemo wanaCHADEMA mwenzangu wamemkosoa mdude hasa kwenye hii kauli "Wembe nilioutumia kumnyoa mtangulizi wake ndio huo huo nitakaotumia kumnyoa yeye akileta jeuri". Niwe mkweli, binafsi sioni utata wala matusi yoyote kwenye hiyo kauli zaidi ya ujasiri.

Ni WAJIBU wa wanaomshambulia Mdude kumuelezea matusi yako wapi, au kutueleza wao wameelewa nini maana naona kuna Shida Kubwa ya Uelewa hasa wa FASIHI ndani ya Jamii.
 
Katiba na sheria ndivyo vinapaswa kuongoza nchi, watu wakikosea wahukumiwe kwa haki kupitia uchunguzi na mahakama huru.
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Yaani kila mtu atumie alichonacho mkononi, si ndio Mkuu
 
Katiba na sheria ndivyo vinapaswa kuongoza nchi, watu wakikosea wahukumiwe kwa haki kupitia uchunguzi na mahakama huru.

Upo sahihi Mkuu, lakini kwa watu aina ya mdude unafikiri Katiba na sheria zinaweza kuwazuia?

Upumbavu huzuiwa kwa upumbavu
 
Watu wengi sana wakiwemo wanaCHADEMA mwenzangu wamemkosoa mdude hasa kwenye hii kauli "Wembe nilioutumia kumnyoa mtangulizi wake ndio huo huo nitakaotumia kumnyoa yeye akileta jeuri". Niwe mkweli, binafsi sioni utata wala matusi yoyote kwenye hiyo kauli zaidi ya ujasiri.

Ni WAJIBU wa wanaomshambulia Mdude kumuelezea matusi yako wapi, au kutueleza wao wameelewa nini maana naona kuna Shida Kubwa ya Uelewa hasa wa FASIHI ndani ya Jamii.

Wanamkosoa kwa sababu wembe alioutumia kipindi cha Jpm unafahamika, vinginevyo hata mimi nisingeandika Mkuu.

Kama ataongea bila kufuata sheria itakuwa ni ajabu ikiwa anafikiri atajibiwa kwa kufuata sheria.
Hizo kanuni alikuwa anazitumia JPM yaani dawa ya moto ni moto.

Jambo ambalo kimsingi sio zuri na linaweza kumuumiza mmoja wapo vibaya
 
Kuna yule wa uvccm aliyetaka wapinzani kuuwawa. Yule mbunge mama mwingine aliyesemea bungeni kutaka mbunge wa upinzani auawe.

Vipi yule aliyewauwa kina Azory Mawazo Ben. Aliyewajeruhi kina Lissu, kudhulumu watu, nk.

Kuna ushauri wowote mliwahi kuwapa au ni machozi mengine ya mamba tu?
Mkuu usije cheza na mwenye dola ata siku moja,kauli anazotumia mdude ni chafu na hazifai.mwenye kuona na aone na mwenye kusikia pia asikie
 
Mdude kakumbuka mabwana zake wa jela anataka kurudi tena
 
Umekurupuka kuandika hii, unasahau hiyo demokrasia ikikosekana watu huitafuta, na uwepo wa watu wa aina ya Mdude ni madhara ya uminywaji haki za raia, na sheria za nchi.

Punguzeni mihemko mtafakari kwa kina, Mdude kudai haki hana kosa, kama unaliona niambie kwenye ile kauli yake kosa liko wapi?
 
Umekurupuka kuandika hii, unasahau hiyo demokrasia ikikosekana watu huitafuta, na uwepo wa watu wa aina ya Mdude ni madhara ya uminywaji haki za raia, na sheria za nchi, punguzeni mihemko mtafakari kwa kina. Mdude kudai haki hana kosa, kama unaliona niambie kwenye ile kauli yake kosa liko wapi?

Demokrasia ni nzuri Kwa watu wenye akili, hekima na pesa.

Demokrasia haifai watu wapumbavu, na masikini
 
Kwa Chadema lugha anayotumia huyo kijana ndio lugha tukufu katika chama chao! Anapongezwa sana kwa kuharisha kwa kutumia kinywa
 
Kama anaakili atafanya mabadiliko, Kama ni mpumbavu asubiri matokeo ya upumbavu
Kuna kauli inayosema mtu ispomfaa akili yake basi utamdhuru ujinga wake! Hii ina mantiki kubwa sana kwa watu ambao wanahisi wako salama katika kufanya vitendo vya kipuuzi kwenye jamii ili waonekane mashujaa!!!
 
DEMOKRASIA HAIWAFAI WATU AINA YA MDUDE CHADEMA

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Mwaka juzi niliandika makala moja iliyokuwa ikimuonya na kumrekebisha Mwanaharakati na mwana chama wa Chadema, Ndugu Mdude Chadema kuwa ukosoaji wake haufai kwani anatumia lugha chafu zilizochanganyika na matusi.

Napenda wakosoaji, warekebishaji, Wanaharakati, ambao Wana misimamo mikali na wenye lugha ngumu lakini zisizo chafu wala matusi.

Mdude Chadema yakupasa ujirekebishe tena Kwa sehemu kubwa.

Kama ulivyozoea kukosoa basi Leo hii natumia nafasi hii kukukosoa kuhusu ukosoaji wako, ikiwa hii ni mara ya pili tangu nilipokukosoa mwaka 2019.

Tumia Lugha Kali Kama za wenzako kina Malisa, Maria Sarungi, Fatma Karume, miongoni mwa wengine.

Usije sema wewe u-unique wako ni kutumia lugha chafu zenye matusi. Huo ni Upumbavu.

Niliwahi andika kuwa Demokrasia haiwafai watu Masikini na Wapumbavu.

Wapumbavu wao huitumia demokrasia Kama kichaka cha kutukana wengine, kuwadhalilisha, kuwavua nguo Kwa matusi ya nguoni kabisa.

Watu dizaini ya Mdude Chadema huweza kuvumilika Kwa Watawala wenye dharau, wanaowapuuza, na wasiojali watu wapumbavu.

Lakini Kwa Watawala wasioweza kuvumilia, watu mithili ya Mdude huweza kujikuta katika taabu, dhahama na shurba isiyoelezeka.

Mdude Chadema Kwa vile hawezi kujizuia mipaka yake ya kuongea ni hatari ikiwa atakutana na mtawala asiyejua naye kujizuia mipaka yake ya mamlaka.

Hii ni kusema,
Mdude atatumia Uhuru wake wa kuongea vibaya.
Na mtawala naye atatumia Madaraka yake vibaya.

Hata hivyo,
Mdude Chadema anaweza akawa jasiri Jambo ambalo ni zuri, lakini kuwa jasiri kipumbavu ni Jambo baya.

Uwezo mzuri wa Mdude wa kuonyesha ujasiri wake ingependeza Kama angeutumia Kwa njia nzuri ya kukosoa kama mtu mwenye hekima.

Vita ya Mdude kipindi cha nyuma dhidi ya utawala wa JPM ilikuwa vita nzuri lakini iliyoharibiwa na wachezaji, wote Mdude na JPM.
Mdude alikuwa na hoja, lakini alikuwa akizitoa Kwa njia chafu na matusi Jambo ambalo halikuwa zuri na nilimtahadharisha.

Wembe alioutumia Mdude awamu ya JPM unafahamika, ulikuwa ni wembe wenye lugha chafu, matusi na lugha zenye ukakasi. Ndio maana mpaka naandika hapa ni kutokana na kuielewa kauli yake Kwa namna hiyo, nikikusudia kumtahadharisha na kumuomba atumie mbinu nyingine.
Kwa maana Kama atatumia wembe ule ule basi mtawala naye Hana budi kutumia shoka Kama alivyokuja akifanya JPM.

JPM naye hakuona ulazima wa kutumia busara Kwa kijana atumiaye upumbavu kumshambulia. Matokeo yake tunayajua.

Mdude na wenzako WA namna yako.
Lazima uelewe kuwa kanuni ya mapambano au vita hutumia Mirror principles ambapo unashambuliwa kadiri unavyokuja.
Ukija unacheka utashumbuliwa unacheka, ukija unapiga mayowe utashumbuliwa wakiwa wanapiga mayowe.

Kanuni za kioo ambazo huzingatia law isemayo input is equal to output ndio msingi WA mapambano.
Wahenga walisema; Dawa ya Moto ni Moto.

Mdude Chadema sitaki kuamini kuwa wewe ni mpumbavu ambaye Demokrasia huiwezi.

Tafadhali, fanya Sub katika mapambano yako, ingiza akili na hekima alafu mtoe upumbavu akae bench Kwanza.

Siku zote ukitumia upumbavu basi matokeo yatakayo kupata yatafanana kiwango cha upumbavu uliowekeza. Halikadhalika na ukitumia akili, hekima na maarifa.

Pambano liendelee lakini tahadhari zizingatiwe, sheria za mchezo zisipuuzwe.

Linda nchi yako, penda watu wako.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
Mdude ni Malema wa tz, alichokiongea, sio tusi na siona Kama ni shida na wenda SSH rais amechukulia kawaida maana anakijua kiswahili haswa, that's alipotoa neno kudemka, Kwa fikra za kawaida ungesema ni kadhalilisha watu, ila sivyo,ila Sasa nyie wapambe ndo mmekomaa Sana

Mdude kasema, MWAMBIEN MAMA YENU, WEMBE NILIOTUMIA MNYOLEA MTANGULIZI WAKE NITATUMIA MNYOLEA YEYE KAMA KAMA HATATENDA HAKI, ivyo ieleweke Mdude alimnyoa mwendazake KWA kumkosoa hadhalani na ndo maana akawa anatekwa

Sasa kosa la Mdude kwenye maneno yake yako WAPI? au CCM Kindakindaki, maslahi, limbukeni, mmeamua kulivalia njuga ili mpote upepo wa KATIBA

NAWAOMBA RAFIKI ZANGU WANACCM HURU, waje watwambie Kama kweli Kuna shida hapa, Maana ninaona Hawa ndio wanajitambua NDANI ya CCM na wakipewa nafasi NDANI ya Chama chenu, wenda wakakirudisha Chama Katika mstari, nami napenda ccm iliyoimara ili tukakutane kwenye majukwaa, hoja KWA hoja
 
Na ndio aina ya watu wengi waliopo chadema, hiki chama lazima utolewe nati kichwani ndio unaweza kukielewa, upuuzi mtupu

Ukitaka kujua siasa ni mchezo wa ajabu, usishangae huyo Mdude kuchukuliwa na ccm kwakuwa ni maarufu, kisha kupewa madaraka na akaagizwa awe anawatukana hao cdm. Nakumbuka siku moja kwenye mkutano wa kampeni huko Geita kampeni za 2015, mbunge msukuma alikuwa anawauliza wahudhuriaji kuwa "Lowassa kafanyaje", wakawa wanajibu "kajinyea". Wakati huo Magufuli alikuwa anatabasamu kauli hizo. Leo hii aliyekuwa anatoa lugha zile chafu ni mbunge wa ccm!
 
Back
Top Bottom