Demokrasia iliyopo ndani ya CCM ni mfano wa kuigwa kwa vyama vyote Barani Afrika, hakuna wa kukiondoa madarakani

Demokrasia iliyopo ndani ya CCM ni mfano wa kuigwa kwa vyama vyote Barani Afrika, hakuna wa kukiondoa madarakani

1. Nimeishia kusoma kichwa cha uzi kisha nikaanza kusoma comment

2. Imebidi niangalie ID ya mleta mada

3. Ikabidi niangalie na profile ya mleta mada nikakuta ni ID mpya hata miezi sita haijakamilisha
4. Mleta mada anaposts elfu tatu huku reaction score zikiwa elfu moja maana yake asilimia kubwa ya post zake ni pumba/anapost kutafuta umaarufu

Nimewasilisha
 
Hata ije Tume ya uchaguzi kutoka marekani bado CCM itashinda na kupita kwa kishindooo kikubwa,kinachoibeba CCM Ni Sera na ajenda zake zinazomgusa mtanzania. Utekelezaji Bora wa ilani yake yenye kubeba masuala yote muhimu kwa wananchi ndiko kunakoifanya CCM Kuendelea kuaminika na kukubalika na watanzania
Nakuhakikishia kuwa ccm bila wizi haiwezi kushinda popote!
 
Demokrasia ya kura za NDIO na HAPANA.......
 
Hapo uliposema hakuna wakuitoa madarakani nakuunga mkono, lakini Hapo kwenye demokrasia Kama uzi wako ungekua ni dunia ama gari la kwenda mbinguni kwakweli ningekuomba nishuke(Mana mbinguni Kuna moto na pepo, gari lenu lingeruhusiwa kwenda motoni ambako kwa binafsi sihitaji kwenda huko).
Nimekuunga mkono kwa maana ya kuwa ni vigumu hicho chama kutoka madarakani kwa sababu hakiishi misingi ya demokrasia.
Moja ya definition Nyepesi ya demokrasia Ni ile isemayo demokrasia Ni serikali ya watu(raia) iliyoundwa na watu(wananchi) kwa ajili ya watu( wananchi+raia). Ila demokrasia ya chama chetu inaruhusu kupatikana serikali yao iliyoundwa na wao kwaajili yao, ugumu wa wao kutoka madarakani ndo unapatikana Hapo.
 
Ndugu zangu CCM Ni Kama Maji usipoyanywa utayaoga Tu,Huwezi ukazikwepa kuzisikia habari za CCM,huwezi ukajipa upofu wa kutokuona ukubwa na mizizi ya cccm hapa nchini,huwezi ukazuia habari za CCM na ukafanikiwa,huwezi ukaishinda CCM katika medani za kisiasa,huwezi ukaibomoa CCM hata kwa nyundo,huwezi ukaisambaratisha CCM kwa mdomo wako au fedha zako au mikono yako,huwezi ukaiteka CCM na kuifanya Kama Mali yako,huwezi ukaiteka CCM na kuiweka mfukoni mwako na ikakaa na kutosha Wala huwezi ukaihifadhi CCM katika begi lako.

CCM Ni kubwa ,Ni kubwa kuliko mtu mwingine yeyote,Ni kubwa kuliko mtu binafsi,Ni kubwa kuliko jina la mtu binafsi,CCM ni Taasisi,Taasisi iliyo imara ,nguvu na ushupavu wa kiuongozi, mizizi ya CCM Ni mirefu mikubwa ,mipana na iliyokwenda mbali sana,. Hakuna taasisis au eneo ambako hutaikuta CCM na Wana CCM,kila mahali lazima uikute CCM,lazima uione CCM,lazima uone sauti,ishara na matawi ya CCM, Ni CCM kila mahali ,Ni ccm kila eneo,Ni CCM kila uendako lazima uikute CCM na kukutana na nguvu ya CCM.

Huwezi ukaitisha Wala kuiyumbisha Wala kuikoromea CCM,.Hakuna mtu mwenye uwezo huo ,hayupo na Wala bado hajazaliwa.ukiondoka CCM kwa mbwembwe utarudi CCM kwa magoti na majuto ya kuondoka. Hakuna anayeweza kuondoka ndani ya CCM na akaiishi kwa amani uhamishoni,lazima aikumbuke CCM maana ndani ya CCM Kuna demokrasia ya kutosha na upendo wa kutosha

Hakuna ubaguzi Wala kubaguana ndani ya CCM,Hakuna udini Wala ukabila Wala ukanda ndani ya CCM,bali ndani ya CCM Kuna watu wa Dini zote,makabila yote na Kanda zote na wote wanaishi kwa amani upendo ushirikiano na mshikamano. Ndani ya CCM yeyote anaweza kuwa kiongozi wa ngazi yoyote Ile bila kujari familia aliyotokea kiuchumi. Ndani ya CCM wanachama wote Wana nafasi sawa,

Kinachokubeba kiuongozi na kuwa kiongozi ndani ya CCM ni Sera zako,sifa zako kiuongozi katika kumudu majukumu ya uongozi, kukubalika kwako na ushawishi wako kwa wanachama wenzako na mengine Kama hayo. Ndani ya CCM mfuko wako wa fedha siyo tiketi ya kupewa uongozi maana unaweza ukatoa fedha na ukanyimwa Kura.

Hakika vyama vingine Barani Afrika vina kila sababu ya kujifunza demokrasia Iliyopo Ndani ya CCM katika kuendesha mambo yake na kushughulikia migogoro ya wanachama wake. Vyama vya upinzani viache kujiendesha Kama vikundi vya watu binafsi kwa maslahi ya familia zao,visijiendshe Kama miradi ya kujipatia vipato binafsi,vsiwe Kama vitega uchumi vya watu kwa maslahi Binafsi.

Hakuna wakuitoa CCM madarakani,Hakuna chama Wala mtu mwenye ubavu huo,hayupo na Wala hajazaliwa bado. Hakuna chama chenye Sera na ajenda zenye kugusa maisha ya watanzania Kama ilivyo kwa CCM,ndio maana vyama vingine vinapuuzwa na kudharaulika Sana, huku CCM ikiendelea kukubalika na kuungwa mkono na mamillion ya watanzania kutokana na umadhubuti na ushupavu wake kiuongozi na kimfumo ulio imara na Thabiti.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa , kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627
KIJANA MZIMA UNAKUWA MJINGA KIASI HICHO KWELI
20221104_231648.jpg
 
Kama chama haikiwezi kuondoka madarakani basi hakina tofauti na Mseven, kagame nk, chama gani toka kianzianzishwe hakijawahi kuwa na rais mbovu na kumtimua hiyo ni kasoro kubwa, chama badala ya kumkemea rais au serikali serikali inakemea chama.Bunge badala ya kukemea serikali, zerikali inakemea bunge na wewe kama ni mbunge ukainua mabega kwa serikali miaka 5 ikiisha harudi tena bungeni.Hiyo ndio ccm uipendayo.
 
Back
Top Bottom