Aina hii ya fikra ndio imetufikisha pabaya. Tanzania sio kisiwa, nasema tena sio kisiwa!! Tuna mambo ya ujumla katika dunia hii. Ulichokisema ndio “chama kushika hatamu”. Utakubali kuwa hata hapa nyumbani, Lissu na marehemu Seif hawakuwa viongozi wa juu kabisa katika vyama vyao. Hii ni ishahidi kuwa kinachofanyika CCM sio utaratibu wa ki-nchi bali ki-CCM. Na Mwinyi wa Zanzibar anawezaje kuongoza Zanzibar na wakati sio hata Mwenyekiti upande wa Zanzibar? Au unasema hapa kuwa anaamliwa na Mwenyekiti/Rais wa Jamhuri mambo ya kufanya? Ikiwa ni hivo, uko wapi uhuru wa mamlaka hiyo yenye bunge na mahakama zake??
Kiazi ni kiazi tu!! Ujuaji mwingiii kumbe hakuna kitu!