Kiti cha mwenyekiti wa CCM Taifa kiko wazi baada ya kifo cha Rais Magufuli. Kinachofuata hivi sasa ni kumsimika Mama Samia Suluhu kuwa mwenyekiti mpya baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania. Hii si sawa kabisa na wala hakuna demokrasia hapo!
Kwanini kusifanyike uchaguzi ili wanachama wenye sifa washindanishwe kwa kupigiwa kura? Iko wapi demokrasia ambayo CCM inajitapa nayo? Makundi ndani ya CCM yanazaliwa kwa sababu hii. Kwani CCM isingeshinda kiti cha Urais utaratibu upi ungefuatwa kumpata mwenyekiti mpya?
Mbowe pamoja na kuwa mwenyekiti wa muda mrefu CHADEMA lakini anapigiwa kura. Hii ndiyo demokrasia.
Kitu cha ajabu kuna viongozi ndani ya CCM wakiongozwa na Polepole wameanza kujipendekeza na kujibebisha kwa Mama Samia ili waendeleze ulaji wao. Pity!
Ccm mmeanza Tabia mbaya,Sana hata x mwenyekiti kumpumzisha kwenye nyumba ya milele bado ,kumbe ndo maana mama mh rais leo katoa neno leo lenye maana mapana Sana wenye akili wamemuelewa
Leo ndo mnazungumzia Rais atokanaye na chama Cha ccm kwamba ni nongwa kuwa mwenyekiti wa chama ,imeanza lini ndani ya chama Cha ccm,Kama hata uchanguzi wa mwaka jana mlitia form moja ya mgombea wenu mkisema ndo mila na desturi ya chama, why Iyo democracy hamkuisema?
Je ni lini imetoka rais asiwe mwenyekiti wa chama katika marais waliopitia chama Cha ccm,na je katiba ya ccm kuhusu mwenyekiti wa chama unasemaje? Why mnaazisha mjadala huu leo,ku nani nyuma ya pazia,
Kama ilivyo na ilivyokua mh Rais mpya ataendelea kuwa mwenyekiti wako wa chama, leo kuanza ccm jilinganisha na chadema imeanza lini,
Ccm mkianza kumsumbua, mh Rais hivyo vivyeo wakati anakazi ngum ya kufanya mbele ,sie wananchi tutamkumbatia na tutawavulmisha mkose pa kutoke, KWA Sasa ni kujenga nchi,