Demokrasia inavyohujumiwa CCM. Mwenyekiti hana mshindani

Sumaye aliambiwa "sumu haionjwi" ni baada ya kutaka uwenyekiti. Sitazungumzia ya Zitto, Wangwe na wengineo. Siasa ni biashara mkuu

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
Sumaye huenda alikuwa ni Pandikizi, mtu wa Kitengo. Amekuwa waziri mkuu miaka 10. Anajua'' in and out'' za usalama wa Taifa.Kumpa uwenyekiti ilikuwa risk kubwa sana kwa chadema.

Ingekuwa ndio mwisho wa chdema. Rejea: Uenyekiti wa Lyatonga Mrema na NCCR -Mageuzi. Chadema na viongozi kama Mbowe, Lissu, Lema wapo kupigania chama kuliko maslahi yao binafsi. Pamoja na mbinu zote chafu za Jiwe ,lakini mapaka leo wapo chamani!
 
Kwamba nafasi ya mwenyekiti igombaniwe? Si watauana hadharani.
 
Demokrasia ziko za aina nyingi. Naona nyumbu za ufipa zimekaririshwa kuwa demokrasia ni lazima kupiga kura tu!

Hehehe!
 
Sumaye huenda alikua pandikizi wa CCM kama ambavyo Lissu ni pandikizi wa mabeberu.

Ilikua risk kumpa uenyekiti wa chadema kama ambavyo ni risk na kujitakia maafa na laana kumpa Lissu uraisi.
 
Demokrasia ziko za aina nyingi. Naona nyumbu za ufipa zimekaririshwa kuwa demokrasia ni lazima kupiga kura tu!!

Hehehe!!
Duu naona wewe ni mbuzi jike lililokubuhu! Demokrasia bila kupiga kura ni ubeberu! Ndiyo sababu unapandwa bila hiari yako!
 
Demokrasia ni pamoja na kuchagua na kuchaguliwa. Demokrasia si kupitisha wakubwa nakufunga mlango wa wengine kugombea, Demokrasia si kuteuana hata kama mtu akubaliki.

Kinachoendele CCM nikukua kwa kasi ya kuogopa uchaguzi. Hakuna kuchaguana tena CCM bali kuna kupitisha. Zaidi ya miaka 10 sasa viongozi wakuu wamekuwa awachagui na hakuna uchaguzi unaotangazwa Kama Katibu na utaratibu wa vyama vya siasa unavyotaka bali kuna utaratibu mpya wakupitisha majina kwa vitisho vya dola.

Kutokana na kukosekana courage yakuchagua na kuchaguliwa ndipo inazaliwa kauli mbiu yao kwamba hakuna kiongozi anapatikana kwenye sanduku la kura na chama kisipotumia dola kusalia madarakani kisijilaumu kikiondolewa

Kama utaratibu mpya nikupitishana lini watajenga mbibishano wa hoja kupata viongozi wenye sifa? Leo Bado siku mbili kuelekea uchaguzi wa mwenyekiti lakini watu wamebaki kunung'unika tu ndani ya chama kunyimwa nafasi kugombea na kuelekezwa kumpitisha mtu mmoja kupitia utamaduni na si uchaguzi. Je, katiba yao inasema viongoz watapatikana kwa utamaduni?

Huu unaoitwa utamaduni ndio uliopelekea wabunge na viongoz wasio na sifa kupitishwa bila kura za wananchi kwa kutumia dola na leo tunaona bunge bovu kuwahi kutokea Tanzania. Turudi kwenye uchaguzi tuache maisha ya kupe tuliyoyajenga kupitia dhana isiyo yakisheria ya utamaduni.
 
Kuwa na mgombea mmoja na huyo kupigiwa kura ni ishara ya demokrasia kuwa kubwa sana kuliko kuwa na wagombea zaidi ya mmoja ambao hawana haki sawa na matokeo kupangwa ili mmoja wanayemhitaji hapo kuna ulakini wa demokrasia. Nikikumbuka ya Nyalandu na Sumaye nabaki kushangaa.
 
We unaonaje huo UTARATIBU?hata Kama upo KATIKA Katiba ya chama.. Demokrasia KATIKA hili IPO?
Mkuu huu ni utaratibu waliokubaliana/walioridhiana.Hii ndio demokrasia yao.Na wewe hicho unachokiita demokrasia ndio utaratibu wako.
Demokrasia nayo ni utaratibu tu usitishwe na hilo neno
 
Mkuu ushauri wake ni mzuri, lakini Kwanini na wewe usingetoa hiyo alternative?! Badala ya kwemweleza, si ungeonesha kwa vitendo?!
 
Jomba si afadhali Demokrasia hii in muda maalum wa kipindi Cha uongozi say Miaka 5 mitano...vipi Demokrasia ya uenyekiti wa maisha ya mavyama mengine...unatueleza nini..hiyo Ni Demokrasia kweli au utawala wa kifalme...tuanzie hapo
 
Mkuu kwani demokrasia nini?
Kama huelewi ni kwamba, huu mfumo ndani ya CCM ulikubaliwa na wengi na hii ndiyo maana ya demokrasia.
Itakapo fika muda wana CCM wenyewe wakaona kunahaja ya kufanya mabadiriko ndipo maoni ya wengi pia yatafanyiwa kazi.
Wewe unateseka kutoka chama gani?
 
Wewe ndiyo kichwa maji kweli kweli, katiba gani unayosoma? Hivi Rais wa nchi atatoka CCM milele?
Hahaha labda tuambie kwa ndoto zako au utabiri, Rais huko baadae atatoka chama gani jomba..usitake kulazimisha vitu ambavyo havipo katika uhai wetu..huko milele kwani tutakuwepo..au wewe utakuwepo milele
 
Mbowe pamoja na kuwa mwenyekiti wa muda mrefu CHADEMA lakini anapigiwa kura. Hii ndiyo demokrasia.[emoji1548][emoji1534][emoji1752]
Anapigiwa kura au watu wanalazimika kumpigia kura kwa lazima..wewe acha bana..usitake tuseme na ya Siri za ndani..usilete mchezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…