Demokrasia inavyohujumiwa CCM. Mwenyekiti hana mshindani

Demokrasia inavyohujumiwa CCM. Mwenyekiti hana mshindani

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
Kiti cha mwenyekiti wa CCM Taifa kiko wazi baada ya kifo cha Rais Magufuli. Kinachofuata hivi sasa ni kumsimika Mama Samia Suluhu kuwa mwenyekiti mpya baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania. Hii si sawa kabisa na wala hakuna demokrasia hapo.

Kwanini kusifanyike uchaguzi ili wanachama wenye sifa washindanishwe kwa kupigiwa kura? Iko wapi demokrasia ambayo CCM inajitapa nayo? Makundi ndani ya CCM yanazaliwa kwa sababu hii. Kwani CCM isingeshinda kiti cha Urais utaratibu upi ungefuatwa kumpata mwenyekiti mpya?

Mbowe pamoja na kuwa mwenyekiti wa muda mrefu CHADEMA lakini anapigiwa kura. Hii ndiyo demokrasia.

Kitu cha ajabu kuna viongozi ndani ya CCM wakiongozwa na Polepole wameanza kujipendekeza na kujibebisha kwa Mama Samia ili waendeleze ulaji wao. Pity!
 
Soma Katiba Kiongozi.... Soma. Ni muhimu sana.. kabla hujaungumza juu ya kitu uwe unakijua atleast mara tatu zaidi ya Mtu wa kawaida..

Na tusiwe watu wa kulalamika tuuu..kila wakati.. its unhealthy.. ukiona shida sema utatuzi..sio wakutoa hewani.. soma uone uvunjifu wa taratibu kwa Mujibu wa sheria zinazoongoza swala hilo.. tupe alternative... Unatoka umefaidika kwa kujua na sisi tunasoma bandiko lako tunakuwa tumejua kupitia kwako.

Tusome au tuulize ..tusije kuandika tu for the sake of writing.
 
Ukitaka kujua kama CCM kuna demokrasia au la,fuatilia vyama vyake rafiki;Chama cha kikomunisti cha China,North Korea,Chama cha Putin,Cuba huko n.k.Ukitaka kujua tabia ya mtu angalia marafiki zake ni wa aina gani!
 
Soma Katiba Kiongozi.... Soma. Ni muhimu sana.. kabla hujaungumza juu ya kitu uwe unakijua atleast mara tatu zaidi ya Mtu wa kawaida..

Na tusiwe watu wa kulalamika tuuu..kila wakati.. its unhealthy.. ukiona shida sema utatuzi..sio wakutoa hewani.. soma uone uvunjifu wa taratibu kwa Mujibu wa sheria zinazoongoza swala hilo.. tupe alternative... Unatoka umefaidika kwa kujua na sisi tunasoma bandiko lako tunakuwa tumejua kupitia kwako.

Tusome au tuulize ..tusije kuandika tu for the sake of writing.
We unaonaje huo UTARATIBU?hata Kama upo KATIKA Katiba ya chama.. Demokrasia KATIKA hili IPO?
 
Na Chadema kwenye demokrasia ambako mwenyekiti ana miaka 20 pale kwenye kiti
Je,katiba ya chadema imekiukwa katika hilo?Mbowe amekuwa akihonga au kuwatishia wajumbe ili wamchague?
 
Hivi umekielewa ulichokiandika. Kama bado haujasoma umeposti tu soma tena.
Unatakiwa unalaumu baaada ya kuisoma Katiba ya Nchi na Katiba ya CCM
 
Je,katiba ya chadema imekiukwa katika hilo?Mbowe amekuwa akihonga au kuwatishia wajumbe ili wamchague?
Siyo tu kuhonga, bali hata kuua na kufukuza wanaojaribu kuwania nafasi hiyo. Kwanini Lowasa na Sumaye walikimbia Chadema?
 
We unaonaje huo UTARATIBU?hata Kama upo KATIKA Katiba ya chama.. Demokrasia KATIKA hili IPO?
Huwezi kuendesha nchi kama the highest ranking officer halafu uwe na bosi wako.ambaye ni kikundi kidogo tu kutoka katika kundikubwa unaloliongoza. Kwa wenye busara kama CCM tumeliona hilo ndio maana Raisi wa Jamuhuri lazima ndio awe Mwenyekiti wa Chama.

Na anakuwa mwenyekiti baada ya kuwa Rais... Sio Kabla. Regardless amepatikana Vipi.. lengo ni kuharmonize operations za taifa.

Sijui Vyama vingine vitatumia utaratibu gani vikipewa dhamana ya kuongoza.. ila natumaini busara ya utaratibu huu itaendelea kutumika.
 
. Kwanini Lowasa na Sumaye
Hawa walirudi ili kulinda maslahi yao.Dikteta Jiwe alikuwa anawatishia.Angalia mpaka mkwe wa Lowassa aliwekwa kizuizini.Sumaye alikuwa anatishiwa kunyang'anywa mashamba yake.Wazee wa watu wakakubali tu yaishe,wakarudi CCM!
 
Soma Katiba Kiongozi.... Soma. Ni muhimu sana.. kabla hujaungumza juu ya kitu uwe unakijua atleast mara tatu zaidi ya Mtu wa kawaida..

Na tusiwe watu wa kulalamika tuuu..kila wakati.. its unhealthy.. ukiona shida sema utatuzi..sio wakutoa hewani.. soma uone uvunjifu wa taratibu kwa Mujibu wa sheria zinazoongoza swala hilo.. tupe alternative... Unatoka umefaidika kwa kujua na sisi tunasoma bandiko lako tunakuwa tumejua kupitia kwako.

Tusome au tuulize ..tusije kuandika tu for the sake of writing.
Wewe ndiyo kichwa maji kweli kweli, katiba gani unayosoma? Hivi Rais wa nchi atatoka CCM milele?
 
Wewe ndiyo kichwa maji kweli kweli, katiba gani unayosoma? Hivi Rais wa nchi atatoka CCM milele?
Kuwa na hekima... Umeleta hoja..na hakuna aliyekutusi... Ukitumia muda wako kujibu kama Mwanaume ulifunzwa kwenu unakuwa unapungukiwa na nini!?

Ikiwa rais wa atatoka ADA TADEA ila asiwe mwenyekiti wa chama chake... Akirudi chamani anakuwa na mwenyekiti wake..

Kwa sheria za vyama mbalimbali... chama kinaweza kumfuta mtu uanachama...na anakosa nafasi ya kuendelea kuwa kiongozi katika.nafasi aliyogombea. Wakimfuata Rais... Au wakitumia.power hiyo kujinufaisha!?

Yaani umekaa hapo umeshashiba basi unaona wote wanaokaa kuja na hizi taratibu hayawani na vichwa maji!?
 
Back
Top Bottom