Salaam, Shalom!!
Nauliza tu,
Hawa waliotuletea DEMOKRASIA mataifa ambayo Bado tunajitafuta yalilenga nini?
Mbona wao walipokuwa wanajenga Uchumi wao, miaka mingi iliyopita mbona waliotumia mijeredi?
Yaani mtoto asiyetaka shule, mzazi ampe mtoto huyo DEMOKRASIA na uhuru Ili iweje?
DEMOKRASIA kumpa bodaboda uhuru ,asiye na lesseni anayeingilia njia ya mwendokasi makusudi yafaa ni ni?
DEMOKRASIA na uhuru usio na mipaka wa kumwachia mtoto achezee bunduki yenye risasi yafaa nini?
DEMOKRASIA Kwa wezi, waovu ,wabadhirifu yafaa nini?
Kwanini wanasiasa wote na watumishi wa umma wasipelekwe JKT Kwa lazima Kwa angalau miezi SITA wafundishwe Uzalendo Kwa viboko?
Yaani HAKI za binadamu Kwa Wasiokuwa wazalendo Kwa nchi Yao, Ina mchango Gani Kwa maendeleo yetu?
DEMOKRASIA ni ya nini Kwa wezi wa kura?
Yaani mtu auze msitu Kwa Mfano, alindwe na Sheria, mchakato uanze Polepole, kabla kesi haijaenda mahakamani, ameshahonga wote hapo juu, baada ya siku chache hakuna kesi, hakuna msitu!!
Swali: DEMOKRASIA Kwa wajinga Ina manufaa Gani?
OMBI: TULETEENI DIKTETA MWINGINE TAFADHALI!!!
Karibuni!!
Hapo kwenye JKT umekosea .
JKT ni kichaka cha kujenga wezi wanaojiamini na wasio na woga wa kuiba malo za umma.
JKT ni kichaka cha kujenga wahuni wasiotii sheria za kiraia.
JKT ingafaa tu kama nchi ingakua inaendeshwa kijeshi au kidikteta mana wamejifunza kutii kwa amri na sio kwa hiyari.
Mafano mdogo ni vijana wakiomaliza JKT wenge ndio wanaoaniriwa serikalini lakini wanageuka kuwa wezi na wanadhithirifu wasio na chembe ya utu. Tofauti na wale wa sekta binafsi ambao wanaajiriwa kwa utaallamu na ujuzi wao na wanafanya vizuri zaidi.
Mfumo wa JKT ni mfumo wa kijeshi hautakiwi utolewe kwa raia bila kiwa na malengo ya kijeshi.
Kule JKT kuna msemo mmoja 'Iba lakini usikamatwe'
Mtu anaweza akachukua hata unifomu ya mwenake akavaa alimradi asikamatwe . Akikamatwa atakipata cha mtema kuni!!
Sasa mbinu kama hizo hazimjengi mtu mwema zaidi ya mtu anayejihami kwa nafsi yake na sio ya wengine.
Mfumo wa JKT unapaswa ubadilike iwe ni sehemu ya kuwajenga watu katika kazi ,kinidhamu na kimaadili na sio woga wa kutii kwa lazima. Iwe kama inavyokuwa kwenye Seminari . Hawana purukushani za Kijeshi lakini nidhamu inakua ya hali ya juu lakini pia mtoto anajengwa kimaarifa.
JKT ile ya JPM ilikua inaanza kuleta maana na pia magereza zilianza kunadilika na kuwa zenye tija kwa jamii na kuwarekebisha wakosaji?
Jambo la pili JKT hawafundishwi kuwaheshimu watu na taasisi nyingine mfano kutii sheria na wasimamizi wake kama Polisi na Vyombo vingine . Polisi wanawaita wanawake tu. Sasa mtu asiyeheshimu wasimamizi wa sheria na sheria huyo ni mhalifu na hafai kikanidhiwa mali ya umma mana haogopi chochote wala haheshimu chochote isipokua kwa kulazimishwa na mtutu wa bunduki .
Bukina Faso ni mfano mzuri wa mageuzi ya kijamii na kiuchumi kuelekea maendeleo ya kweli.
Hongera sana Jeshi la BukinaFaso