Natamani akujibu hoja yako hapa.Labda hujui maana ya demokrasia
Demokrasia haiondoi utawala Sheria na maadili ya utu
Rudi tena shule jifunze demokrasia inavyooperate
Mimi na walio wengi watafiti na wanazuoni tunaikubali demokrasia kuwa ni mfumo mzuri wa utawala duniani kwa jamii mchanganyiko kama za kwetu
Sijui wewe mwenzetu kwa utafiti wako ni mfumo Gani wa utawala unaona unafaa
Pamoja na uliyo eleza kuhusu uzuri wa demokrasia, hapo nadhani unasahau kwamba hizi nchi zetu hizi zinazoshinikizwa tufuate demokrasia inayo toka nje, hiyo siioni kuwa ni demokrasia yetu wenyewe. Hiyo ni ya kuletewa.
Kwa hiyo, huo "ubora" unao uzungumzia wewe, pengine maswala kama haya unayasahau kuwa ni muhimu.
Unaambiwa, ukitaka tukupe msaada, fanya hivi, hizo ndizo 'values' zetu za kidemokrasia. Wewe na jamii yako huko, hamuwezi kuwa na demokrasia yenu, inayojali 'values' zenu!
Demokrasia haiwezi kuwa bidhaa inayo uzwa kwenye vipaketi.