DEMOKRASIA Kwa wajinga, wasiostaarabika, Wasiokuwa wazalendo yafaa nini?

Natamani akujibu hoja yako hapa.

Pamoja na uliyo eleza kuhusu uzuri wa demokrasia, hapo nadhani unasahau kwamba hizi nchi zetu hizi zinazoshinikizwa tufuate demokrasia inayo toka nje, hiyo siioni kuwa ni demokrasia yetu wenyewe. Hiyo ni ya kuletewa.

Kwa hiyo, huo "ubora" unao uzungumzia wewe, pengine maswala kama haya unayasahau kuwa ni muhimu.
Unaambiwa, ukitaka tukupe msaada, fanya hivi, hizo ndizo 'values' zetu za kidemokrasia. Wewe na jamii yako huko, hamuwezi kuwa na demokrasia yenu, inayojali 'values' zenu!

Demokrasia haiwezi kuwa bidhaa inayo uzwa kwenye vipaketi.
 
Ndicho nilichomaanisha.

Kiongozi ambaye atasababisha Walio chini yake kuogopa kuiba.

Mnyoofu, mzalendo kiongozi wa mfano.

Mungu ni neema, atajalia tutampata tena.
 
Ndicho nilichomaanisha.

Kiongozi ambaye atasababisha Walio chini yake kuogopa kuiba.

Mnyoofu, mzalendo kiongozi wa mfano.

Mungu ni neema, atajalia tutampata tena.
Nina imani atapatikana.
Tanzania siyo nchi ya kuchezewa chezewa na hivi vikaragosi, sijui viliokotwa wapi hivi.
 
Kwamba wananchi Wana shida na mbolea,

Mkopeshaji anakwambia pesa hii nikupayo hakikisha unanunua kondom na vilainishi Kwa ajili ya mashoga,

Na mkopo huo, shart uje kununua kondom na vilainishi kwenye kampuni Toka Nchi yetu.

Hiyo ndio sababu Magu alienda kukopa kwenye MABENKI binafsi yenye Riba kubwa maana mikopo mingi Ina masharti mabaya.

Tunahitaji tukae chini tufanye kikao Cha familia ya Watanzania wote Ili kupata namna Bora ya kujitawala.
 
Hicho kikao hata akina Mwashamba watakuwemo.....Nacheka tu mkuu 'Rabbon'.

Hapana.
Kiongozi mwenye kulijali taifa hili hawezi kupoteza muda na vikao vya namna hiyo, ingawaje naelewa umuhimu wake.

Bila kujali ilivyotokea, na kuna sababu nyingi zinazo eleweka kuhusu "Ujamaa" enzi za akina Mwalimu Nyerere. Lakini maamuzi hayakusubiri hadi akina Mwashamba wa wakati huo na wao washiriki na kukubali.

Kiongozi mwenye dira, ataonyesha njia. Ndiyo sababu tunamtafuta kiongozi wa namna hiyo ajitokeze sasa.
 
Demokrasi ni namna ya kumpata kiongozi bora. Labda hujui maana ya demokrasia.

Usipokuwa na demkrasi uta.pata kiongozi bogus kama jpm
 
Mpaka sasa bado hayo mataifa makubwa hayana Demokrasia, ni maigizo tu.
Kaangalie uingereza. Waziri mkuu akizingua siku hiyohiyo anajiudhuru kwa kupenda au kutopenda. Hii ndo maama ya demkrasia. Ila kwendu jpm alizingua kila sehemu lakini nani athubutu kumwajibisha ikiwa bunge zima aliingiza maccm kwa nguvu bila kushinda
 
Demokrasi ni namna ya kumpata kiongozi bora. Labda hujui maana ya demokrasia.

Usipokuwa na demkrasi uta.pata kiongozi bogus kama jpm
Huyo unayemdharau ndiye alifanikiwa kuwatisha wauza drugs, cocaine ikaadimika mtaani,

Ndiye aliyewatisha Majambazi wakasalimisha silaha,

Ndiye aliyefanya vitu ambavyo Hadi sasa hatujui pesa alipata wapi!!

Sasa kumbe Watz wanahitaji utisho Ili kufanya KAZI,

Mijeredi irudi tu hakuna namna.
 
Kaangalie uingereza. Waziri mkuu akizingua siku hiyohiyo anajiudhuru kwa kupenda au kutopenda. Hii ndo maama ya demkrasia. Ila kwendu jpm alizingua kila sehemu lakini nani athubutu kumwajibisha ikiwa bunge zima aliingiza maccm kwa nguvu bila kushinda
Kujiudhuru ndo nn!!
 
Sasa kama Mama Anaenda kuomba mikopo lukuki Unategemea nini? Sasa hivi majambazi yamerudi maana Yanatetewa tena Wanao onekana kutaka kukata mirija yao wanaambia waacheubabe sasa unategemea Nini?

Tuna safari ndefu sana kufikia nchi ya Ahadi. Panya wana nenepa kwenye sufuria la Unga.
 
Orijino Makasiriko Orchestra Jazz Band.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ’‰
 
Orijino Makasiriko Orchestra Jazz Band.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ’‰
DEMOKRASIA Kwa wajinga, chawa, yafaa nini?
 
Kwanini watumishi wa umma tu ndio waende JKT kwa lazima na sio watanzania wote? Na je, kwenda JKT ndio mtu anapata uzalendo? Hata jakaya, Chenge, walipita JKT.
 
Aisee jiwe azinduke atawale hata kama atakuwa mifupa mitupu nyama zitarudi baadae
 
Watanzania ni makondoo na wanafiki na wazembe tunahitaji Magufuli wa pili katili zaidi ainyooshe nchi...tukana uwezavyo lkn bila hivyo nchii ni kilema
Jizazi!

Ni wewe kweli unayesema hivi?

Kha!

Wajua nini? Hata kule kwao huko inakotoka hii demokrasia uchwara hawakuendelea kwa kubembelezana. Weengi waliendelea wakati wakitawaliwa na udikteta wa kifalme na kimalkia. Naamini kama wangekuwa na huu upuuzi unaoitwa sijui demokrasia wasingeweza kutoboa. Demokrasia imekuja wakati wengi wao wameshakuwa stable. Na mpaka sasa pamoja na demokrasia yao kuna mambo huwa hawachezi nayo. Ukicheza na ufisadi kama huu wetu wa kihayawani watakufunga. Ukicheza na ulipaji wa kodi watakufunga. Na mengine ya msingi.

Naamini hata Mchina angekuwa na hizi ngonjera sijui za demokrasia asingeweza kutoboa. Ndiyo maana mimi huwa nasema kwamba Afrika nzima Kusini mwa jangwa la Sahara tupate viongozi dizaini ya akina Magufuli na Kagame halafu tuwape miaka 30 wafanye watakavyo na baada ya hapo wote waondoke halafu turudi kwenye huu ujinga wa demokrasia. Aisee wataiacha Afrika mahali pazuri sana.

Naamini hii demokrasia ya kizungu hii ni mtego mwingine ambao wametuletea ili tusiweze kuendelea. Na demokrasia ya kweli daima ni ile inayotokana na watu wenyewe; na inaheshimu historia, mila, desturi na tamaduni zao. Sisi badooooo!
 
Ninachoweza kusema ni kwamba hujitambui. Pole sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…