Mwaka 1961 GDP Korea ya Kusini ilikuwa USD 2.42 Bilioni. GDP ya Tanganyika ilikuwa USD 2.65 Bilioni.
Mwaka 2023 GDP ya Korea ya Kusini ilifikia USD 1,818.43 Bilioni na ya Tanzania ilifikia USD 79.16 Bilioni.
Korea yake Kusini imekuwa ikiendeshwa kidemokrasia wakati Tanzania kiuhalisia (virtually) inaendeshwa kidikteta tangu tupate uhuru.
Ni fikra NYEPESI SANA kuchukulia demokrasia au udikteta kama kichocheo cha maendeleo. Kuna mambo (factors) nyingi sana zinazochangia maendeleo. Think again.
Umri WA demokrasia WA Korea kusini na Tanzania haina tofauti, Kwa kipindi cha muda mrefu Korea imeongozwa na military dictators, unajua kuwa Park Chung Hee alibadirisha katiba na kuwa rais w maisha, mwaka 1980 kulitokea maandamano ya kutaka demokrasia ambayo yaligharimu maisha ya watu zaidi ya 600, na vyombo vya ndani havikuwa vinaripoti taarifa sahihi.
Baada ya Mapinduzi ya kijeshi 1961, dikteta Park alichukua muelekeo tofauti WA kuendesha uchumi Kwa uelekeo WA export oriented economy huku wafanya biashara wakiwa wamewekewa kama kisu shingoni Kwa kulazimishwa kufuata mpango WA maendeleo WA serikali, vinginevyo serikali ya park itampa Mali zako mfanya biashara mwingine anayefanya vizuri.
Wakati huo Korea kusini ilikuwa inapokea massive support ya kifedha, kisoko na teknolojia toka Kwa USA, Japan, Germany na hata UK kwenye ship building, pia France kwenye nuclear plants
Wakati huo Tanzania ilichagua njia ambayo sio sahihi ya kutengeneza state monopolies enterprises ambazo hazikuwa na ufanisi wowote maana targets zilikuwa chini, njia za nyerere zilitenga wajasiliamali(domestic private sectors) kushika usukani WA maendeleo kiuchumi maana ujamaa hautaki matabaka
Na bahati mbaya hatukua na privilege kama za Korea Kusini toka Kwa nchi matajiri, 1961-1979 Korea kusini ilitengeneza misingi mizuri ya industrialization na uwekezaji ukaanza kutoa faida miaka 1980 hata baada ya Park kuuwawa.
Wakati huo Tanzania ikaingia kwenye kipindi kigumu Sana miaka ya 1980-ujamaa unaporomoka, china imeshabadilisha Sera zake, Na nchi ikageukia IMF na WB, Sera ambazo ziliua kabisa industrialization process nchini
Mpaka mwaka 1979 Korea kusini GDP ilifika $69 billions, wakati Tanzania ilikuwa $10, yaani zaidi ya mara 6.
Kati 1961-1993 udikteta Korea ulikuwa mkubwa kuliko Tanzania