Demokrasia ni adui wa maendeleo

Kwa hio miaka ya 90 hadi 2024 haitoshi kujipata? Miaka 34 hio, Una estimate miaka mingapi zaidi inahitajika? 100, 200, 1000 ama 10,000
 
Korea zote ziliendeshwa kidikteta. Moja ikawa tajiri nyingine bado. Hiyo iliyokuwa tajiri ikaamua kuwa na demokrasia. Sina mfumo ninaotaka, ninachotaka ni tukae chini na kutafuta mfumo utakaoweza kuteletea maendeleo.
Mwaka 1961 GDP Korea ya Kusini ilikuwa USD 2.42 Bilioni. GDP ya Tanganyika ilikuwa USD 2.65 Bilioni.

Mwaka 2023 GDP ya Korea ya Kusini ilifikia USD 1,818.43 Bilioni na ya Tanzania ilifikia USD 79.16 Bilioni.

Korea yake Kusini imekuwa ikiendeshwa kidemokrasia wakati Tanzania kiuhalisia (virtually) inaendeshwa kidikteta tangu tupate uhuru.

Ni fikra NYEPESI SANA kuchukulia demokrasia au udikteta kama kichocheo cha maendeleo. Kuna mambo (factors) nyingi sana zinazochangia maendeleo. Think again.
 
Maendeleo yanasababushwa na matumizi sahii ya akili
 
Kwa hio miaka ya 90 hadi 2024 haitoshi kujipata? Miaka 34 hio, Una estimate miaka mingapi zaidi inahitajika? 100, 200, 1000 ama 10,000

..unachokishuhudia sasa hivi katika nchi mbalimbali kina afadhali kuliko nyakati za udikteta.

..Na usisahau kwamba Udikteta nao ulijaribiwa, au ulidumu ktk nchi za Afrika, toka miaka ya 60.

..tunachotakiwa kufanya Waafrika ni kuiboresha mifumo yetu ya kiutawala, na sio kuibomoa na kurudi kwenye tawala za kiimla.

..Kwa nchi kama Tanzania ni kweli tulipitisha sheria mwaka 1993 kuwa na mfumo wa vyama vingi. Lakini tangu kipindi hicho Ccm imekuwa ikifanya kila aina ya figisu kuhujumu mfumo huo. Kwa msingi huo, huwezi kudai kwamba demokrasia imefeli wakati kinachoendelea nchini ni hujuma,na figisu dhidi ya demokrasia.
 
Huko sio kuhifadhi ni kwenda kuficha hili wala sio jambo la ajabu kwa matajiri wezi.

China inaongoza kwa Banks bora duniani tajiri au mwanasiasa anaye enda kuficha pesa Singapore au Switzerland ni mwizi anayekwepa mifumo ya kibenki ya China.
Pia China wana surplus ya dolari. Inawabidi kuzipeleka nje kuwekeza.
 
Lakini majirani zetu wamefanikiwa kutoa CCM zao na still hakuna walichofanikiwa, Zambia, Kenya na wengineo.

Mtoa mada kaongea point moja muhimu sana Kukiwa na Mfalme fisadi inakua familia moja ila kukiwa na Demokrasia mafisadi kila sehemu.

Nchi zilizoendelea ni zile ambazo zimefanikiwa kukomesha rushwa na kuangalia Strength za Nchi na ku focus kwenye hizo strength.
 
Umri WA demokrasia WA Korea kusini na Tanzania haina tofauti, Kwa kipindi cha muda mrefu Korea imeongozwa na military dictators, unajua kuwa Park Chung Hee alibadirisha katiba na kuwa rais w maisha, mwaka 1980 kulitokea maandamano ya kutaka demokrasia ambayo yaligharimu maisha ya watu zaidi ya 600, na vyombo vya ndani havikuwa vinaripoti taarifa sahihi.

Baada ya Mapinduzi ya kijeshi 1961, dikteta Park alichukua muelekeo tofauti WA kuendesha uchumi Kwa uelekeo WA export oriented economy huku wafanya biashara wakiwa wamewekewa kama kisu shingoni Kwa kulazimishwa kufuata mpango WA maendeleo WA serikali, vinginevyo serikali ya park itampa Mali zako mfanya biashara mwingine anayefanya vizuri.

Wakati huo Korea kusini ilikuwa inapokea massive support ya kifedha, kisoko na teknolojia toka Kwa USA, Japan, Germany na hata UK kwenye ship building, pia France kwenye nuclear plants

Wakati huo Tanzania ilichagua njia ambayo sio sahihi ya kutengeneza state monopolies enterprises ambazo hazikuwa na ufanisi wowote maana targets zilikuwa chini, njia za nyerere zilitenga wajasiliamali(domestic private sectors) kushika usukani WA maendeleo kiuchumi maana ujamaa hautaki matabaka

Na bahati mbaya hatukua na privilege kama za Korea Kusini toka Kwa nchi matajiri, 1961-1979 Korea kusini ilitengeneza misingi mizuri ya industrialization na uwekezaji ukaanza kutoa faida miaka 1980 hata baada ya Park kuuwawa.

Wakati huo Tanzania ikaingia kwenye kipindi kigumu Sana miaka ya 1980-ujamaa unaporomoka, china imeshabadilisha Sera zake, Na nchi ikageukia IMF na WB, Sera ambazo ziliua kabisa industrialization process nchini

Mpaka mwaka 1979 Korea kusini GDP ilifika $69 billions, wakati Tanzania ilikuwa $10, yaani zaidi ya mara 6.

Kati 1961-1993 udikteta Korea ulikuwa mkubwa kuliko Tanzania
 

Mkuu kwenye avatar yako namuona fundi Park Chung Hee

Au nimeona vibaya?
 
Kwani mtoa mada kaja na solution kwamba tuongoze nchi zetu kwa mifumo wa nchi izo ulizotaja?

Hata mimi sijatoa solution. Nime highlight the fact kwamba Africa, kwa asilimia kubwa, Haina democracy na bado inaongoza kwa umaskini na maendeleo duni which defeats argument ya mleta uzi.
 

..Kenya ya sasa hivi ina ahueni kubwa sana kulinganisha na enzi za udikteta wa Mzee Kenyatta, au Mzee Moi.
 
..Kenya ya sasa hivi ina ahueni kubwa sana kulinganisha na enzi za udikteta wa Mzee Kenyatta, au Mzee Moi.
Raisi mmoja tu ndio utasema ana ahueni Uhuru, ila kina Kibaki, Huyu Ruto na wengi tu ni so and so
 
Hata hizo Nchi zilizoendelea kuna Deep state ambayo ipo juu ya sheria, Nchi kama Usa Raisi sio kiongozi mkubwa kabisa, kuna watu ambao raisi hawezi wagusa, Deep state = Disctator = Mfalme etc
Amerika zipo Strong institutions ambazo kwa mujibu wa Katiba yao haziwezi kuingiliwa na mtu yeyote hata angekuwa mkubwa kiasi gani !
Kila taasisi inafanya mambo yake kwa mujibu wa sheria sio kwa maelekezo kutoka kwa yeyote yule !!
 
Hivi ni vituko

Yaani wewe unadhani mwanadamu mmoja mwenye mapungufu kama mimi na wewe aje hapa duniani achape wanadamu wenzie viboko kuwalazimisha kufanya vitu anavyotaka yeye?

Demokrasia ni the best form of governing

Watu wazima kama wewe wawe huru kuamua watakacho hata kama kinawaumiza ni wao kwa utashi wao ilimradi hawajavunja sheria yeyote

Na uhuru wa kuvunja sheria kila mtu apewe ilimradi awe na uwezo kuvumilia consequences zake mahakamani

Kiongozi wa serikali asimamie sheria tu,maamuzi binafsi ni maamuzi binafsi

Udikteta ni ujinga wa kuungilia maamuzi binafsi ya watu binafsi na maisha yao

Wewe simamia serikali,watu binafsi waache

Kama kusimamia serikali kama chombo ni kazi inayokushinda mpaka ufatilie uhuru wa watu binafsi tayari huna akili na hutufai

Watu wazima wakiamua kua huru bila kuvunja sheria zilizopo achana nao,unaogopa nini uhuru wa watu?

Majitu yenye low IQ hua yanakimbilia udikteta kuwatawala wanadamu wengine,shame!
 
Hawajapata Viongozi wenye maono kama kwa mfano wangempata mtu kama JPM ungeona maajabu ndani ya muda mfupi sana 😳 !

Kwahiyo kumbe tatizo ni maono sio democracy? Democracy haiwezi toa Kiongozi mwenye maono?
 
Kwahiyo kumbe tatizo ni maono sio democracy? Democracy haiwezi toa Kiongozi mwenye maono?
Demokrasia itamuwekea vikwazo vingi asiweze kutekeleza maono yake. Ataishia kufanya business as usual.
 
Amerika zipo Strong institutions ambazo kwa mujibu wa Katiba yao haziwezi kuingiliwa na mtu yeyote hata angekuwa mkubwa kiasi gani !
Kila taasisi inafanya mambo yake kwa mujibu wa sheria sio kwa maelekezo kutoka kwa yeyote yule !!
Ni rahisi kubadili sheria na kufit hao mabwana wa kubwa na pia hao jamaa wanaweza vile vile wasifuate sheria.

Nakupa mifano.
1. Matajiri Usa/West hawalipi kodi, Kodi inalipwa na walalahoi

Hii article inaongelea west kiujumla

Ukisoma hapo unaona Mabilionea wanalipwa 0.5% ya tax haifiki hata asilimia 1 wakati kina kajamba nani wanalipishwa na ndio wanaendesha nchi.


Nyengine hii inakazania hivyo hivyo

2. Hao wanaotajawa kama Deepstate whether unataka ama hutaki wakiwa na jambo lao wanafanya mfano vita vya Iraq, kwa sheria zote za kimataifa na hata Marekani hivi vita havikua halali ila umesikia hata mtu mmoja kapelekwa mbele ya vyombo vya sheria?


3. sheria zinawekwa kufaidisha wao na sio wananchi etc.
Mfano mzuri sheria ya kumiliki silaha bila kibali inafaidisha zaidi makampuni ya kutengeneza silaha kuliko wananchi
Takribani, Asilimia 58 ya Marekani wanataka stricter gun laws, wakati asilimia 26 pekee ndio wanaridhika na Sheria ya sasa ya Silaha.


Kuna mambo mengi tu yapo hivyo hao ambao wapo juu ya sheria wanafanya wanavyotaka wao. Na sio mimi na conspiracy theories tu hadi watu wakubwa kama Trump ama Putin utawasikia mara kwa mara wakiongea kuhusu hizi deep States.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…