Nimeweka studies mbili so nipo sahihi ni tafiti!!
Umesoma hadi level gani? Hakuna utafiti utafanya bila control variables. Of course kuna tofauti ya resources, FDIs, population, inflation etc na zote hizo huwa controlled. Na hizo tafiti nimeweka zimeweka hizo control variables.
So njoo na tafiti zingine zenye methodology tofauti ufanye ulinganisho sio maneno matupu
Tafiti hizo ni batili kwakuwa kuna confounders nyingi ambazo hazikuzingatiwa katika hizo tafiti. Katika nchi zenye wafalme na masulutani hakuna hata uchaguzi huko. Ni lini ulisikia uchaguzi huko Saudi Arabia, Dubai, Qatar?.
Kule Misri Rais Abdel Fattah El-Sisi aliingia madarakani kwa nguvu (bila demokrasia) na kumuondoa Rais Mohamed Morsi wa chama cha Muslim brotherhood kilichoshinda uchaguzi wa kidemokrasia, lakini uchumi wa Egypt ni mkubwa kuliko wa Ghana, Namibia, Zambia sijui na wapi ambako hawa maandazi wanasema kuna uchumi mkubwa uliochangiwa na demokrasia, nonsense!!!.
Vitu ambavyo lazima uvizingatie ni pamoja na:
1. Rangi ya ngozi ya watu wa taifa hilo:. Mabeberu walituweka weusi chingi ya jangwa la sahara kama watu wa chini sana nyuma ya watu wenye asili ya Asia na Ulaya. Mgawanyo huo kwenye mindset zao uko hadi leo. Rasilimali na bidhaa kutoka nchi za Afrika ya weusi, Asia (light color), South America na Ulaya zinapatiwa bei tofauti na mashariti tofauti kwenye masoko ya ulaya na marekani. Afrika ya weusi ndiyo inapewa bei za chini kabisa na mikopo yenye riba kubwa kuliko mataifa ya mabara mengine.
2. Uwekezaji mkubwa wa viwanda mama haufanywi kwenye nchi za Afrika ya weusi bali unawekezwa Asia, North Amerika na Ulaya hata kama hakuna demokrasia kama ya Magharibi.
3. Misaada: Kuna nchi zinapewa misaada na nchi za magharibi kwasababu tu imekubali kulinda maslahi ya nchi za magharibi kwenye nchi hiyo au ukanda huo. Kenya imekubali kulinda maslahi ya mabeberu pamoja na kukubali kuwekewa military bases na kutoa askari kwenda kupigania maslahi yao kwenye nchi fulani. Egypt inapokea mapesa mengi kutoka marekani kwasababu ya kulinda maslahi ya Israel na marekani. Hivyo unaweza kuona uchumi wao mkubwa kuliko kumbe ni mikataba tu ya muda ambayo inaweza kuvunjika wakati wowote.
4. Uchumi mkubwa wa muda tu: Kuna wakati nchi inaonekana kuwa na uchumi mkubwa kwasababu inapora mali za wengine kama vile Rewanda kule DR Congo, au uwepo wa madini ambayo yataisha baada ya muda fulani na kubakiwa na mashimo tu baada ya miaka 20. Mfano, mafuta nchi za uarabuni, dhahabu kule Botswana.