Demokrasia si kwa ajili yako na mimi. Ni mfumo wa kuwaserve elites.

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,884
Reaction score
21,175
Mfumo wowote wa utawala huwa unawekwa na watu walioshika uchumi. Upo kuwaserve walioshika uchumi.

Kabla ya ubepari kulikuwa na ukabaila. Kwenye ukabaila kunakuwa na mabwana(feudal lords/aristocrats) na watwana(serfs). Mabwana huwa wanamiliki eneo kubwa la ardhi. Wanawapangishia watwana maeneo ya kulima na wao huchukua asilimia ya mazao. Mambo yameenda hivyo kwa miaka mingi. Serikali chini ya mfumo huu zilikuwa za kifalme. Watumishi wengi wakuu kwenye serikali hizi kama wabunge, mawaziri, maafisa wakubwa jeshini na wengine wenye vyeo walitoka hili tabaka la mabwana. Aina hii ya siasa za kifalme iliwafaa sana makabaila.

Baadaye huko Ulaya Technolojia ikakua. Usafiri baharini ukaboreka na njia za biashara na masoko mapya yakafunguliwa. Kitendo hiki kikafanya wafanyabiashara kuanza kupata nguvu za kiuchumi. Wakaanza kufungua karakana/viwanda vya uzalishaji na kuajiri watu. Uchumi ukawa unatoka kwa mabwana wamiliki ardhi kwenda kwa wafanyabiashara hawa.

Mtu mwenye nguvu za kiuchumi ndiye anaamua siasa ziwaje. Hata kwenye level ya familia ipo hivyo. Hawa wafanyabiashara wakaanza kudai nguvu kuwe na siasa zinazoserve maslahi yao. Wakataka wawe na wabunge. Ndiyo chanzo za mfumo wa mabunge mawili. Lile la mabwana likawa House of Lord na la wafanyabiashara/watu wa kawaida house of commons.

Wakaanza kudai mabadiliko ya sheria za nchi. Haki za kusikilizwa. Haki na sheria za makampuni. Sheria za kodi. Haki za waajiri. Na haki nyingine nyingi. Ikafikia hadi imekuja kuwa wafalme nguvu yao ni ceremonial tu. Wakaweka mfumo ambao unawafanya wao ndiyo waweke mkuu wa nchi. Mfumo huu mpya uliotengenezwa na wafanyabiashara ndiyo ukawa demokrasia. Demokrasia ni concept ya kale sana lakini haikuweza kusimama sababu haukuwafaa wenye nguvu za kiuchumi hadi pale walipokuja wafanyabiashara/mabepari.

Sasa mabepari hawa wakataka kuja kuwekeza kwenye hizi nchi zetu za dunia ya tatu. Ili mambo yao yaende wakahitaji nchi zetu nazo ziwe na mtindo wa utawala utakaowasaidia. Ndiyo hapo wakaanza kupiga kelele nchi zetu nazo ziwe na demokrasia.

Kwa hiyo sababu kubwa ya nchi za magharibi kutupigia kelele tuwe na demokrasia si kwamba ni mfumo bora sana. Ni kwa sababu wanataka mazingira mazuri ya kiuchumi kwa ajili yao wenyewe.
 
Kaka swali kwenye maada ni upi mfumo Bora wa utawala ambayo unaweza kubwa mbadala wa Demokrasia?
 
Binafsi sifahamu. Tunaweza kaa na kuona unaotufaa. Hata ule wa chama kimoja wa Nyerere, isingekuwa sera za ujamaa ulikuwa mfumo mzuri.
 
M
Mfumo wowote wa utawala huwa unawekwa na watu walioshika uchumi. Upo kuwaserve walioshika uchumi.

Kabla ya ubepari kulikuwa na ukabaila. Kwenye ukabaila kunakuwa na mabwana(feudal lords/aristocrats) na watwana(serfs). Mabwana huwa wanamiliki eneo kubwa la ardhi. Wanawapangishia watwana maeneo ya kulima na wao huchukua asilimia ya mazao. Mambo yameenda hivyo kwa miaka mingi. Serikali chini ya mfumo huu zilikuwa za kifalme. Watumishi wengi wakuu kwenye serikali hizi kama wabunge, mawaziri, maafisa wakubwa jeshini na wengine wenye vyeo walitoka hili tabaka la mabwana. Aina hii ya siasa za kifalme iliwafaa sana makabaila.

Baadaye huko Ulaya Technolojia ikakua. Usafiri baharini ukaboreka na njia za biashara na masoko mapya yakafunguliwa. Kitendo hiki kikafanya wafanyabiashara kuanza kupata nguvu za kiuchumi. Wakaanza kufungua karakana/viwanda vya uzalishaji na kuajiri watu. Uchumi ukawa unatoka kwa mabwana wamiliki ardhi kwenda kwa wafanyabiashara hawa.

Mtu mwenye nguvu za kiuchumi ndiye anaamua siasa ziwaje. Hata kwenye level ya familia ipo hivyo. Hawa wafanyabiashara wakaanza kudai nguvu kuwe na siasa zinazoserve maslahi yao. Wakataka wawe na wabunge. Ndiyo chanzo za mfumo wa mabunge mawili. Lile la mabwana likawa House of Lord na la wafanyabiashara/watu wa kawaida house of commons.

Wakaanza kudai mabadiliko ya sheria za nchi. Haki za kusikilizwa. Haki na sheria za makampuni. Sheria za kodi. Haki za waajiri. Na haki nyingine nyingi. Ikafikia hadi imekuja kuwa wafalme nguvu yao ni ceremonial tu. Wakaweka mfumo ambao unawafanya wao ndiyo waweke mkuu wa nchi. Mfumo huu mpya uliotengenezwa na wafanyabiashara ndiyo ukawa demokrasia. Demokrasia ni concept ya kale sana lakini haikuweza kusimama sababu haukuwafaa wenye nguvu za kiuchumi hadi pale walipokuja wafanyabiashara/mabepari.

Sasa mabepari hawa wakataka kuja kuwekeza kwenye hizi nchi zetu za dunia ya tatu. Ili mambo yao yaende wakahitaji nchi zetu nazo ziwe na mtindo wa utawala utakaowasaidia. Ndiyo hapo wakaanza kupiga kelele nchi zetu nazo ziwe na demokrasia.

Kwa hiyo sababu kubwa ya nchi za magharibi kutupigia kelele tuwe na demokrasia si kwamba ni mfumo bora sana. Ni kwa sababu wanataka mazingira mazuri ya kiuchumi kwa ajili yao wenyewe.
Kabla huja walaumu wa magharibi unapaswa kujua Demekrasia ni pana sana na inagusa hadi masikini wa mwisho licha ya kuwanufaisha zaidi hao uliowataja…… Just imagine unachoma picha ya Rais na unapotezwa kama kuku na wamagharibi wakisema hii sio sawa tunaona wanataka kujinufaisha
 
Back
Top Bottom