Demokrasia vs Uchumi

Demokrasia vs Uchumi

tofyo

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2013
Posts
2,755
Reaction score
764
Kunatofauti kubwa Kati ya Demokrasia na Uchumi, na nivitu ambavyo haviendi Pamoja, lakini vilevile Ikiwa kimoja kitainuka lazima kingine kianguke.

Demokrasia katika ulingo wa kisiasa kwa upana wake haishii kwenye kuchagua na kuchaguliwa, Bali inaenda Mpaka kwenye uwajibikaji wake,

Yakwamba uwajibikaji wake wa yule aliechaguliwa ni lazima atii katiba, sheria na maadili ya utawala Bora, na pia awe anaongoza kwa mjibu washeria na kulinda haki za binaadamu.

Naweka sawa kwamba Ikiwa taratibu zote za kisheria zitafuatwa kwenye kuchagua na kuchaliwa, na kwenye na utawala wa sheria,haki za binaadamu na maadili ya utumishi wa umma na utawala Bora hapo tunasema Demokrasia imeimarika.

Upande wa pili ni upande wa uchumi, ili upate uchumi mzuri na Usimamizi mzuri wa mapato na matumizi ya serikali na Usimamizi mzuri wa rasilimali za nchi na kudhiti ufisadi,hujuma,matumizi mabaya madaraka na unyang'anyi lazima utapita katika njia za kidikteta.

Naomba kuweka sawa ya kwamba, binaadamu ili uweze kumdhibiti wizi,hujuma na ufisadi sheria tulionazo pekeyake haiwezi Bali maamuzi magumu nje ya sheria hizi zilizopo ndio zinaweza kudhiti hayo tajwa hapo juu.

Kupanga ni kuchagua.

Alipokuwepo mzee Magu alijaribu kuonyesha Hilo kwa vitendo kwa kukanyaga baadhi ya maeneo ili kuharakisha maendeleo, mfano.

Mzee alikuwa hataki kuipa muda "sheria ya manunuzi" kwasababu michakato yake inachukua muda mrefu,na alikuwa hataki utafiti wa muda mrefu "visibility study" kwenye miradi ya maendeleo. Kwahio utaona kwamba miradi ilienda Kasi lakini ilikuwa ipo nje ya sheria za manunuzi, na ndio maana mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali alikuwa anatoa riport ya upotevu wa Pesa au Pesa zilizotumika bila kufata sheria za manunuzi au manunuzi ambayo hayaja ainishwa ununuzi wake. Kwahio hio tu pekeyake NI ukiukwaji wa sheria na maadili ya utawala Bora. Huo niliotoa ni mfano tu, sio mada.

Ukitama nchi nyingi ingawa sio zote, zilipata maendeleo kwa njia ya kidikteta, sio kidemokrasia, Leo ukitaja maendeleo ya marekani huwezi kuacha kutaja utumwa wa watu weusi na ukitaja maendeleo Ufaransa, wingereza na ujerumani huwezi kuacha kutaja ukoloni.

Ukitaja China huwezi kuacha kumtaja Mao, pia huachi kutaja sheria Kali za kudhibiti ufisadi ambazo ni zakidikteta.

Ukitaja nchi za kiarabu ni lazima utaje na sheria zilizopo ambazo sio kwamba kiongozi wao hupatikana kwa njia za kidikteta Bali pia shera zao zinapingana na haki za kibinaadamu, Kama vile haki za wanawake,haki za mashoga,haki za kuishi(kwasababu kunyongwa kwao ni Kama kuku,pindi ukibainika umehujumu,umezini n.k)

Kupanga ni kuchagua.

Kwahio Demokrasia ni kichaka Cha wezi mafisadi na wahujumu wa nchi kwasababu wanajua sheria zilizopo hazina uwezo wa kuwabana, na mianya ya kupata Pesa ni mingi zaidi kwenye serikali inayofata sheria kuliko serikali yenye maamuzi nje ya sheria.

Nilichotaka niseme ni kwamba, UCHUMI ni Vita, Hakuna uchumi unaweza kusimama bila watu Fulani kubaki ili wengine waende haupo.

Na Vita ya uchumi Vita mbaya zaidi inahitaji mtu aliejitoa. Sio porojo.

Kwahio kwa Hali halisi iliopo na inayoendelea kuwepo kiuchumi Hakuna wa kumlaumu kwasababu tumechagua sheria na haki za binaadamu, kwahio hutaweza kuona watu wanatumbuliwa kwasababu tu kumtumbua mtu kwa ufisadi au sio kwa ufisadi NI udhalilishaji na ukiukwaji wa haki za kibinaadamu (haki ya kujieleza na kusikilizwa, haki ya kupata suluhu ya kimahakama nje Mahakama n.k)

Mwisho niseme kwenye uchumi Demokrasia hujitenga na kwenye Demokrasia Uchumi hujitenga.

Naomba kuwasilisha
 
Kama udictator unaleta maendeleo, basi ilitakiwa Afrika iwe tajiri zaidi, maana huku kumejaa udictator na madictator kibao.
 
Kwani rwanda mbona inapiga hatua kwa Kasi ya 4g pamoja na udictator wa kagame.
 
Hujaeleweka bado maana maongezi YAKO yote yamejikanganya,unasema ukifuata utawala wa Sheria ,kuheshimu haki za binadamu nk demokrasia inakua imekamilika .hapo hapo hujaonyesha kukamilika kwa demokrasia kunavyo zorotesha ama kuua uchumi.unahamia kwenye kusifia udikteta kwamba unaharakisha maendeleo kama alivyofanya rais aliyepita kwa kukanyaga Sheria alileta maendeleo haraka.mwisho husemi kwamba hayo maendeleo ni yepi yaliyotakana na udikteta unaousema ukilinganisha na mendeleo yaliyo letwa na watu waliyotawala kwa kufuata misingi ya demokrasia.hebu rudia tuone
 
Kama udictator unaleta maendeleo, basi ilitakiwa Afrika iwe tajiri zaidi, maana huku kumejaa udictator na madictator kibao.
Na huko China alikokwenda kuomba huyo mama yenu,ndio kiini cha udikteta ila mnafunika kombe mwanaharamu apite!

Huko ndio kuna Jamii ya Uigur ambao wamewekwa utumwani kwa malaki,wanatumikishwa bila msaada wa Dunia hihii!

Halafu huku mnafanya DOMOKULA-SIA.

China Fisadi kunyongwa sio suala la kupepesa macho!
Hapa mnawaita Asali boys !

China amri ni ya Rais pekee na Congres ya chama huwa ni kupitisha tu!

Juzi wiki mbili zilizopita,tuliona makamu mwenyekiti wa chama,akiondolewa kwa nguvu,ndani ya mkutano mkuu mbele ya Rais Xi-Jinping ,kisa tu alikuwa na hoja tofauti na mwenyekiti.

Mbona mnaenda kujikomba huko?
Demokradia ya Tanzania ni ya Majizi na Mafisadi kukwapua jasho la walalaHOI, ili wao walale HAI!

Acheni kuzugazuga humu!
Msidhani wote ni empty headed!
 
Demokrasia ni mtego wa wazungu tu,lingekua ni jambo la kuleta maendeleo kwa nchi masikini wazungu wasingelishikilia hivyo,wao nchi zao ziliendelea kwa mkono wa chuma.kuanzia US,Russia,Germany,China na huko kwingineko,

Unakuta mtu anachukia maendeleo ya nchi yake kisa anayeongoza nchi sio wa chama chake! kila jema yeye ataliponda tu! Wazungu walijenga nchi zao kwanza kisha ndio wakaanza hii issue ya demokrasia.
 
Wewe ni Brain Stream!
Umechambua pumba na mchele....ila yako majitu humu uzao wa kifisadi ambayo kazi yao ni kuponda bila tafakuri yoyote.

Hii ni hoja na topic bora ya kuigwa.

Congratulations!
 
Nani aliitawala US kwa mkono wa chuma?
Demokrasia ni mtego wa wazungu tu,lingekua ni jambo la kuleta maendeleo kwa nchi masikini wazungu wasingelishikilia hivyo,wao nchi zao ziliendelea kwa mkono wa chuma.kuanzia US,Russia,Germany,China na huko kwingineko,

Unakuta mtu anachukia maendeleo ya nchi yake kisa anayeongoza nchi sio wa chama chake! kila jema yeye ataliponda tu! Wazungu walijenga nchi zao kwanza kisha ndio wakaanza hii issue ya demokrasia.
 
Hujaeleweka bado maana maongezi YAKO yote yamejikanganya,unasema ukifuata utawala wa Sheria ,kuheshimu haki za binadamu nk demokrasia inakua imekamilika .hapo hapo hujaonyesha kukamilika kwa demokrasia kunavyo zorotesha ama kuua uchumi.unahamia kwenye kusifia udikteta kwamba unaharakisha maendeleo kama alivyofanya rais aliyepita kwa kukanyaga Sheria alileta maendeleo haraka.mwisho husemi kwamba hayo maendeleo ni yepi yaliyotakana na udikteta unaousema ukilinganisha na mendeleo yaliyo letwa na watu waliyotawala kwa kufuata misingi ya demokrasia.hebu rudia tuone
Demokrasia ikifuatwa na Kumpata Kiongozi HALALI na anatawala kwa misingi ya Utawala bora KATIBA ya Nchi hiyo itakuwa Bora hata ktk Suala la Uchumi litakuwa zuri kwa sababu ya Utawala bora
 
Na huko China alikokwenda kuomba huyo mama yenu,ndio kiini cha udikteta ila mnafunika kombe mwanaharamu apite!

Huko ndio kuna Jamii ya Uigur ambao wamewekwa utumwani kwa malaki,wanatumikishwa bila msaada wa Dunia hihii!

Halafu huku mnafanya DOMOKULA-SIA.

China Fisadi kunyongwa sio suala la kupepesa macho!
Hapa mnawaita Asali boys !

China amri ni ya Rais pekee na Congres ya chama huwa ni kupitisha tu!

Juzi wiki mbili zilizopita,tuliona makamu mwenyekiti wa chama,akiondolewa kwa nguvu,ndani ya mkutano mkuu mbele ya Rais Xi-Jinping ,kisa tu alikuwa na hoja tofauti na mwenyekiti.

Mbona mnaenda kujikomba huko?
Demokradia ya Tanzania ni ya Majizi na Mafisadi kukwapua jasho la walalaHOI, ili wao walale HAI!

Acheni kuzugazuga humu!
Msidhani wote ni empty headed!
Mkuu unachanganya vitu vingi sana kuhusu China, ningependa upitie maandishi yako tena upya.

: China sio taifa la kidikteta.
 
Government of the people, by the people, for the people.
Kama ndio hivyo basi maaelezo ya mleta mada yana mkanganyiko mkubwa sana kuhusu tafasiri sahihi ya neno“demokrasia”
 
China ni ya udikteta wa kichama zaidi japo Xi anajaribu na yeye kusimika udikteta wa mtu kupitia kutengeneza "cult of personality".
Mkuu unachanganya vitu vingi sana kuhusu China, ningependa upitie maandishi yako tena upya.

: China sio taifa la kidikteta.
 
Kama udictator unaleta maendeleo, basi ilitakiwa Afrika iwe tajiri zaidi, maana huku kumejaa udictator na madictator kibao.
Madikteta wa Africa wote ni wajinga. Zero brain kabisa
 
Hii
Kunatofauti kubwa Kati ya Demokrasia na Uchumi, na nivitu ambavyo haviendi Pamoja, lakini vilevile Ikiwa kimoja kitainuka lazima kingine kianguke.

Demokrasia katika ulingo wa kisiasa kwa upana wake haishii kwenye kuchagua na kuchaguliwa, Bali inaenda Mpaka kwenye uwajibikaji wake,

Yakwamba uwajibikaji wake wa yule aliechaguliwa ni lazima atii katiba, sheria na maadili ya utawala Bora, na pia awe anaongoza kwa mjibu washeria na kulinda haki za binaadamu.

Naweka sawa kwamba Ikiwa taratibu zote za kisheria zitafuatwa kwenye kuchagua na kuchaliwa, na kwenye na utawala wa sheria,haki za binaadamu na maadili ya utumishi wa umma na utawala Bora hapo tunasema Demokrasia imeimarika.

Upande wa pili ni upande wa uchumi, ili upate uchumi mzuri na Usimamizi mzuri wa mapato na matumizi ya serikali na Usimamizi mzuri wa rasilimali za nchi na kudhiti ufisadi,hujuma,matumizi mabaya madaraka na unyang'anyi lazima utapita katika njia za kidikteta.

Naomba kuweka sawa ya kwamba, binaadamu ili uweze kumdhibiti wizi,hujuma na ufisadi sheria tulionazo pekeyake haiwezi Bali maamuzi magumu nje ya sheria hizi zilizopo ndio zinaweza kudhiti hayo tajwa hapo juu.

Kupanga ni kuchagua.

Alipokuwepo mzee Magu alijaribu kuonyesha Hilo kwa vitendo kwa kukanyaga baadhi ya maeneo ili kuharakisha maendeleo, mfano.

Mzee alikuwa hataki kuipa muda "sheria ya manunuzi" kwasababu michakato yake inachukua muda mrefu,na alikuwa hataki utafiti wa muda mrefu "visibility study" kwenye miradi ya maendeleo. Kwahio utaona kwamba miradi ilienda Kasi lakini ilikuwa ipo nje ya sheria za manunuzi, na ndio maana mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali alikuwa anatoa riport ya upotevu wa Pesa au Pesa zilizotumika bila kufata sheria za manunuzi au manunuzi ambayo hayaja ainishwa ununuzi wake. Kwahio hio tu pekeyake NI ukiukwaji wa sheria na maadili ya utawala Bora. Huo niliotoa ni mfano tu, sio mada.

Ukitama nchi nyingi ingawa sio zote, zilipata maendeleo kwa njia ya kidikteta, sio kidemokrasia, Leo ukitaja maendeleo ya marekani huwezi kuacha kutaja utumwa wa watu weusi na ukitaja maendeleo Ufaransa, wingereza na ujerumani huwezi kuacha kutaja ukoloni.

Ukitaja China huwezi kuacha kumtaja Mao, pia huachi kutaja sheria Kali za kudhibiti ufisadi ambazo ni zakidikteta.

Ukitaja nchi za kiarabu ni lazima utaje na sheria zilizopo ambazo sio kwamba kiongozi wao hupatikana kwa njia za kidikteta Bali pia shera zao zinapingana na haki za kibinaadamu, Kama vile haki za wanawake,haki za mashoga,haki za kuishi(kwasababu kunyongwa kwao ni Kama kuku,pindi ukibainika umehujumu,umezini n.k)

Kupanga ni kuchagua.

Kwahio Demokrasia ni kichaka Cha wezi mafisadi na wahujumu wa nchi kwasababu wanajua sheria zilizopo hazina uwezo wa kuwabana, na mianya ya kupata Pesa ni mingi zaidi kwenye serikali inayofata sheria kuliko serikali yenye maamuzi nje ya sheria.

Nilichotaka niseme ni kwamba, UCHUMI ni Vita, Hakuna uchumi unaweza kusimama bila watu Fulani kubaki ili wengine waende haupo.

Na Vita ya uchumi Vita mbaya zaidi inahitaji mtu aliejitoa. Sio porojo.

Kwahio kwa Hali halisi iliopo na inayoendelea kuwepo kiuchumi Hakuna wa kumlaumu kwasababu tumechagua sheria na haki za binaadamu, kwahio hutaweza kuona watu wanatumbuliwa kwasababu tu kumtumbua mtu kwa ufisadi au sio kwa ufisadi NI udhalilishaji na ukiukwaji wa haki za kibinaadamu (haki ya kujieleza na kusikilizwa, haki ya kupata suluhu ya kimahakama nje Mahakama n.k)

Mwisho niseme kwenye uchumi Demokrasia hujitenga na kwenye Demokrasia Uchumi hujitenga.

Naomba kuwasilisha
Hii ni mada ya kijinga, haina uchambuzi wa kisomi.. sasa ngoja nikwambie bw mdogo
1. Democrasia ni sayansi, na sayansi ni ukweli na uwazi mtupu..
2. Uchumi ni sayansi na sayansi ni ukweli na uwazi mtupu.
3. Bila Demokrasia, sahau Uchumi. Demokrasia ni pana sana, inaenda mbali zaidi ya kuchagua na kuchaguliwa. Tanzania hatujafika hata 5% ya maana halisi ya demokrasia.. Demokrasia inavipa nguvu vyombo vya kutenda na kutoa haki.. Nenda Ulaya halafu utende ka kosa kadogo tu uone utakavyopambana na sheria.. lazima ufilisiwe.. hauhitaji kuwa na mpuuzi kama jiwe kuendesha uchumi katikati ya demokrasia

4. Uchumi wa kidemokrasia unahusu uchumi jumuishi (inclusive economy) ambapo taasisi zote zinatekeleza majukumu yake yote kwa uwazi, kidemokrasia na jumuishi.
Taasisi fulani haitatengeneza, haitatekeleza sheria ambazo zinawabana watu flani na kuwalinda watu fulani.. Hakuna uchumi wa hivyo wala demokrasia ya hivyo..
5. Mifano halisi.. Korea Kusini inatekeleza uchumi wa kidemokrasia.. Kila kitu kiko wazi, wananchi wanashirikishwa kila hatua ya maamuzi na utekelezaji wa sera husika.. kwa njia ya demokrasia. Korea Kusini ni next level..
6. Siasa za Jiwe alikuwa anazijuwa tu yeye.. ndo maana kwa taarifa yako, ukuaji wa uchumi uliporomoka kutoka 6.7% mwaka 2015 hadi -2% kipindi anakata moto. Naona uliamua kumuweka jiwe kama mfano, bila kujuwa kuwa udikteta wa jiwe uliharibu uchumi kiwango cha kutisha

Tuwe tunajielimisha kabla ya kuja hapa jamvini
 
Back
Top Bottom