tofyo
JF-Expert Member
- Jul 18, 2013
- 2,755
- 764
Kunatofauti kubwa Kati ya Demokrasia na Uchumi, na nivitu ambavyo haviendi Pamoja, lakini vilevile Ikiwa kimoja kitainuka lazima kingine kianguke.
Demokrasia katika ulingo wa kisiasa kwa upana wake haishii kwenye kuchagua na kuchaguliwa, Bali inaenda Mpaka kwenye uwajibikaji wake,
Yakwamba uwajibikaji wake wa yule aliechaguliwa ni lazima atii katiba, sheria na maadili ya utawala Bora, na pia awe anaongoza kwa mjibu washeria na kulinda haki za binaadamu.
Naweka sawa kwamba Ikiwa taratibu zote za kisheria zitafuatwa kwenye kuchagua na kuchaliwa, na kwenye na utawala wa sheria,haki za binaadamu na maadili ya utumishi wa umma na utawala Bora hapo tunasema Demokrasia imeimarika.
Upande wa pili ni upande wa uchumi, ili upate uchumi mzuri na Usimamizi mzuri wa mapato na matumizi ya serikali na Usimamizi mzuri wa rasilimali za nchi na kudhiti ufisadi,hujuma,matumizi mabaya madaraka na unyang'anyi lazima utapita katika njia za kidikteta.
Naomba kuweka sawa ya kwamba, binaadamu ili uweze kumdhibiti wizi,hujuma na ufisadi sheria tulionazo pekeyake haiwezi Bali maamuzi magumu nje ya sheria hizi zilizopo ndio zinaweza kudhiti hayo tajwa hapo juu.
Kupanga ni kuchagua.
Alipokuwepo mzee Magu alijaribu kuonyesha Hilo kwa vitendo kwa kukanyaga baadhi ya maeneo ili kuharakisha maendeleo, mfano.
Mzee alikuwa hataki kuipa muda "sheria ya manunuzi" kwasababu michakato yake inachukua muda mrefu,na alikuwa hataki utafiti wa muda mrefu "visibility study" kwenye miradi ya maendeleo. Kwahio utaona kwamba miradi ilienda Kasi lakini ilikuwa ipo nje ya sheria za manunuzi, na ndio maana mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali alikuwa anatoa riport ya upotevu wa Pesa au Pesa zilizotumika bila kufata sheria za manunuzi au manunuzi ambayo hayaja ainishwa ununuzi wake. Kwahio hio tu pekeyake NI ukiukwaji wa sheria na maadili ya utawala Bora. Huo niliotoa ni mfano tu, sio mada.
Ukitama nchi nyingi ingawa sio zote, zilipata maendeleo kwa njia ya kidikteta, sio kidemokrasia, Leo ukitaja maendeleo ya marekani huwezi kuacha kutaja utumwa wa watu weusi na ukitaja maendeleo Ufaransa, wingereza na ujerumani huwezi kuacha kutaja ukoloni.
Ukitaja China huwezi kuacha kumtaja Mao, pia huachi kutaja sheria Kali za kudhibiti ufisadi ambazo ni zakidikteta.
Ukitaja nchi za kiarabu ni lazima utaje na sheria zilizopo ambazo sio kwamba kiongozi wao hupatikana kwa njia za kidikteta Bali pia shera zao zinapingana na haki za kibinaadamu, Kama vile haki za wanawake,haki za mashoga,haki za kuishi(kwasababu kunyongwa kwao ni Kama kuku,pindi ukibainika umehujumu,umezini n.k)
Kupanga ni kuchagua.
Kwahio Demokrasia ni kichaka Cha wezi mafisadi na wahujumu wa nchi kwasababu wanajua sheria zilizopo hazina uwezo wa kuwabana, na mianya ya kupata Pesa ni mingi zaidi kwenye serikali inayofata sheria kuliko serikali yenye maamuzi nje ya sheria.
Nilichotaka niseme ni kwamba, UCHUMI ni Vita, Hakuna uchumi unaweza kusimama bila watu Fulani kubaki ili wengine waende haupo.
Na Vita ya uchumi Vita mbaya zaidi inahitaji mtu aliejitoa. Sio porojo.
Kwahio kwa Hali halisi iliopo na inayoendelea kuwepo kiuchumi Hakuna wa kumlaumu kwasababu tumechagua sheria na haki za binaadamu, kwahio hutaweza kuona watu wanatumbuliwa kwasababu tu kumtumbua mtu kwa ufisadi au sio kwa ufisadi NI udhalilishaji na ukiukwaji wa haki za kibinaadamu (haki ya kujieleza na kusikilizwa, haki ya kupata suluhu ya kimahakama nje Mahakama n.k)
Mwisho niseme kwenye uchumi Demokrasia hujitenga na kwenye Demokrasia Uchumi hujitenga.
Naomba kuwasilisha