Demokrasia ya Tanzania ni nzuri kuliko ya Marekani, hapa Rais hawezi kuratibu maandamano ya ghasia

Umeandika vizuri sana, bravo!
 
Alichokifanya Trump ndio kinachofanyika hapa Tanzania, ila Trump ameshindwa huo uhuni wake maana huko rais sio mungu kama hapa Tanzania, na huko taasisi zina nguvu kuliko madaraka ya rais.
Trump ameshindwa huo uhuni wake!

Kinachofanyika huko USA ni sawa na hapa Tanzania? Yaani unafananisha ustaarabu wa hapa bongo na nchi ya kishenzi? Ambayo watu wapuuzi wanaovunja na kuvamia bunge?
 
Namefurahi kwakuwa unajua ukipewa uhuru bila mipaka ni fujo.

Pia Trump "si" Rais wa kwanza kutawala muhula mmoja Marekani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kutulisha matango-pori. Harry Truman, Richard Nixon, Lyndon Johnson, Jimmy Carter, George H.W. Bush na wengine wengi walitawala muhula mmoja tu.
 
Acha uongo
 
Alichokifanya Trump ndio kinachofanyika hapa Tanzania, ila Trump ameshindwa huo uhuni wake maana huko rais sio mungu kama hapa Tanzania, na huko taasisi zina nguvu kuliko madaraka ya rais.
HUNA AKILI KWA HERUFI KUBWA
 

[A]. Uhuni wa Rais Magufuli ni mbaya zaidi maana alishindwa kwenye sanduku la kura, kwa kutumia madaraka yake ya Urais akaamuru machineries za nchi/serikali i.e jeshi, polisi, TISS, NEC nk zimshindishe (kuiba kura) kwa nguvu...

Ikaonekana hivyo mbele ya macho ya watu na dunia kuwa ameshinda. Na baada ya hapo nguvu kubwa inatumika kuulinda ushindi wake haramu..

Ole wako useme, hakushinda na wakakupata. Angeshindwa na ikatangazwa hivyo na NEC hata kwa bahati mbaya tu, ungeona ambacho kingetokea...

Rafiki yangu, yale ya Ivory Coast 2006 na Laurent Gbagbo ni cha mtoto; ya Kenya mwaka 2007 ni cha mtoto...!!

Kilichofanywa na Magufuli, ndicho anachojaribu kufanya Donald Trump kwa ujinga wake akidhani kuwa anajua na anaweza kumbe hajui na definitely hawezi kufanya vile unless aje kuwa Rais Tanzania au Uganda...!!

. Ya huko U.S.A hiyo ndiyo demokrasia halisi sasa. Kwamba, taasisi kwa maana Jeshi, FBI, Tume ya Uchaguzi, polisi, mahakama nk nk ziko huru hazina upande, haziangalii uso wala madaraka ya mtu, zinasimama katikati...

Hakuna cha "maelekezo toka juu" na ndiyo maana Incumbent President kwa ujinga wake anafanya matendo ya kijinga kabisa kujaribu kutetea madaraka yake ambayo hawezi kuyapata tena kwacha njia hizo..

Tayari hata siku 14 zilizosalia wamerekani wanaona ni mbali kwa Donald Trump kuendelea kuwa madarakani..

Utaratibu wa kumtoa kwa nguvu ya sheria (impeachment) kwa kutumia (article 25 of U.S Constitution) unafanyika. Wanasema he's mentally unfit kuendelea kushikilia ofisi hiyo...

Angalia kilichotokea huko usiku wa kuamkia leo kwa hapa Tanzania..
Your browser is not able to display this video.
Video hiyo hapo juu ni wafuasi wa Trump wakivamia Capitol Hill ili kuzuia Bunge la Congress kumuidhinisha Joe Biden. Kwa Tanzania hawa maana yake wangekuwa wafuasi Pombe Magufuli (CCM) wakipinga ushindi wa Tundu Lissu (CHADEMA). Ingekuwa ni ajabu kweli eti eeh..??

Your browser is not able to display this video.

Video hii ya pili inaonesha dunia ilivyoshangazwa na uhuni wa Rais aliyeko madarakani kuwa kinara wa vurugu..

Donald Trump alipewa Uhuru wote wa kutumia wa kidemokrasia kudai haki yake ya kushindwa. Ameenda mahakamani, ameshindwa. Amejaribu kulazimisha baadhi ya mamlaka za uchaguzi kupindua ushindi wa Biden, kushindwa..

Sasa amevuka mstari wa njia za kidemokrasia na kuamua kutumia njia za kihuni. Trump anabeba taswira ya viongozi wa aina ya Magufuli ama Yoweri Museven kwa hapa Afrika...!
 
Heri ya mwaka mpya kwako pia bwashee!
 
Yaani wewe elimu yako ndogo demokrasia siyo matakwa ya kiongozi wa nchi na chama chake bali ni matakwa ya wananchi wote kwa ujumla wao hivyo andiko lako halina mantiki.
Wananchi wenyewe ndio hawa wanaompuuza Tundu Lisu na wanamsikiliza Trump kwa swala lile lile!
 
Kwa Tanzania Rais analielekeza bunge cha kufanya na linafanya, kwanini tena ahamasishe maandamano dhidi ya bunge wakati linatekeleza aichokiakiagiza?...... yahani us wangekuwa kama Tz au chini ya Tz kidemokrasia, Trump angejichukulia mhula mwengine.
 
Kima
 
Marekani imefedheeka sana kuhusu uchaguzi wao
Tanzania kuko vizuri kuliko amerika
 
Umeona walivyomdhibiti lakini?
 
Wewe uliona wapi Rais anawashawishi wafuasi wake wakavamie bunge ambalo ni muhimili unaojitegemea?
Sasa hiyo ndiyo demokrasia, yaani rais anachochea maandamano badala ya kuyazuia. Nadhani umeongea kinyume
 
Aisee!
Kwa kweli nimem miss sana FaizaFoxy na kale kamsemo kake kuhusu elimu!
 
Nani kasema, waloruhusiwa kupanga nyanya ndani ya ofisi ya meya!
 
Trump ameshindwa huo uhuni wake!

Kinachofanyika huko USA ni sawa na hapa Tanzania? Yaani unafananisha ustaarabu wa hapa bongo na nchi ya kishenzi? Ambayo watu wapuuzi wanaovunja na kuvamia bunge?
Kubali kataa Trump angekuwa anaongoza nchi kama Tz, angeshatangazwa kuongoza mingine tena. Ni kutamka na inakuwa kama afanyavyo Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…