Demokrasia ya Tanzania ni nzuri kuliko ya Marekani, hapa Rais hawezi kuratibu maandamano ya ghasia

Hehehe... imebidi nicheke kicheko cha dharau mno.

Nchi zilizostaarabika kisiasa zinaendeshwa kwa mifumo na taasisi imara.

Hakuna mambo ya sijui mzizi umejichimbia ardhini. Mara sijui "muhimili wangu" umejikita matopeni.

Mahakama imemdhibiti Trump ipasavyo. Alitaka kuleta ulevi wake akarudishwa kwenye MSTARI.

Bunge ndio likammalizia kabisa. Kama ni jeneza basi nyundo imeshindilia msumari wa mwisho.

Ndio maana anababaika anajaribu kuwatumia manyumbu walete ghasia. Those are the last kicks of a dying horse. KWISHA HABARI YAKE.

Hakuna cha mzizi umejichimbia matopeni.

Huko Tanganyika, ndugai anaamrishwa jinsi mfalme atakavyo. Na hana jeuri ya kuleta fyoko. Athubutu aone!

Nchi inaendeshwa kama geto la machokoraa!
Umeandika vizuri sana, bravo!
 
Alichokifanya Trump ndio kinachofanyika hapa Tanzania, ila Trump ameshindwa huo uhuni wake maana huko rais sio mungu kama hapa Tanzania, na huko taasisi zina nguvu kuliko madaraka ya rais.
Trump ameshindwa huo uhuni wake!

Kinachofanyika huko USA ni sawa na hapa Tanzania? Yaani unafananisha ustaarabu wa hapa bongo na nchi ya kishenzi? Ambayo watu wapuuzi wanaovunja na kuvamia bunge?
 
Huwezi kulinganisha mwalimu na mwanafunzi. Kilichokea ni matokeo ya kumpa uhuru kupitiliza rais ambae kichwani hayupo vizuri.

America amekuwa mfano wa democracy miaka na miaka. Trump anakuwa rais wa kwanza kutawala muhula mmoja.
Na hili sio tatizo za institution za america.. bali rais mwenyewe ni jipu.. ndio maana kaondolewa
Namefurahi kwakuwa unajua ukipewa uhuru bila mipaka ni fujo.

Pia Trump "si" Rais wa kwanza kutawala muhula mmoja Marekani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kulinganisha mwalimu na mwanafunzi. Kilichokea ni matokeo ya kumpa uhuru kupitiliza rais ambae kichwani hayupo vizuri.

America amekuwa mfano wa democracy miaka na miaka. Trump anakuwa rais wa kwanza kutawala muhula mmoja.
Na hili sio tatizo za institution za america.. bali rais mwenyewe ni jipu.. ndio maana kaondolewa
Acha kutulisha matango-pori. Harry Truman, Richard Nixon, Lyndon Johnson, Jimmy Carter, George H.W. Bush na wengine wengi walitawala muhula mmoja tu.
 
Kiukweli Marekani siyo baba wa Demokrasia bali ni wababe kwenye Demokrasia. Na ukiangalia kwa makini Tanzania tuko vizuri katika kusimamia misingi ya Demokrasia kuliko Marekani.

Wewe uliona wapi Rais anawashawishi wafuasi wake wakavamie bunge ambalo ni muhimili unaojitegemea?

Itoshe tu kusema Tanzania tuko vizuri kidemokrasia.

Maendeleo hayana vyama!
Acha uongo
 
Alichokifanya Trump ndio kinachofanyika hapa Tanzania, ila Trump ameshindwa huo uhuni wake maana huko rais sio mungu kama hapa Tanzania, na huko taasisi zina nguvu kuliko madaraka ya rais.
HUNA AKILI KWA HERUFI KUBWA
 
Kiukweli Marekani siyo baba wa Demokrasia bali ni wababe kwenye Demokrasia. Na ukiangalia kwa makini Tanzania tuko vizuri katika kusimamia misingi ya Demokrasia kuliko Marekani.

Wewe uliona wapi Rais anawashawishi wafuasi wake wakavamie bunge ambalo ni muhimili unaojitegemea?

Itoshe tu kusema Tanzania tuko vizuri kidemokrasia.

Maendeleo hayana vyama!

[A]. Uhuni wa Rais Magufuli ni mbaya zaidi maana alishindwa kwenye sanduku la kura, kwa kutumia madaraka yake ya Urais akaamuru machineries za nchi/serikali i.e jeshi, polisi, TISS, NEC nk zimshindishe (kuiba kura) kwa nguvu...

Ikaonekana hivyo mbele ya macho ya watu na dunia kuwa ameshinda. Na baada ya hapo nguvu kubwa inatumika kuulinda ushindi wake haramu..

Ole wako useme, hakushinda na wakakupata. Angeshindwa na ikatangazwa hivyo na NEC hata kwa bahati mbaya tu, ungeona ambacho kingetokea...

Rafiki yangu, yale ya Ivory Coast 2006 na Laurent Gbagbo ni cha mtoto; ya Kenya mwaka 2007 ni cha mtoto...!!

Kilichofanywa na Magufuli, ndicho anachojaribu kufanya Donald Trump kwa ujinga wake akidhani kuwa anajua na anaweza kumbe hajui na definitely hawezi kufanya vile unless aje kuwa Rais Tanzania au Uganda...!!

. Ya huko U.S.A hiyo ndiyo demokrasia halisi sasa. Kwamba, taasisi kwa maana Jeshi, FBI, Tume ya Uchaguzi, polisi, mahakama nk nk ziko huru hazina upande, haziangalii uso wala madaraka ya mtu, zinasimama katikati...

Hakuna cha "maelekezo toka juu" na ndiyo maana Incumbent President kwa ujinga wake anafanya matendo ya kijinga kabisa kujaribu kutetea madaraka yake ambayo hawezi kuyapata tena kwacha njia hizo..

Tayari hata siku 14 zilizosalia wamerekani wanaona ni mbali kwa Donald Trump kuendelea kuwa madarakani..

Utaratibu wa kumtoa kwa nguvu ya sheria (impeachment) kwa kutumia (article 25 of U.S Constitution) unafanyika. Wanasema he's mentally unfit kuendelea kushikilia ofisi hiyo...

Angalia kilichotokea huko usiku wa kuamkia leo kwa hapa Tanzania..
Video hiyo hapo juu ni wafuasi wa Trump wakivamia Capitol Hill ili kuzuia Bunge la Congress kumuidhinisha Joe Biden. Kwa Tanzania hawa maana yake wangekuwa wafuasi Pombe Magufuli (CCM) wakipinga ushindi wa Tundu Lissu (CHADEMA). Ingekuwa ni ajabu kweli eti eeh..??

Video hii ya pili inaonesha dunia ilivyoshangazwa na uhuni wa Rais aliyeko madarakani kuwa kinara wa vurugu..

Donald Trump alipewa Uhuru wote wa kutumia wa kidemokrasia kudai haki yake ya kushindwa. Ameenda mahakamani, ameshindwa. Amejaribu kulazimisha baadhi ya mamlaka za uchaguzi kupindua ushindi wa Biden, kushindwa..

Sasa amevuka mstari wa njia za kidemokrasia na kuamua kutumia njia za kihuni. Trump anabeba taswira ya viongozi wa aina ya Magufuli ama Yoweri Museven kwa hapa Afrika...!
 
Tutakujibu.. hapa anaweza kuratibu yafuatayo
1. kupotea kwa watu akina Ben Saanane,
2. kupigwa risasi akina Lisu
3. Nikupe gari etc halafu umtangaze mpinzani mshindi
4. Wizi wa kura za serikali za mitaa
5. Wizi wa kura za urais
6. etc etc....................................

By the way habari za mwaka mpya? Upo?
Heri ya mwaka mpya kwako pia bwashee!
 
Yaani wewe elimu yako ndogo demokrasia siyo matakwa ya kiongozi wa nchi na chama chake bali ni matakwa ya wananchi wote kwa ujumla wao hivyo andiko lako halina mantiki.
Wananchi wenyewe ndio hawa wanaompuuza Tundu Lisu na wanamsikiliza Trump kwa swala lile lile!
 
Kiukweli Marekani siyo baba wa Demokrasia bali ni wababe kwenye Demokrasia. Na ukiangalia kwa makini Tanzania tuko vizuri katika kusimamia misingi ya Demokrasia kuliko Marekani.

Wewe uliona wapi Rais anawashawishi wafuasi wake wakavamie bunge ambalo ni muhimili unaojitegemea?

Itoshe tu kusema Tanzania tuko vizuri kidemokrasia.

Maendeleo hayana vyama!
Kwa Tanzania Rais analielekeza bunge cha kufanya na linafanya, kwanini tena ahamasishe maandamano dhidi ya bunge wakati linatekeleza aichokiakiagiza?...... yahani us wangekuwa kama Tz au chini ya Tz kidemokrasia, Trump angejichukulia mhula mwengine.
 
Kiukweli Marekani siyo baba wa Demokrasia bali ni wababe kwenye Demokrasia. Na ukiangalia kwa makini Tanzania tuko vizuri katika kusimamia misingi ya Demokrasia kuliko Marekani.

Wewe uliona wapi Rais anawashawishi wafuasi wake wakavamie bunge ambalo ni muhimili unaojitegemea?

Itoshe tu kusema Tanzania tuko vizuri kidemokrasia.

Maendeleo hayana vyama!
Kima
 
Hehehe... imebidi nicheke kicheko cha dharau mno.

Nchi zilizostaarabika kisiasa zinaendeshwa kwa mifumo na taasisi imara.

Hakuna mambo ya sijui mzizi umejichimbia ardhini. Mara sijui "muhimili wangu" umejikita matopeni.

Mahakama imemdhibiti Trump ipasavyo. Alitaka kuleta ulevi wake akarudishwa kwenye MSTARI.

Bunge ndio likammalizia kabisa. Kama ni jeneza basi nyundo imeshindilia msumari wa mwisho.

Ndio maana anababaika anajaribu kuwatumia manyumbu walete ghasia. Those are the last kicks of a dying horse. KWISHA HABARI YAKE.

Hakuna cha mzizi umejichimbia matopeni.

Huko Tanganyika, ndugai anaamrishwa jinsi mfalme atakavyo. Na hana jeuri ya kuleta fyoko. Athubutu aone!

Nchi inaendeshwa kama geto la machokoraa!
Marekani imefedheeka sana kuhusu uchaguzi wao
Tanzania kuko vizuri kuliko amerika
 
Umeona walivyomdhibiti lakini?
Kiukweli Marekani siyo baba wa Demokrasia bali ni wababe kwenye Demokrasia. Na ukiangalia kwa makini Tanzania tuko vizuri katika kusimamia misingi ya Demokrasia kuliko Marekani.

Wewe uliona wapi Rais anawashawishi wafuasi wake wakavamie bunge ambalo ni muhimili unaojitegemea?

Itoshe tu kusema Tanzania tuko vizuri kidemokrasia.

Maendeleo hayana vyama!
 
Wewe uliona wapi Rais anawashawishi wafuasi wake wakavamie bunge ambalo ni muhimili unaojitegemea?
Sasa hiyo ndiyo demokrasia, yaani rais anachochea maandamano badala ya kuyazuia. Nadhani umeongea kinyume
 
Kiukweli Marekani siyo baba wa Demokrasia bali ni wababe kwenye Demokrasia. Na ukiangalia kwa makini Tanzania tuko vizuri katika kusimamia misingi ya Demokrasia kuliko Marekani.

Wewe uliona wapi Rais anawashawishi wafuasi wake wakavamie bunge ambalo ni muhimili unaojitegemea?

Itoshe tu kusema Tanzania tuko vizuri kidemokrasia.

Maendeleo hayana vyama!
Aisee!
Kwa kweli nimem miss sana FaizaFoxy na kale kamsemo kake kuhusu elimu!
 
Kiukweli Marekani siyo baba wa Demokrasia bali ni wababe kwenye Demokrasia. Na ukiangalia kwa makini Tanzania tuko vizuri katika kusimamia misingi ya Demokrasia kuliko Marekani.

Wewe uliona wapi Rais anawashawishi wafuasi wake wakavamie bunge ambalo ni muhimili unaojitegemea?

Itoshe tu kusema Tanzania tuko vizuri kidemokrasia.

Maendeleo hayana vyama!
Nani kasema, waloruhusiwa kupanga nyanya ndani ya ofisi ya meya!
 
Trump ameshindwa huo uhuni wake!

Kinachofanyika huko USA ni sawa na hapa Tanzania? Yaani unafananisha ustaarabu wa hapa bongo na nchi ya kishenzi? Ambayo watu wapuuzi wanaovunja na kuvamia bunge?
Kubali kataa Trump angekuwa anaongoza nchi kama Tz, angeshatangazwa kuongoza mingine tena. Ni kutamka na inakuwa kama afanyavyo Magufuli.
 
Back
Top Bottom