Demokrasia ya Tanzania ni ya vichekesho sana!

Demokrasia ya Tanzania ni ya vichekesho sana!

Bongo hakuna demokrasia bali kuna maigizo ya demokrasia ambao wanafanya kijani kuwahadaa wadanganyika na mabeberu..ila kimsingi ni mambo ya hovyo sana yanavyofanywa na kijani.

#MaendeleoHayanaChama
 
angalia hata Kenya watu wanaanzisha Vyama
Siasa za Kenya nazo ni kubusu makalio ya alie Ikulu.

EOuSzgeWsAc3xFZ.jpg
 
Duh...!. Watanzania tunapenda sana kulalamika na karibu kila kitu tunamlalamikia rais!.

Usajili wa vyama ni kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, rais wa nchi hakusiki kwa namna yoyote na issues zozote za usajili wa vyama zaidi ya kuwateua watendaji.

Chama chochote kikikidhi vigezo, na kutimiza masharti, kinasajiliwa!, na chama chochote kitakacho nyimwa usajili, kinaelezwa kwa maandishi, Madam Presidaa has nothing to do with usajili wa vyama.
P
Watu wamezowea kusikia sikia kuna kitu inaitwa maagizo kutoka juu !! Hata mimi siielewi hii kitu kama ipo au haipo na hasa huwa ni maagizo gani. !! Ndio maana likitokea la kutokea kama kunyimwa usajili au kingine kama hicho basi watu wanaanza kuhisi kuwa Sauti kuu imeshaingia hapo !! Kazi Kweli Kweli !!
 
VYAMA vya UPINZANI TANZANIA ukikiacha Chama cha CHADEMA sio VYAMA vya UPINZANI kulijua hilo lazima uwe na AKILI KUBWA
Ni kweli lakini hata Chadema wapo ndani yake watu ambao ni ndivyo sivyo !! Hali kadhalika na ndani ya Ccm ni vivyo hivyo !! Chama ni taasisi ya kuwaongoza watu ili wayafikie mafanikio sio mahali pa Kutafutia utajiri humo !! Ile falsafa ya kwamba Uongozi ni wito imeshapotea kitambo sana !
 
Siasa za Kenya nazo ni kubusu makalio ya alie Ikulu.

View attachment 2393167

Hiyo picha jaribu kumchora raisi wenu hivyo kwenye Gazeti la Tanzania halafu uone banyamulenge watakachokufanya. Fikiria hivi Ruto alikuwa Makamu wa raisi Kenya Chama kimoja na Raisi wake Uhuru wakatofautiana Ruto akatoka chama cha Raisi Uhuru na kuanzisha cha kwake na kikasajiliwa kikaingia kwenye uchaguzi na kushinda hayo yote yametokea akiwa bado Makamu wa Raisi na wala hakundugaiwa sasa geuza scenario Tanzania Mpango atofautiane na Samia atoke CCM na kuanzisha Chama chake bila ya kujificha popote na Chama kusajiliwa na kuanza Kampeni against Samia, unajua kitakachompata kama watu wanafukuzwa kazi kwa kupiga picha na Raisi wa USA, ije kuwa kuanzisha Chama?
 
Duh...!. Watanzania tunapenda sana kulalamika na karibu kila kitu tunamlalamikia rais!.

Usajili wa vyama ni kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, rais wa nchi hakusiki kwa namna yoyote na issues zozote za usajili wa vyama zaidi ya kuwateua watendaji.

Chama chochote kikikidhi vigezo, na kutimiza masharti, kinasajiliwa!, na chama chochote kitakacho nyimwa usajili, kinaelezwa kwa maandishi, Madam Presidaa has nothing to do with usajili wa vyama.
P

Hata wewe mwenyewe siajabu ulichokiandika haukiamini, kila siku mnasema Raisi kajenga Barabara, raisi kajenga daraja, Samia kagawa mabilioni hayo yote mnaona ni sawa ila linapokuja swala la responsibility mnakimbia na kuruka mnasema siyo kila kitu anafanya raisi kwamba ni kazi ya msajili, kwani kujenga barabara ni kazi ya raisi ? Hakuna Waziri na Bunge la kupitisha bajeti?

Hata Ndugai mnasena alijuzulu wakati mtiririko wa matukio unakinzana na ninyi, alianza raisi kumchamba Ndugai live baada ya Ndugai kuhoji, tukasikia kajiuzulu aliyekuja kumrithi akasema Serikali iko juu ya Bunge hizo hints zote bado mnaona watu ni wajinga tu?
 
Waafrika [ watanzania ] kwa sasa tuna hitaji maendeleo hatuhitaji blah blah za majukwaani zisizo na msaada kwetu wowote ule Afrika ipo nyuma tena bado ipo nyuma sana bila kukaza mikanda hatuta fika popote pale kimaendeleo.
Jikaze mkanda mwenyewe. Shenzi!
 
Yule hakuwa spika bali jambazi. Ilikuwa halali kufurushwa.

Lakini Cheo chake kilikuwa ni Spika wa Bunge la JMTZ, hapa swala siyo personality ya mtu unaweza mchukia yeye kama yeye lkn that’s besides the point, hapa ni Cheo chake ndiyo muhimu, Spika ni Mhimili unaojitegemea sasa kudhalilishwa na kufukuzwa kazi ni jambo la ajabu sana, hayo hutokea nchi zilizopinduliwa!
 
Eti Rais wa nchi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Siasa anaweza kuzuia Chama xyz kisipewe usajili - hii ni Demokrasia au ujinga?

Nchi ya Kidemokrasia mtu yoyote anaweza kuanzisha Chama chochote popote na muda wowote, angalia hata Kenya watu wanaanzisha Vyama kila uchwao sijawahi kusikia chama kikinyimwa usajili, lkn Tanzania kuanzisha Chama ni ishu, Rais aliyeko madarakani akiona hicho chama kinaweza kuwa tishio anakipinga kinanyimwa usajili.

Ulaya watu wanaanzisha mpaka vyama vya wanywa bia, kuna vyama vya wageni tu wahamiaji Ulaya kuna vyama vya Kanisa tu vyote poa tu.

Hapa Bongo Mbatia katimuliwa kwenye Chama chake na Polisi, kisa yuko mlengo tofauti na walamba asali na amekataa kulamba asali.
Mambo magumu tu
 
Duh...!. Watanzania tunapenda sana kulalamika na karibu kila kitu tunamlalamikia rais!.

Usajili wa vyama ni kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, rais wa nchi hakusiki kwa namna yoyote na issues zozote za usajili wa vyama zaidi ya kuwateua watendaji.

Chama chochote kikikidhi vigezo, na kutimiza masharti, kinasajiliwa!, na chama chochote kitakacho nyimwa usajili, kinaelezwa kwa maandishi, Madam Presidaa has nothing to do with usajili wa vyama.
P
Hivi bado tunaitumia katiba! Nilidhani tuliiacha baada ya Magufuli kuingia madarakani, hebu weka kumbukumbu zako vizuri.
 
Serikali ina tuhuma nyingi sana dhidi yake yenyewe.

Lakinu kinakosekanika kitu kimoja nacho ni PROOF ya hayo matuhuma.

Tumbebeshe Rais tuhuma ambazo zina evidences zenye muelekeo wa kuaminisha na siyo mere accusations without facts
Ukikataa Hilo hatuna la kukusaidia.
 
Demokrasia ipi unayozungumzia hapa? Unakumbuka marehemu Dr. Wilbert Kleruu (Mkuu wa Mkoa pekee hapa Tanzania kuondolewa duniani kwa mauaji - 1971)) aliandika kitabu kiitwacho Demokrasia ya Chama Kimoja?

Hakuna demokrasia ya chama kimoja. Ndio maana mwandishi alitwangwa risasi na raia kwa udikteta wake.
 
Tunamlalamikia Rais kwasa
Duh...!. Watanzania tunapenda sana kulalamika na karibu kila kitu tunamlalamikia rais!.

Usajili wa vyama ni kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, rais wa nchi hakusiki kwa namna yoyote na issues zozote za usajili wa vyama zaidi ya kuwateua watendaji.

Chama chochote kikikidhi vigezo, na kutimiza masharti, kinasajiliwa!, na chama chochote kitakacho nyimwa usajili, kinaelezwa kwa maandishi, Madam Presidaa has nothing to do with usajili wa vyama.
P

Tunamlalamikia Rais kwasababu ndio mtendaji mkuu. Kama Rais katoa zuio la kutofanya siasa lipi litamshinda kufanya.

Halafu Rais mwenye akili akikuta mapungufu ya kisiasa anayaboresha na sio kufanya ujinga.
 
Tunamlalamikia Rais kwasa

Tunamlalamikia Rais kwasababu ndio mtendaji mkuu.
Sawa japo mkubwa ni jalala, basi ndio kila kitu yeye?!
Kama Rais katoa zuio la kutofanya siasa lipi litamshinda kufanya.
Aliyetoa zuio la kufanya mikutano ni JPM, Samia hawezi kujiondolea tuu hata kama hakubaliani na msimamo wa JPM, ataonekana ana mpinga!.

Kinachofanyika kuhusu zuio la mikutano ni kilichofanyika kwenye corona, iliundwa timu ya wataalam wakashauri. Sasa Mama kaunda kikosi kazi kitashauri!.
Halafu Rais mwenye akili akikuta mapungufu ya kisiasa anayaboresha na sio kufanya ujinga.
Mkuu hapa uwe na adabu na adabu ikushike!, unaposema rais mwenye akili anamaanisha nini?.
tutmie lugha ya heshima!, tusiwakosee adabu na kuwavunjia heshima viongozi wetu!.
P
 
Sawa japo mkubwa ni jalala, basi ndio kila kitu yeye?!

Aliyetoa zuio la kufanya mikutano ni JPM, Samia hawezi kujiondolea tuu hata kama hakubaliani na msimamo wa JPM, ataonekana ana mpinga!.

Kinachofanyika kuhusu zuio la mikutano ni kilichofanyika kwenye corona, iliundwa timu ya wataalam wakashauri. Sasa Mama kaunda kikosi kazi kitashauri!.

Mkuu hapa uwe na adabu na adabu ikushike, tumia lugha ya heshima!, unaposema rais mwenye akili anamaanisha nini?
P
Mikutano imo ndani ya katiba ila sidhani kama Korona nayo ima ndani ya katiba, kwakuwa mikutano imo ndani ya katiba ni ukiukwaji wa katiba kwa rais kuiingilia, hata hivyo uingiliaji huo ni wa uoga kwani umewazuia wenye sauti ya juu na kujiachaa asiye na sauti(CCM) atumie dola ili asikike kwa lazima.
 
Back
Top Bottom