Demokrasia ya vyama vya upinzani nchini vingi kama sio vyote inatia shaka na ukakasi

DAT BOY SU

Member
Joined
Nov 15, 2017
Posts
29
Reaction score
30
Demokrasia ya vyama vyetu vya upinzani hapa kwetu inatia mashaka sana maana vyote vimekuwa vinahubiri yale wasiotenda wala kuyafanya katika vyama vyao.

Vingine tena vimekuwa sio tena vyama vya upinzani bali vyama vya kiharakati maana wameshindwa kutofautisha ule mstari unawagawa kati yao.

Vyama vya CHADEMA, TLP, NCCR, UPDP, CHAUMA, NRD, ACT WAZALENDO na vingine kama utavingalia hivi vyama mfumo wa uongozi wao hasa wa juu bila kuwa na mahaba na vyama hivyo basi utagundua kuwa kuna pahala kuna ombwe kubwa la kiongozi ndani ya vyama hivyo ambalo linafunikwa na kelele za kiharakati na kukosoa serikali ilipo madarakani.

Viongozi wao kalibia wote ni wakudumu huku wakidanganga kwa uchaguzi wa kiini macho na kila panapokalibia chaguzi za vyama hivyo basi kumekuwa na ama kupeleka mbele tarehe za uchaguzi ama kuwafanyia figisu figisu wenzao wanaoonyesha nia ya kutaka nafasi hizo za juu za uongozi kwa kuwapa majina mabya kama usaliti.

Wametumwa ama wamenunuliwa na chama tawala hii yote ni kijiwekea mazingila ya wao kuendelea kutawala ama kuongoza vyama hivyo.

Ukitaka kuwa adui namba moja wa vyama hivyo basi wewe jaribu kukosoa ama kushauri mambo fulani ya kiongozi basi utaambulia matusi kutoka kwa viongozi wao pamoja na wanachama wao.

Viongozi wa vyama hivi hawajawahi kukosea na wala hawakosei wamejigeuza miungu watu ndani ya vyama vyao.

Ila wao wamekuwa mstari wa mbele kukosoa viongozi wa chama tawala na serikali tena bora hata wange wakosoa kwa yale ya kweli au nidhamu ni matusi na kejeli.

Tunahitaji upinzani sana ili kuendeleza, nchi yetu maana bila upinzani wa kuwakumbusha viongozi wetu mtajisahau.

Ila sasa upinzani tunaohitaji ni ule ulio makini na nia ya dhati ya kutaka kushika dola na kutoa changamoto zinazofaa kwa viongozi wetu.

Ila upinzani huu wa kusubiri ruzuku za serikali utasubiri sana.

Mwisho.
 
Ulitaka Upinzani usubiri nini kwani CCM haisubiri ruzuku?
 
Pia andika shairi lingine ukielezea demokrasia ya uchaguzi wa s/mitaa
 
CCM haitaki uwepo wa upinzani na ushahidi ni pamoja na kuzuia mikutano,kwa hivyo sio rahisi kupata Upinzani wa kweli na wenye tija kwa chama tawala kinachotaka kisikosolewe na ndio maana pamoja na kuwa madaraka kwa miaka 58 ustawi wa Taifa na watu wake pamoja na raslimali kibao Watanzania ni Maskini na ndio maana CCM yenyewe inawaita watu wake Wanyonge
 
Viongozi wao kalibia wote ni wakudumu huku wakidanganga kwa uchaguzi wa kiini macho
Ktk hili naunga mkono hoja. Ukiwasikiliza mfano wanachadema sabb wanazotoa kwann Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti.

Wanatoa sabb za kijinga kabisa, kwamba eti hakuna mwingine anayeweza kuhimili mikikimikiki na figisu za serikali ya ccm. Ebo! Kwani Mbowe alijifunzia wapi huo uvumilivu? Mbowe akifa chama hakitakuwa na mwenyekiti? Ni ujinga wa mwafrika huu.

Hii inahitimisha usemi kwamba udikteta Afrika ni asili yetu. Udikteta upo mpk majumbani mwetu kwenye familia zetu. Ndiyo maana ni ngumu sana kuwapata viongozi bora Afrika.
 
Back
Top Bottom