Baba V
JF-Expert Member
- Dec 29, 2010
- 19,479
- 9,540
Habari zenu wadau, leo asubuhi nimepata ujumbe kutoka kwa mdau Dena Amsi akinipa taarifa kuwa ameamua kuachana na Mr Rocky kutokana na tabia za Mr Rocky za kubeba beba wanawake kumchosha. Sehemu ya ujumbe huo ilisema hivi, Nanukuu "Mwenyekiti nimefikia hatua ya kuachana na mume wangu Mr Rocky baada ya kumvumilia kwa muda mrefu nikidhani kuwa angebadilika lakini nimegundua kuwa tabia ni kama ngozi huwezi kuibadili, hivyo nimeamua kujiweka pembeni aendelee na mambo yake kwa uhuru". Mwisho wa kunukuu, Kwa mujibu wa ujumbe huo ni kuwa hadi sasa Dena Amsi amekata kamba kwa Mr Rocky. Juhudi zangu kumtafuta Mr Rocky ili aelezee jambo hili zimegonga mwamba baada ya simu yake kuita muda wote bila majibu na baadae ikapokelewa na Mamndenyi ambaye baada ya kumwambia kuwa nilitaka kuongea na Mr Rocky kuhusu habari yake na Dena Amsi alinijibu kuwa Mr Rocky yuko nje ya nchi kwa mapumziko afu akasonya na kukata simu. Nimeamua kuileta hapa ili Mr Rocky aje alizungumzie hili.
Copy: Arushaone Nicas Mtei, Sefeti Erickb52, Mungi, Filipo et al.
Wasalaam Baba V.
Copy: Arushaone Nicas Mtei, Sefeti Erickb52, Mungi, Filipo et al.
Wasalaam Baba V.
Last edited by a moderator: