Deni kubwa la Taifa limevuruga mfumo wa Uchumi

Deni kubwa la Taifa limevuruga mfumo wa Uchumi

fikikungetaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2015
Posts
331
Reaction score
79
Some problems with National Debt like Tz includes;

1. It can crowd out private investment

2. It can create inflation

3. It promotes overconsumption

4. Not everyone holds the debt
 
But think ccm candidate he say yesterday in campaign that he gonna give every village 150 million but still Tanzania We have to pay 33 trillion. Thank abaut that.

Swissme
 
But think ccm candidate he say yesterday in campaign that he gonna give every village 150 million but still Tanzania We have to pay 33 trillion. Thank abaut that.

Swissme
Kwanini tusitumie tu lugha yetu ya kiswahili ambayo tunaweza kuiongea, kuisikia na kuiandika kwa ufasaha teh
 
Kwanini tusitumie tu lugha yetu ya kiswahili ambayo tunaweza kuiongea, kuisikia na kuiandika kwa ufasaha teh

Hata aliyefika darasa la saba wa zamani anaelewa hizo sentensi maana lugha ni nyepesi sana. Wewe elimu yako ipoje kwani?. Kiswahili kwa Tanzania bado sana, msingi wa Lugha yetu ya kiswahili ulikosewa tangu zamani. Kwahiyo nisamehe tu ndugu yangu!
 
Wala sijakuambia wewe mpendwa wangu, wala mie sina elimu
 
Madhara ya deni letu la taifa hatutayaona sasa hivi. Ni vile ilivokuwa kwa ugiriki yalianza siku nyingi Ila kadri mda unavozidi kwenda na deni linazidi kuwa kubwa.

Shida zitaanza kujitokeza pale deni la taifa likiwa kubwa kuliko pato la taifa GDP. yaani itakuwa na maana kwamba kinachozalishwa hakitoshi kufinance madeni ya nchi. Kama ilivokuwa kwa ugiriki.

Sasa ikishafika hapo kwa nchi kama Tanzania ambayo uchumi unakuwa kama konokono kwa maana ya uchumi halisi. Ndipo tutashuhudia matatizo kama haya; shilingi kushuka, inflation, social misery zitaongezeka kama tunavoshughudia ugiriki maana inflation na shilingi kushuka thamani kunapelekea real income ya watu inapungua hivo uwezo wa kununua mahitaji nao unashuka.

Itakuwa hatari sana cha kuomba hapa ni serikali inayokuja iweke kipaumbele cha kupunguza deni la taifa. Ila cha kushangaxa bado Naona wanasiasa wanazidi kutuahidi ku splash out money kwenye vitu visibokuwa vya msingi na sisi tunakubali tuu.

Wakati huo deni la taifa halistahimiliki tena tutakumbuka hizi hela zilizopigwa kwenye maufisadi ya mabilioni ya shilingi na sisi tukakaa kimya. Ubaya ni kwamba social misery zinapotokeaga waathirika ni raia wa chini kabisa.

Tubadilike deni la taifa linatuletea janga kubwa huko mbele
 
mwalimu wangu alinieleza kuwa kama jambo ulilolisoma shuleni kwa lugha ya kingereza huwezi kwenda kijijini kwenu ukamweleza bibi yako asiyejua kizungu bali ukamweleza kwa lugha yake ya asili na akakuelewa haijalishi unaweza kulipamba vipi kwa maneno ya kizungu itakuwa hujalielewa bali umelikalili.

wasiwasi wangu ndio huo.

Hata aliyefika darasa la saba wa zamani anaelewa hizo sentensi maana lugha ni nyepesi sana. Wewe elimu yako ipoje kwani?. Kiswahili kwa Tanzania bado sana, msingi wa Lugha yetu ya kiswahili ulikosewa tangu zamani. Kwahiyo nisamehe tu ndugu yangu!
 
Deni kama deni linaweza kuwa kubwa na lisiwe na madhara na linaweza kuwa dogo likawa na madhara.

kwa logic ya kawaida ya maisha, bakhressa anaweza kuwa anadaiwa bilioni moja na benki na isiwe tatizo lakini masikini akawa anadaiwa milini hamsini tu na ikawa tatizo.

lakini vilevile kwa bakhresa kukopa bilini moja kuanzisha shughuli ambayo haina tija au biashara ainayokufa mkopo huu ni tatizo kwake kuliko masikini aliyekopa milioni 50 ambayo ameiwekeza inazalisha faida na analipa mkopo na kupata faida.

hivyo kwangu mimi sisapoti maneno ya watu wanaotumia theory za kitaalamu tu bila kureflect the real situation na kuongelea deni la taifa.

inategemea unakopa kufanya nini na umeangalia kutokopa vilevile kufanya hilo jambo kuna faida na hasara gani.

lakini nina wasiwasi kwa tanzania hatufanyi analysis kubaini ni jambo gani tufanye na kwa utaratibu gani bali kila mmoja anaibuka na mpango wake.

kwangu mimi nadhani kuanzisha taasisi ya uchumi ambayo ina dhamana ya kuchambua mambo haya yote na kutoa mwongozo kwa taifa wakati wote nini cha kufanya ndio suluhisho.
 
Sidhani kama pesa tunazokopa zinaenda kufanya investment ambazo zitarejesha fedha hizo soon ukikopa na kuweka katika ujenzi wa barabara tu ujainvest haswa katika nchi kama hii ambayo serikali aina kampuni ya logistic. Na mikopo mingi inaenda uko sio kwenye viwanda na inayoenda kwenye kilimo still haina tija kwa sababu exportation bado ni ndogo sana na ata kwenye afya mikopo aiwezi kutengeneza faida haraka ya kulipa deni na riba yake .

Na hata hivyo mikopo uja na masharti ambayo kwa third world ni harsh sana na very exploitative.

Mgombea yeyote anayepanga kukopa atufai kwa ufupi na watanzania tuache kutumia logic za kitoto kudiscuss matter sensitive hivi.

Ubovu na madhara ya mikopo inaonekana vizuri katika nchi kama greece chukua case study apo
 
Back
Top Bottom