Madhara ya deni letu la taifa hatutayaona sasa hivi. Ni vile ilivokuwa kwa ugiriki yalianza siku nyingi Ila kadri mda unavozidi kwenda na deni linazidi kuwa kubwa.
Shida zitaanza kujitokeza pale deni la taifa likiwa kubwa kuliko pato la taifa GDP. yaani itakuwa na maana kwamba kinachozalishwa hakitoshi kufinance madeni ya nchi. Kama ilivokuwa kwa ugiriki.
Sasa ikishafika hapo kwa nchi kama Tanzania ambayo uchumi unakuwa kama konokono kwa maana ya uchumi halisi. Ndipo tutashuhudia matatizo kama haya; shilingi kushuka, inflation, social misery zitaongezeka kama tunavoshughudia ugiriki maana inflation na shilingi kushuka thamani kunapelekea real income ya watu inapungua hivo uwezo wa kununua mahitaji nao unashuka.
Itakuwa hatari sana cha kuomba hapa ni serikali inayokuja iweke kipaumbele cha kupunguza deni la taifa. Ila cha kushangaxa bado Naona wanasiasa wanazidi kutuahidi ku splash out money kwenye vitu visibokuwa vya msingi na sisi tunakubali tuu.
Wakati huo deni la taifa halistahimiliki tena tutakumbuka hizi hela zilizopigwa kwenye maufisadi ya mabilioni ya shilingi na sisi tukakaa kimya. Ubaya ni kwamba social misery zinapotokeaga waathirika ni raia wa chini kabisa.
Tubadilike deni la taifa linatuletea janga kubwa huko mbele