Deni la marekani lafikia dollar trilion 37, wachunge sana marekani isije ikauzwa!

Deni la marekani lafikia dollar trilion 37, wachunge sana marekani isije ikauzwa!

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
23,234
Reaction score
28,473
Deni la Marekani Limefikia Zaidi ya Dola Trilioni 37 kwa Mara ya Kwanza Maishani Hapa ikiwa na maana kwamba Deni limekua kubwa mara dufu kuliko Uchumi wao wa Dolla T 30.

Unaweza jifunza jambo hapa kwamba Unacho tangaziwa kuhusu Uchumi wa Marekani si halisia, Ni ajabu kwa taifa kama la Marekani linalo jitangaza kua ndio Taifa lenye Uchumi mkubwa kuliko Taifa lolote duniani lina daiwa pesa Nyingi na Bank ya watu wa China pamoja na nchi zingine kama Japan hii imekaaje kichwani kwako ?

Hapa kuna orodha iliyokamilika ya nchi zinazodai U.S. kwa njia ya hati za deni (Treasury securities) — takwimu zote ni za hivi karibuni kabisa kutoka kwa mfumo wa U.S. Treasury (TIC) na ripoti za machapisho ya uchambuzi:

Nchi 20 Za Juu Zinazodai Marekani (kwa Aprili–Mei 2025)

Kulingana na data ya Treasury International Capital (MFH table – Mei 2025):

Japan: $1.135 trilioni (Mei 2025)

Uingereza: $809.4 bilioni

China (Mainland): $756.3 bilioni

Cayman Islands: $441.3 bilioni

Canada: $430.1 bilioni

Ubelgiji (Belgium): $415.5 bilioni

Luxembourg: $412.6 bilioni

Ufaransa (France): $375.1 bilioni

Ireland: $327.3 bilioni

Uswisi (Switzerland): $303.7 bilioni

Taiwan: takriban $287 bilioni (Reuters 2025-02)

Singapore: takriban $248 bilioni (Reuters 2025-02)

(Orodha inaendelea hadi nchi 20, ikiwa na India, Hong Kong, nk.)

Muhtasari kwa Kundi la Kwanza (Top 5)

Nchi Kiwango cha Deni (USD)

Japan ~$1.13 trilioni
Uingereza ~$809 bilioni
China ~$756 bilioni
Cayman Islands ~$441 bilioni
Canada ~$430 bilioni

Marekani inadaiwa na Nchi Zaidi ya nchi 100 zinashikilia hati za deni za Marekani, ikijumuisha serikali, benki kuu na wawekezaji binafsi.

Marekani imefikisha kiwango cha juu kabisa cha deni la taifa, likizidi dola trilioni 37 kwa mara ya kwanza katika historia yake.

Hii ni ongezeko la zaidi ya dola bilioni 780 tangu mipaka ya deni (debt ceiling) ilipoongezwa, kufuatia kutangazwa kwa sheria ya “One Big Beautiful Bill Act” tarehe 4 Julai.

Hali hii inamaanisha deni la taifa linaongezeka kwa wastani wa dola bilioni 22 kwa siku.

Tunaona sasa Marekani inakwenda kua mtumwa wa China na mataifa mwingine kama ilivyo zoea kuzifanya Nchi zingine kua Watumwa wake.

Taifa la China ndio Taifa linalo kopesha nchi nyingi kwa Sasa kuliko taifa lolote, China imejikita katika Siasa ya biashara ikikataa vita, China inaamini Vita ina Hasara sana sio Sehemu ya mafanikio yao.
#crocodiletooth news agency plc.Inc..
1754811696792.jpg
 
Mtoa mada unajichanganya sana asee

Kwanza asilimia kubwa ya deni la Marekani ni deni la ndani, yaani wananchi wameikopesha Serikali yao, so kinacho patikana kinarudi mifukoni mwa wananchi wao, tofauti na sisi tunaoenda kukopa mabenki ya kibiashara India huko, tunaijenga India

Pili, hatifungani si deni, ni uwekezaji wa muda mrefu mitaji, yaani unatafuta tajiri mwenye mzunguko mkubwa wa pesa, unampa pesa zako afanyie mambo yake

Halafu anakuwa anakugawia ka asilimia fulani ka mapato kwa mwaka au miezi kadhaa.

Cha ajabu siku Marekani ikivurugwa ikasema Japani na China njooni mchukue pesa zenu, China na Mjapani wanaweza kukimbia hata mahakamani kushtaki.

Unaturudishiaje pesa kabla ya wakati tuliokubaliana?,
Halafu sisi tuzipeleke wapi?,
Nani mwenye uchumi mkubwa kuweza kuzizungusha tupate faida?

Tatu neno uchumi mkubwa , ni tofauti na neno uchumi mzuri.

Nimeona unajichanganya sana katika hayo maeneo.
 
Soma mpaka mwisho,utaelewa vizuri.
 
Marekani inadai dollar ngapi?

Je marekani anatoa dollar kwenye United Nations NGOs?
 
Yaani mpare mmoja kutoka Kilimanjaro Mwanga aje amshauri Mmarekani!!! Kweli huku ni kuutumia uhuru kupitiliza.
 
Back
Top Bottom