Deni la Marekani ni $34 trillioni

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2009
Posts
4,175
Reaction score
2,294
Ukistaajabu ya Musa, utashangaa ya Farao.

Deni la Marekani kwa takwimu za 2023, limefikia $34 trilioni. Kiwango hiki kinaifanya Marekani kuwa kinara wa deni kubwa kabisa duniani. Kumbe hata matajiri wanakopa!

Chanzo:

Reuters
https://www.reuters.com/world/us/total-us-public-debt-tops-34-trillion...

US public debt tops $34 trln as Congress heads into funding fight

The U.S. federal government's total public debt has reached $34 trillion for the first time, the U.S. Treasury Department reported on Tuesday as members

My take: Ukiukumbatia ubebari, raha yake ni kukopa. Japo kulipa ni majanga.
 
Wakichapisha noti za kutosha deni wakalipa wanapata hasara gani?
 
Halafu wanakimbilia kuomba visa nchi inayokaribia kufilisika! Pathetic!
 
Hao matajiri hawakopi kama nyie masikini.
Wanauza Treasury bills na Treasury bonds, deni lao halina dhamana ya kitu chochote cha thamani.
 
Mkuu fanya utafiti kwanza ingawa deni la USA ni kubwa kuliko GDP yake lakini still kuna mataifa mengi yana hali mbaya sana kuliko USA.
Funding of wars across the world ndio imechangia kiasi kikubwa.
 
Ukikopa halafu ukaenda kuzitumia kunyonya nchi za watu ukapata mara mbili basi wewe utakuwa na akili. Ila ukikopa halafu ndege zako baadae zikakamatwa sijui hapo inakuwaje
Hii mentality ya wazungu kuja kunyonya nchi zingne ili wao wawe matajiri sijui ilitokeaga wapi. Kama kweli utajiri huo upo kwetu kweli swali ni je kwann hatunufaiki nao na sisi tuwe matajiri kama hao wazungu mnaosema walikuja iba na kunyonya mali zetu...
Ukwel ni kwamba wazungu wanapambana na sie wengine ni watazamaji tu..wazee wa lawama
 
Deni la Marekani hata likifika trilioni 100 hakuna tatizo katika kulilipa. Madeni yake na sisi wajinga huku ni tofauti kabisa. Yeye ndiyo anachapisha pesa inayotumika dunia nzima. Habari kuwa anadaiwa na sijui debt ceiling ni maigizo tu.
 
Kukopa ni jambo la lazima ili upige hatua zaidi ni lazima ukope zaidi lakini kimkakati na kwa malengo maalumu, mikopo ya hasara ni ile ya kukopa utengenezaji barabara then utengenezaji barabara ya low quality inayoharibika within 2yrs, hii ni mbaya Sana, mimi crocodiletooth nasema kopa fedha tengeneza barabara ya kudumu kwa miaka 50-100, (fanya kazi maliza tatizo)
-Tuachane na wale wapuuzi eti nchi itauzwa hii.
 
Sio walikuja. Wapo na wananyonya. Inahitaji bajeti kubwa kuwa dominant. Mwenye kisu kikali ndio anakula. Kwenye gesi leo nikikuuliza hesabu zake unazijua? Kwenye madini? Ni watanzania wangapi wanamigodi / NI CONTRACTORS wangapi wa kitanzania hupewa contracts USA? Sasa kama wewe unajua unyonyaji ni mpaka waje na mijeledi nakushauri ubadili mentality yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…