Deni la Marekani ni $34 trillioni

Deni la Marekani ni $34 trillioni

Baada ya kushtukia hilo, Gadaffi alisema mafuta ni madini, yatauzwa kwa wateja wao, hususan Marekani kwa kubadilishana na madini kama dhahabu. Baada ya beberu kuu kuona hilo, akaona kiama chake kimefika. Akaona bora amuwaishe huyo mwamba Gadaffi.
UONGO,
Hakuna nchi inaweza kukubali kurudi kwenye barter trade karne hii.
 
Deni la US liko kwa sarafu yao dollar
Tanzania deni letu liko katika sarafu ya dollar, anachofanya Mmarekani anajikopesha mwenyewe na kujilipa. Ndomana tunasema economics hoax
Mimi si mwanauchumi wa kusoma (ila wa mitaani tu), kwani ukikopa toka kwenye biashara yako mwenyewe ndio inakufanya usalimike kama umeshindwa kujilipa?

Nakumbuka tu msemo tuliouzoea kuwa usichanganye mtaji wa biashara yako na matumizi yako ya kawaida. Huo tulipewa mwiko toka nikiwa na miaka 10 nikisimama dukana kwa mjomba.
 
Ukikopa halafu ukaenda kuzitumia kunyonya nchi za watu ukapata mara mbili basi wewe utakuwa na akili. Ila ukikopa halafu ndege zako baadae zikakamatwa sijui hapo inakuwaje
Dah mr Q imekuaje umekula ban?
 
Shida yako ni kwamba umekurupuka tu kuandika Topic bila kuijua Marekani kwa kina, Kwanza Marekani inadaiwa na nchi gani?
Na Kama ni Benki ya Dunia basi hilo siyo Deni,bali Marekani ilijikopa yenyewe,kwa sababu Benki ya Dunia ni Taasisi ya Marekani yenyewe ili kuikalia Dunia kiuchumi
Sikukurupuka. Ila katika uchumi hata topic moja sijawahi kusoma mahala panaposema ukijikopa mwenyewe, ndio una unafuu. Tena hii kiuchumi ni mbaya sana, maana ukilegeza kamba ukidhani ni fedha yako ndio unakwenda kufilisika kabisaaaaaaa.

Kuwa muangalifu kama nawe unafanya hivyo katika familia yako.
 
Na bado mtawaomba wasaidie bajeti yenu
 
😁😁😁 kuna mkatoliki mmoja humu hataki kuambiwa ukweli kuwa dhehebu lake limeingiliwa na mashoga akanipiga ban
Pole sana! Sijui unaweza kukata Rufaa! Maana hii kesi utashinda kwa 100%.
 
Na bado mtawaomba wasaidie bajeti yenu
Hili neno msaada toka kwa bepari liangaliwe upya. Kwa kawaida pepari hatoagi msaada, kwani kila anachotoa utalipa kwa namna moja au nyingine. Ila wanajisikia fahari kutumia neno msaada.
 
UONGO,
Hakuna nchi inaweza kukubali kurudi kwenye barter trade karne hii.
Zipo nchi zinafanya biashara hiyo, hasa kwa wale walio wekewa vikwazo vya uchumi. Iran isingeweza ku-survive bila hiyo biashara.
Wala si vigumu sana kama unavyofikiri.
 
Back
Top Bottom