Deni la Marekani ni $34 trillioni

Kwanza ndio nchi ya kwanza duniani kwa kutoa misaada .........hakuna kama marekani............akisema sitoi misaada miezi 6 tu anakuwa adaiwi hata nukta
kwani misaada anatoa bure? Ukiona anatoa misaada nchi fulani ujue kunakitu anagain in return,au kunajambo lake anataka litekelezwe kutoka kwenye hiyo nchi kama ushoga, marekani hana misaada ya bure nandio maana nchi anazoshindwa kupata anachokitaka kwa mgongo wakutoa misaada hutumia nguvu zakijeshi ili tu apate anachokitaka!
 
Haelewi Hakuna free lunch kwa mzungu
 
Shida yako ni kwamba umekurupuka tu kuandika Topic bila kuijua Marekani kwa kina, Kwanza Marekani inadaiwa na nchi gani?
Na Kama ni Benki ya Dunia basi hilo siyo Deni,bali Marekani ilijikopa yenyewe,kwa sababu Benki ya Dunia ni Taasisi ya Marekani yenyewe ili kuikalia Dunia kiuchumi
 
Marekani inadaiwa na nchi nyingi
China inamdai matrillioni

 
Kama siyo Raslimali,madeni ni mkojo?
Acha kujitoa ufahamu kisa unaichukia Marekani

Mimi naongelea kiutaalam, siyo kihisia, kihusuda au huba.
Sijui kama unafahamu kitu (National Accounts) Balance Sheet.
 
Halafu wanakimbilia kuomba visa nchi inayokaribia kufilisika! Pathetic!
Hapo umesema. Tatizo la binadamu huangalia ya leo tu, ya kesho yatajulikana kesho.

Pengine na wao wanakwenda ili kuifilisi Marekani kwa haraka, waondoke na chao wawaache wenye nchi watupu.
 
Hii ni hatari, ndio maana wanbembelezana. Mara Taiwan, mara ndege na maputo ya ujasusi. Lakini s-power akiwaza inabidi amwite Chini na wakae kitako kuzungumza.
 
Funding of wars across the world ndio imechangia kiasi kikubwa
Nani alimlazimisha afanye hivyo, si uroho wake tu.

Na bado! Wajanja wanampigia hesabu za mbali sana na rahisi kweli kweli kama nitavyoziainisha hapa chini:
  • Kadodoswa Ukraine- USA kaingia kichwa kichwa
  • Baada ya miaka 2 ya Ukraine, Israel ikaguswa- Huku sijui niseme kaingia pua pua - maana hata Ukraine ikasahaulika
  • Yajayo ktk mahesabu ni mazito - Taiwan baada ya miaka 2 anaingizwa tena
  • Bwana kiduku naye anamsubiri, haishi kufanya majaribio ya makombora na kuzitikisa Korea kusini na Japan. Huko nako kunamsubiri baada ya mia 4........
  • Endelea kuhesabu mwenyewe ila usimsahau Iran na ............
 
Na Marekani ndiye mchangiaji mkubwa wa bajeti za mashirika yote ya UN.
Trump Alishastuka, alilalama sana kwenye hilo. Mbeleni msitegemee tena hayo, kwani uwezekano wa bwana yuleee kurudi white house ni mkubwa.
 
Una CPA?
 
Ngoja nasi tuchapishe. Kwa maana tumewaiga kuwa mabepari, hivyo hata hilo nalo litawezekana.

Deni la US liko kwa sarafu yao dollar
Tanzania deni letu liko katika sarafu ya dollar, anachofanya Mmarekani anajikopesha mwenyewe na kujilipa. Ndomana tunasema economics hoax
 
Deni la US liko kwa sarafu yao dollar
Tanzania deni letu liko katika sarafu ya dollar, anachofanya Mmarekani anajikopesha mwenyewe na kujilipa. Ndomana tunasema economics hoax

Baada ya kushtukia hilo, Gadaffi alisema mafuta ni madini, yatauzwa kwa wateja wao, hususan Marekani kwa kubadilishana na madini kama dhahabu. Baada ya beberu kuu kuona hilo, akaona kiama chake kimefika. Akaona bora amuwaishe huyo mwamba Gadaffi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…