CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
Deni la Serikali ya Tanzania viashiria vinaonesha ni stahimilivu na ni tulivu kwa wigo unaokubalika kimataifa kwa kipindi kifupi, cha kati na kirefu hivyo kuweni na amani,
" Hakuna kama Rais Samia "
Deni la Serikali kwa mujibu wa Ripoti ya Hali ya Uchumi ya Taifa iliyotolewa mwezi Jun 2021 na Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba Bungeni Jijini Dodoma ilionesha deni la Serikali kuwa ni Jumla ya Tshs 60.9Trilioni au $27.7BL huku deni la nje likiwa ni Tshs 43.7trilioni au $20BL na deni la ndani likifikia Tshs 17.3trilioni au $8BL,Rais Samia Suluhu tayari kwenye bajeti yake ya kwanza tu ya 2021|22 ameshatenga Jumla ya Tshs 10.66trilioni sawa na 18% ya deni lote la Serikali kwaajili ya kulipunguza deni hili nihakika nchi yetu iko kwenye mikono Salama sana ya Rais Samia Suluhu Hassan
Lazima tufahamu yakuwa deni letu hili la TZS 60.9trilioni au $27.7BL ni Stahimilivu na Nihimilivu kwa mujibu wa vigezo vya Kitaifa na Kimataifa,Kwamujibu wa Uchambuzi uliofanywa mwishoni mwamwaka Jana na watu kutoka nje haya hapa yalikuwa matokeo ya Uchambuzi wao kuhusu deni letu la Serikali
A. JE! VIASHIRIA VYA USTAHIMILIVU WA DENI LA SERIKALI UKOJE?
1. Uwiano wa Deni la Serikali kwa Pato la Taifa (GDP) tumekopa na kufikia 27.9% huku ukomo Kimataifa ukiwa ni 70% maana yake bado iko fursa|nafasi ya kukopa 42.1% zaidi kwa lugha rahisi hata nusu ya kigezo hatujavuka
2. Uwiano wa deni letu la nje kwa Pato la nchi (GDP) tumekopa na kufikia 17.3% huku ukomo wa juu Kimataifa ukiwa ni 55% kwa lugha nyepesi bado iko room|fursa ya kukopa 37.7% zaidi yaani hata nusu ya kigezo hatujavuka
3. Uwiano wa deni la nje kwa mauzo ya nje tumefikia 113.2% huku ukomo ukiwa ni 240% yaani bado iko room|fursa ya kukopa 126.8% zaidi maana yake hata nusu kigezo hatujavuka,
B. JE! UWEZO WETU KAMA TAIFA KULIPA DENI HILI IKOJE?
1. Uwezo wetu wa kulipa deni la nje kwa mapato ya ndani ni 13.7% wakati ukomo ni 23% maana yake bado tuna nguvu ya 9.3% zaidi ya kulipa deni,
2. Uwezo wa kulipa deni la nje kwa mapato ya nje ni 14% huku ukomo ukiwa ni 21% bado iko nafasi ya 7% zaidi ya nguvu yetu katika marejesho
Tukiwa na Rais Makini kuwahi kutokea Mhe Samia Suluhu Hassan na Kwa viashiria hivi bado kama nchi tunao uwezo|nafasi ya kukopa zaidi ya marambili ya tulivyokopa na bado mambo yakasalia kuwa sawa sawa
Deni letu ni stahimilivu sana ila siku mkisikia limefikia zaidi ya Tshs 120trilioni kwa Pato hili hili la $66BL hapo karibisheni mashaka na hofu ndani yenu ila kwa sasa kuweni na amani pengine kuliko wakati wowote wa uwepo wenu hapa Tanzania kwani mnae Mama Samia Suluhu Hassan shujaa wa Africa