Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,884
- 21,175
Hizi ni pesa nyingi sana. Nyingi mno. US ina watu kama milioni 350 na inadaiwa dola Trilioni 40. Afrika nzima ya watu 1.4 bilioni inadaiwa kama trilioni 1.5 tu. Nchi inaweza kukopa hela zote hizo na isiendelee kweli? Hayo mahela yanajenga vitu vingi mno. Barabara, bandari, hospitali, shule na vyuo, reli nk.
Huwa tunadhani Afrika tumeachwa nyuma sababu tunauwezo mdogo kumbe ni sababu wenzetu wana mikopo mikubwa(Ambayo kimsingi ni wanachapisha pesa tu)
Afrika pamoja na ufisadi na ujinga wetu lakini tungekuwa na USD trilioni 40 kwa miaka 50 iliyopita leo hii tungekuwa mbali sana. Trilioni arobaini inajenga barabara, reli na mitambo ya kufua umeme kutoshea bara zima.
Nchi kama UK ina deni la USD trilioni 4. Zaidi ya mara mbili ya Afrika nzima. Ufaransa deni lao ni 4 trilioni na ushee. Japan wanadaiwa 9 trilion.
Leo hii Tanzania tunadaiwa kama dola bilioni 50. Deni la Uingereza ni kubwa mara 80 yetu! Pamoja na ujinga na ufisadi wetu, tungekuwa na access ya kukopa kufikia dola trilioni 4 hakika tungekuwa mbali sana.
Mytake: Madeni(uwezo wa kuchapa pesa kwa kiwango kikubwa) ndiyo hasa kilichofanya nchi za magharibi zituache maendeleo kwa gap kubwa sana. Si ufisadi wala ujinga wetu. Game iko rigged. Ni namna gani tunajinasua?